Kwa wadada hasa walio single

love has no 4mula. Ni sawa na kuwa na kiu ya maji, upewe bia, waweza hisi ahueni kama sio kiu kuisha kbs. Asante kwa siredi bidada
 
Nimetamani sana kujua kilichoandikwa, ila nimeshindwa so many words nimeskia uvivu kusoma
 
Nimetamani sana kujua kilichoandikwa, ila nimeshindwa so many words nimeskia uvivu kusoma
babe S you cant be serious. Hivi hata kusoma mtu anasikia uvivu? hapa ma dia unless kama hupend kusoma but kama unapenda mbona hiyo hafiki hata page moja ya A4? soma mamii kuna ujumbe mzuri sana.
 
Last edited by a moderator:
babe S you cant be serious. Hivi hata kusoma mtu anasikia uvivu? hapa ma dia unless kama hupend kusoma but kama unapenda mbona hiyo hafiki hata page moja ya A4? soma mamii kuna ujumbe mzuri sana.
Napenda kusoma ila honestly nimefungua tu hiyo page nikasikia uvivu, anyways umeniencourage nitaisoma thnx
 
Hili li siredi limekaakaa kikekike zaidi,Ngoja niulize kwanza!Je vidume kama sisi,hasa tulio mabikra tunaruhusiwa kuchangia?


Unaweza kuongezea hakuna shida kabisa!
 

Mamito thou mapenzi / mahusiano hayana formula ila hiyo ni kama guidelines tu.... ni kama zilivyo sheria za sehemu yoyote kuna wakati utalazimika kuvunja ila kuwan wakati utazi-apply tu iwe isiwe!
 
Kingine hiki hapa ambacho kinaweza kujenga mahusiano : Kuwa mkweli na muwazi ni moja ya misingi ya kujenga mahusiano yanayodumu na hata kukabiliana na dhoruba mbalimbali za maisha ya mahusiano ya ndoa.

1. MTAZAMO: Unapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu, pendelea zaidi kuuliza mtazamo wa mwenzako kuhusu mwenendo wa maisha yetu. Hata unapotaka kufanya jambo fulani muulize mwenzako: "Nimefikiria weekend hii twende Bagamoyo / Zanzibar wewe unaonaje?

2. MUZIKI: Ni wazi kwamba muziki unatoa ujumbe na mafundisho. Inapendeza kwa wapenzi kuwekeana nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi thabiti. Unapokuwa na mwenzako chumbani muwekee muziki laini na umwambie: "Sikia wimbo huo mpenzi wangu…tambua kwamba ni ujumbe wangu kwako."

3. MANDHARI YA DUNIA: Ukitafakari juu juu unaweza usione faida ya kutafakari pamoja mandhari zuri ya dunia, lakini mkiwa pamoja kwenye fukwe ya bahari mkitazama machweo ya jua bila shaka mtafurahia utukufu wa Mungu pamoja. Tembeleeni bustani na mbuga za wanyama pamoja.

4. MICHEZO: Ni jambo jema kwa wapenzi kucheza pamoja michezo mbalimbali, mfano karata, kuruka kamba na hata kunyang'anyana vitu, kutupiana mito na mambo kama hayo. Lengo ni kufurahi pamoja kama wapenzi.

5. MAFUNDISHO: Mpe nafasi mpenzi wako akufundishe mambo anayofahamu. "Sijui kabisa kuhusu programu hii ya kompyuta, unaweza kunifundisha mpenzi wangu?" Kufundishana hujenga msingi wa kutegemeana na kuaminiana kuhusu uelewa wa mambo.

6. ULIZA VICHOCHEO. "Mpenzi najua uko mbali na mimi lakini hebu jaribu kufikiria ningekuwa karibu yako ungependa nikufanyie nini kati ya mambo yafuatayo; kukukumbatia, kukubusu mdomoni, kukushika kiunoni?" Mchombeze mwenzako kwa maneno ya namna hiyo siyo anapokuwa mbali bali hata hata kama uko naye. Mazungumzo ya namna hiyo husisimua mwili.

7. MAVAZI YA KUFANANA: mavazi ya kufanana yahamaanishi suti, lakini hata nguo za kawaida, kwa mfano mwenza wako anaweza kuwa na traksuti nyeupe na fulana nyekundu na wewe ukavaa traksuti ya njano na fulana nyekundu, kisha mkatembea barabarani. Hakika mtapendeza na kuwa kivutio kwa watu.

8. MAJONZI: Kuna umuhimu wa kusaidiana katika maisha, lakini mwenzako anapokuwa na tatizo linalomsumbua si vibaya kama utamuuliza kuhusu msaada wako. "Pole mpenzi, lakini nimepanga kukusaidia sijui wewe unasemaje?" Wakati mwingine ni vizuri kusikia mpenzi wako akiomba msaada, kuliko kujitokeza na kumsaidia kwani inawezekana hakutegemei.

9. NDOTO: Vipi kuhusu ndoto. Umewahi kumuuliza mwenzako ameota nini usiku? Siku moja jaribu na ikiwezekana mshirikishe kile ulichoota. Kitaalamu ndoto ni wingi wa kumbukumbu zilizotunzwa akilini.

Hebu fikiria kuhusu usemi huu: "Nimeota tuko pamoja yaani nilikuwa nasikia raha sana." Bila shaka, licha ya kuwa ni ndoto lakini utafurahi kusikia ulimfurahisha kupitia njozi.

Mwanajamvi ruksa kuongeza chochote! Karibuni


 
Charminglady nimesoma kwa uchungu na masikitiko maelezo yako yote ya awali na ya hapo juu kwa sababu nimetoka kuachwa jamani last friday! yaani naumia mno...kisa? niliacha simu nyumbani kwa hiyo sikujibu sms wala kupokea calls za jamaa mpaka nilivorudi kutoka kazini! Au alikua keshajichokea anatafuta sababu?
 
somo zuri.
duh ku apply mbinu zote ni ishu sana aisee. ngoja leo nikitoka job napiga kiroba then anapokuja kunipokea wife nitamkumbatia mbele ya watu akome na vijiaibu vyake.
bhaelezeee bhaelezee
 
nasema upande wa mahusiano ndio ujibu its compliated.

sijasema wewe upo complicated mamito. mwanaume wa kukudhibiti ww

labda awe na sifa za wapenzi wangu wote ndio atakuweza. teh teh
Nilidhani mpenzi niko peke yangu, kumbe tuko wengi?
 

Pole jamani mpenzi caven dish, ndo maisha kumbuka kuwa kila jambo hutokea sababu... na huenda Mungu kakuepushia jambo fulani kwa huyo mwenzi wako, pia huenda kaona mbeleni hamtawezanana na vitu kama hivyo... Mshukuru Mungu kwa kila jambo wa kwako yupo na nina imani utampata... hata mimi niliwahi kuachwa hadi nikataka kunywa sumu ila rafiki yangu alinishauri nikaona ni ujinga cha ajabu huyo bwana akaoa mke mwingine na ninavosikia mwanaume kawa mlevi na muhuni yan hana ndoa yeney amani mkewe analalamika hadi kwa wafnyakazi wenzie na mwanaume huyuo ... pole Mungu ana kusudi na wewe!
 
Last edited by a moderator:

Thanks my dear! nitaku-PM
 
so many rules.,so many do's and dont's..it makes everything complicated and not fun anymore!!i believe one should be who she is..if you cannot be yourself and rather take on characters that are not yours-what should that tell us about you??be who you are and have fun being you..some one worth you will come along..and you wont have to hide your true self to be happy..
 
Mabinti kuweni makini..si kila cheupe ni teluji,hata chokaa pia ni nyeupe...
Namaanisha sio kila mtazamo unafanya mabadiliko...
 
Napenda kusoma ila honestly nimefungua tu hiyo page nikasikia uvivu, anyways umeniencourage nitaisoma thnx
babe S, wala hakuna hata..pm me nitakuhadithia....
 
Last edited by a moderator:

umesema vyema mjumbe.....some ones true colour can not be hiden forever.....kama we ni mwehu ni mwehu tu....
 
Ushauri mzuri sana. Ila una washinda wengi sana. Kama unavyojua mapenzi ni kikohozi.
 

Pole sana mama,kuachwa si mchezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…