Kwa Wadada/Ladies/Wanawake/Wamama tu

Kwa Wadada/Ladies/Wanawake/Wamama tu

Kindred Spirit

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
260
Reaction score
375
Jinsi ya Kutunza Ngozi yako (Ushauri wa Bure)

Unajua ilivyo kazi kubaki na mwonekano mzuri wa ngozi throughout. Mara chunusi, mara ngozi kavu kama ya mamba, mara ngozi haina nuru yaani ile rangi yako halisi haionekani.

Ni hivi, utunzaji wa ngozi unahitajika ili ubaki au uboreshe mwonekano wako. Nakuwekea list ya mambo ya msingi kuzingatia na interval katika hiyo skin care routine.

1. Hakikisha unasafisha uso kabla ya kulala, most importantly unaoga kabla hujaenda kulala. Usiruhusu makeup yako ilale usoni mwako hakika unakaribisha bacteria watakaoshambulia ngozi na kukuletea chunusi. Pia badili mashuka at least mara kwa mara.

2. Kila wiki fanya scrub. Dead skin inahitajika kufanyiwa exfoliation ili itoke badala ya kuganda juu ya ngozi hai. Scrub nyingi hasa zile za apricot zinafanya kazi vizuri. Epuka lightening scrubs.

3. Tumia cream/lotion inayokufaa. Si mbaya kufanya majaribio mara kadhaa kujua product inayofaa ngozi yako, them maintain hiyohiyo. Zaidi ya yote tumia product halisi. Hizi za ki-tz, Uturuki au China sikushauri. Hawa wanatia lightening products au cheap products ambazo hata hazina ushirikiano. Products za West Africa, South Africa, Ulaya na Marekani ni genuine. Nunua products original kidogo kidogo si vitu vya kuisha mara moja.

4. Kunywa maji mengi. Mfano lita 1 kwa siku kidogo kidogo ni bora kuliko kunywa yote kwa wakati mmoja. Hydrated your skin slowly, water is magical.

5. Unaposafisha usisugue uso wako kwa nguvu. Kwa kufanya hivyo unadisturb layer ya mafuta chini ya ngozi yanapanda kwenye pores na kukutana na bacteria then chunusi zinatokea.

6. Ukiwa na chunusi acha iive hadi ikauke yenyewe. Yaani siku unaibinya inatoka ikiwa solid. Kama imevimba au inauma huo siyo muda wa kuitoa, hakikisha imekauka kabisa. Kubinya au kutoboa chunusi ambayo haijakauka kunasababisha makovu utakayosumbuka sana kuyaondoa.

7. Tumia sunscreen au foundation/powder. Hizo zote zinapunguza effect ya jua directly kwenye ngozi na kuzuia ngozi kuzeeka haraka au kusinyaa na kufifia. Kila mmoja ana ngozi ya mng'ao hivyohivyo ulivyo. Avoid sun rays! Again hakikisha products ni OG.

8. Fanya mazoezi. Kazi/mazoezi yoyote inayofanya usweat inasaidia sana kuondoa blackheads na kufanya ngozi ing'ae, ndo maana mtu akiwa mikoa ya pwani ngozi inakuwa nzuri tofauti na mkoani, humidity inafanya mtu asweat hata katika micro level matokeo ni ngozi murua.

9. If you can, tumia serum every night, na retinol once a week. Hizi zina healing effect kwenye ngozi. Otherwise let your skin breath usiku usipake kitu. Mara 2 au 3 usiku gently futa ngozi yako kwa kutumia cleanser na pamba. Step hizi zote zitakufanya uonekane na ngozi ya kitajiri (Advanced skin care, siyo lazima)

10. Kula vyakula rafiki wa ngozi. Mfano matunda hasa yenye uchachu uchachu kama vile orange, pia mbogamboga na karoti na upunguze soda, na junk food (advanced skin care, siyo lazima as inategemea na kipato).

11. Tumia same products mwili mzima. Except usiku mfano unaweza kutumia oil miguuni na serum usoni. Ila mchana paka product same mwili mzima then kama unaongeza oil au petroleum jelly au miguuni that's right. Hii itasaidia uwe na same tone mwili mzima.

12. Katika kila lotion au cream, usisahau kuongeza glycerin. Ni product rafiki sana wa ngozi ila usiipake peke yake itakuunguza.

Sharing is caring....
 
Back
Top Bottom