Kwa Wachumi wetu,Ni kwa nini tusitumie hela ya China kununulia bidhaa?

wakomong'we

Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
30
Reaction score
2
Ndugu wana Board,kuna vitu vinanitatizi sana kuhusu Uchumi wa dunia ulivyo kwa sasa.
Kwanza kabisa fedha ya Taifa fulani kuwa super currency wanaangalia vitu gani mfano ilivyo US $,Pound ya Uingereza na zingine nyingi.Kama moja ya factor ni uzalishaji basi nilitegemea kwa kipindi cha miaka mitatu mpaka minne ingekuwa JAPAN maana uzalishaji wa Taifa hili ulikuwa uko juu sana,Na kwa sasa ni CHINA ambapo uzalishaji wa Taifa hili uko juu sana naweza sema kwa sasa China wanazalisha kila kitu unachokifahamu kipo hapa duniani.Narudi kwenye hoja yangu ,Kwa kuwa Tanzania na Dunia nzima inanua product za China kwa nini tusitumie currency ya China (yuan) kununua na kuuza bidhaaa zetu ukizingatia kuwa Exchange rate ya fedha ya Kichina haifiki hata Tshs 300 ukibadili, ambapo US Dolla 1 = 1584 Tshs,ambapo tukitumia fedha ya China (yuan) tunaweza kununua product nyingi zaidi ukilinganisha na US $.Kwa mfano unakuta mtu anaenda China kununua bidhaa anatafuta US $, sasa kwa nini huyu mtu asitafute yuani ya China? Najua kuna swala la currency revaluation lakini hilo nafikiri halituzui kuona wapi kuna unafuu wa kuweza kununua product nyingi.
PILI, Kwa nini uingereza currency yao iko juu sana ukilinganisha na currency za nchi nyingine mfano US $,Euro,Canadian Dollar zingine nyingi? Je factor inayotumika hapa ni ipi? na Why not Tanzania?
Naomba kuwasilisha ndugu zanguni.JF is more than a school, naamini sana
 
Kwa part ya kwanza ya swali lako utajikuta ukishaexchange pesa yako from dollars to rmb itakuwa equivalent na pesa ile ile sababu hata wauzaji wa China wanapanga bei kulinganisha na fluctuations za dollars, kabla hatujaenda mbali kwanza soma hapa kuhusu mchezo wa China kushusha value ya currency yao ili kuvutia wateja (ingawa wewe ukiomba qoute in RMB utapewa bei baada ya conversion ya bei yake in dollars to RMB kulinganisha na exchange rate ya siku hio) kwahio mkuu vitu vingi vya China vipo qouted in dollars kwahio wewe hapa bongo na pesa yako ya madafu, utatoa approximately kiasi kile kile kununua huo mzigo no matter unanunua RMB, au Dollar

seeingredinchina.com/2011/10/11/what-is-currency-manipulation-and-why-should-i-care/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…