Kwa wadada wenzangu: tuwe makini na aina hii ya wanaume.......

Kwa wadada wenzangu: tuwe makini na aina hii ya wanaume.......

Dunia ina changamoto nyingi sana sio kwa wanawake tu bali hata wanaume japo wanaume hawa semi yanayo wakuta hadharani. Nakubaliana na ushauri wako japo unaweza kuwasaidia zaidi wanawake ambao walio na elimu na wenye uwezo wa kusimamia maisha yao bila utegemezi. Sehemu kubwa ya wanawake katika jamii yetu wameathiriwa na mfumo dume ambapo sehemu kubwa ya uchumi unamilikiwa na wanaume. Kutokana na mfumo huo sehemu ndogo ya wanawake wamebahatika kupata elimu nzuri na kumiliki uchumi na hawa kwa kiasi kikubwa wanapatika mijini. Baadhi ya wanaume katika jamii wanatumia matatizo ya kiuchumi na ya kijamii kuwadanganya wanawake kwa kutumia kigezo cha mahusiano na ahadi hewa lakini hawawahitaji kwa malengo yenye manufaa. Elimu ndio ukombozi wa wanawake katika nyanja zote kimapenzi na kiuchumi, hata mataifa yaliyoendelea wanawake wanathaminiwa kwa sababu wanamiliki uchumi na sio tegemezi kwa jamii ya wanaume hivyo anakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi anayo yaona yeye ni sahihi katika maisha yake.

Siku zote unanibariki kwa michango yako....asante kwa analysis ya kisomi na yenye utafiti wa ukweli sana....Mungu akubariki....nafikiri imetosha kwa mawazo yako kufunga hii thread.....
 
Kwa wadada wenzangu....wanasema experience is the best teacher....leo tu share experience na tupeane ushauri......

Wengi wetu tutakuwa tumekutana na wanaume ambao mimi ninawaita wanaume malengo ya mbele na wanaume waharakisha mambo na wanaume maneno.....

Mwanaume ya malengo mbele ni Yule ambaye kupitia maneno yake anakujengea picha ya baadaye ili apate mahitaji yake ya sasa.Yeye anakujengea picha ya nyie mkiwa na familia yenu,watoto,ndoa nzuri,mkienda matembezi pamoja mwisho wa mwaka nk....hii yote ni ili kukujengea picha kuwa wewe ni sehemu ya maisha yake na kwamba kila analoliwaza analiwaza kulifanya akiwa na wewe siku za mbeleni.
Kwa furaha wanawake walio wengi huwapokea wanaume wa aina hii kwa mikono miwili na wengine wetu huenda hata kutoa sadaka maombi yetu yamejibiwa na kuanza kuwaweka maanani aina hii ya wanaume......

Wanaume waharakisha mambo ni wale ambao wana haraka sana utafikiri wanakimbizwa na moto...hawa ni wale unakutana nae na mara moja anahakikisha umekuwa nae karibu sana kwa wakati mfupi....anahakikisha huoni wala huzifahamu tabia zake chafu.hawa tofauti na wanaume malengo mbele,kwa muda mfupi sana wanahakikisha umewaweka kwenye akili yako,kila saa wanapiga simu,wanaandika message,wanataka kuwa pamoja nawe kila saa,wanakutambulisha kwa ndugu wale kama binamu,mpwa na si wazazi na marafiki zao,wanakupa funguo za nyumba zao na ujanja mwingine wa aina hiyo.
Hawa wanajenga hisia za msichana kwao haraka na wanataka muwe na uhusiano wa kimapenzi haraka.....
Kwa akilo ya kawaida utajiona hakuna kama wewe hapa duniani na una bahati sana,ila baada ya muda mfupi sana watakuliza vibaya walio wengi.

Wanaume maneno.....hawa ni wanaume wazuri sana kwenye kusema...yaani anaweza kuahidi kila awezacho na atakujengea mazingira ya kuamini anaweza kufanya hivyo....ila hawatekelezi na hawana uwezo huo wa kufanya hivyo ,na wengine hata kama wanao uwezo hawafikirii ndani ya roho zao kufanya hivyo,wanaahidi wapate wakitakacho........

Ushauri wangu sasa:

1.Wasichana tuwe makini na tuchukue muda kuwafahamu wanaume wanaokuja kutaka mahusiano na sisi....haraka haraka haina baraka.....mtu hata jina lako la pili halijui anakuahidi ndoa sijui nini....tuweni makini....there is no fire,you do not have to rush kutoa akili.moyo na mwili wako kwa mwanaume usiyemfahamu vizuri. Kile kipindi cha dating tukitumia vizuri kuwasoma na kuwafahamu wanaume...na si wakati wa dating umeshatoa mwili na akili yako na hata moyo wako.....open your ears and eyes and intelligency 100% and not your legs.

2.Tuache tabia ya kuamini ovyo,mtu anakuahidi hiki hafanyi,kile hafanyi....he does not keep promises....wewe nawe umo tu unaendelea nae ukiamini atabadilika au amesahau au unaogopa kumuuliza.....mtu anayekupenda atatenda lile alisemalo kwa wakati,na kama atashindwa utakuwa wa kwanza kujua sababu na zitaeleweka......tuwe wakali kidogo na tuhoji....unamuogopa oh,nikimuuliza ataniacha,kama ni wakukuacha atakuacha tu.

3.Tukubali kuwa tumedanganywa na tuwe wajasiri wa kusonga mbele.Mara kibao unasikia msichana anasema najua ananidanganya ila sasa nifanyeje ndo nimeshalala nae,nimezaa nae,siwezi muacha,tutabanana hapo hapo hadi anioe.....we si wa kwanza kudanganywa,kaa chini lia kama inakubidi,fikiria ulivyodanganywa na ukadanganyika na jifunze then tulia kwa muda na chukua uamuzi wa kuondoka kwenye utumwa wa kosa la kudanganyika then songa mbele kwa kujiamini,kuwa makini na kumuomba Mungu kwa sana.

Ni hayo tu,.....nawapenda wote na nawatakia wikiendi njema.
ulipokuwa na hashycool ulikuwa unaongea ma pumba tu, tangu ukuwe close na mimi sku hizi unaongea ma pointi ya kufa mtu. dah! kweli ukikaa na klorokwini lazima utashine tu. bandiko limetulia

bek to ze topik: mbona waaminifu hatupo katika bandiko lako? unatubagua ujue
 
Da Michelle lazima utakua una degree ya Education tu japo sielewi kama ni yapale UDSM au lah!!!!

Nimekusoma, nimekuelewa!! Big up ma sis!! umenipigisha hatua, na kunitia moyo pia

that's why i lov u!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
I SALUTE YOU KLORO....kweli umefanya kazi ya ziada....jamani Hashy...u wapi???
 
Ha ha ha ha ha......thank you Susy

You know i love you even more, i hope you are doing well on that matter....mi wish to hear from you!!!

Enjoy your weekend!!!
 
Hii ni maalumu kwa tunaotakiwa kuwaogopa! We ukiwa mmoja wapo!
baba mchungaji yupo around, nitakuPM baadae kuhakikisha hauna tatizo lolote. ni kwa nia njema tu. dini zote zinahubiri upendo.
 
I SALUTE YOU KLORO....kweli umefanya kazi ya ziada....jamani Hashy...u wapi???
hashy ni mwanaume malengo mbele. alimzuga mdada wa watu anafanya Sheraton , majuzi amefumwa na mdada anachimba vyoo uswahilini, kwavile mdada ni memba wa JF, hashy anaiogopa JF kuliko tripoli libya
 
hashy ni mwanaume malengo mbele. alimzuga mdada wa watu anafanya Sheraton , majuzi amefumwa na mdada anachimba vyoo uswahilini, kwavile mdada ni memba wa JF, hashy anaiogopa JF kuliko tripoli libya

:A S 13::A S 13: Uongo mbaya sana....sasa ananipoteza na mimi jamani? ila bado nampenda na U-plumber wake.....:rain:
 
:A S 13::A S 13: Uongo mbaya sana....sasa ananipoteza na mimi jamani? ila bado nampenda na U-plumber wake.....:rain:
behind every keyboard there is a mystery hiding . by klorokwini

bek to ze topik: nikiread btn them lines umesema unaongea from eksperiens, ina maana ushatendwa na wote hao? i mean , malengo mbele , waharakishaji a.k.a vodafasta na maneno mengi? ukijibu suala hili litafatia suala la nyongeza
 
ndiyo wameshanitenda....
 
ndiyo wameshanitenda....
sasa ningeomba unieleweshe hivi malengo mbele unamjuaje? sababu kila nikiangalia naona lazima tuweke malengo ndio mambo yatokee. sasa baada ya sredi hii utasababisha nikimpa malengo lizzy , yeye ataniona mimi ni malengo mbele tu wakati kumbe mimi niko serious. naomba ufafanue hii ili kuweka sawa lizzy asije akanielewa vibaya nikimpa malengo yangu serious
 
malengo mbele ni yule ambaye hata kabla hajakufahamu jina ashakuambia atakuoa.....yaani yeye haitaji kukufahamu kukupa iyo ahadi....ila ukikosea ukampa mzigo....safari ndo inakuwa imeanza....l.o.l......kama Lizzy,yabidi uwe makini....she is smart....take your time to know her well,make her your friend and you can talk.....si mnakutana club tu unataka one night stand unaanza na promise za ndoa na watoto....umenielewa sema unajidai tu kusumbua kichwa changu na kimechoka.....!!!
 
nimekuelewa sasa, nani kachokesha kichwa chako nimpoteze katika ramani ya ulimwengu? unajua mimi naweza kuvumilia watu wote kukerwa hapa JF lakini sio wewe. naomba unipunguze hasira kabla sijachukua uamuzi mbaya
 
wewe ndo umenichokesha...:rain:
 
baba mchungaji yupo around, nitakuPM baadae kuhakikisha hauna tatizo lolote. ni kwa nia njema tu. dini zote zinahubiri upendo.

Ndo maana nakupenda Kloro kwasababu unajali!Ngoja nikupe kabisa mahitaji yangu uje nayo PM!Mchele kilo 10...mafuta lita 5...Nyama kilo 2, ya ng'ombe tafadhali..Vitunguu na viazi kisado na nyanya debe!Oh bila kusahau soda 5 za jumapili!
 
naomba utafautishe baina ya mpenzi na waiter. khaa! na ma vitunguu tena?
 
Hehehe dearest mpe somo huyo asidhani usanii haujulikani!
 
Back
Top Bottom