Kwa wadau wote wa jamii forums

Kwa wadau wote wa jamii forums

Hivi umeisoma hiyo taarifa yote au umepitisha macho kwenye kichwa cha habari? Soma tena uelewe chakula kipo, maghala ya serikali yana chakula. Hakuna Mtanzania ata kufa kwa njaa. Tanzania sio Kenya.

Number of Kenyans going hungry doubles to three million

Halafu kinacho shangaza, mnalalamika hakuna mvua ndio maana na chakula hakitoshi, mbona mauwa chai na kahawa mnalima kwa nguvu zote na huku kuna ukame??

Cha masingi watu wenu wanaishia kula viwavi tena kwenye mji mkuu, hayo mengine ya chakula kujaa kwenye ghala ni blabla ambazo mwenye anakula viwavi hajui na haimsaidii.

Kenya, kwa sababu ardhi yenye rotuba ni kidogo, hivyo tunaona bora ukulima wa mimea yenye faida kubwa halafu tutumie hizo hela kwenye kununua mahindi na bidhaa zingine. Kuna nchi nyingi tu ambazo hufanya hivyo, sio lazima kila mtu apande mahindi.
Njoo Kenya uone kuna mtu mwenye ekari tano tu, lakini anafanya ukulima wa kisasa wenye aina ya mimea na mazao yenye faida ya kumzidi aliyepanda mahindi kwenye ekari hamsini.
Cha msingi ni kutumia akili, basi.
 
DAmNTqOWsAAZDN3.jpeg
 
mwenye macho haambiwi tazama. hivi huoni waKenya walivyopiga hatua? tuwape heshima ndugu zetu waKenya kwa kuwa mfano mwema Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla
Unajiita Lewis254, 254=Code ya Kenya.

Halafu unasema "...tuwape heshima ndugu zetu waKenya..." Haujui kwamba hilo jina tu linaifanya komenti yako kua kipande cha upuuzi?
 
fuata mada kijana.
 
Cha masingi watu wenu wanaishia kula viwavi tena kwenye mji mkuu, hayo mengine ya chakula kujaa kwenye ghala ni blabla ambazo mwenye anakula viwavi hajui na haimsaidii.

Kenya, kwa sababu ardhi yenye rotuba ni kidogo, hivyo tunaona bora ukulima wa mimea yenye faida kubwa halafu tutumie hizo hela kwenye kununua mahindi na bidhaa zingine. Kuna nchi nyingi tu ambazo hufanya hivyo, sio lazima kila mtu apande mahindi.
Njoo Kenya uone kuna mtu mwenye ekari tano tu, lakini anafanya ukulima wa kisasa wenye aina ya mimea na mazao yenye faida ya kumzidi aliyepanda mahindi kwenye ekari hamsini.
Cha msingi ni kutumia akili, basi.
Unarudi kule kule nilikoanza mwanzo "mnauza kuku kununua mayai". Huko kwenu Kenya ni bora kumpedezesha tajiri anayeshikilia ardhi kuliko kumpa chakula cha kutosha mwananchi wa kswaida.

Hao unao wazungumzia wa Dodoma walisha shughulikiwa siku ya pili tu baada ya habari kuchapishwa.

Linganisha tarehe katika hizi taarifa mbili. Tanzania sio Kenya
Wala viwavi jeshi kuikabili njaa

Chamwino yapata msaada wa Chakula | East Africa Television
 
mwenye macho haambiwi tazama. hivi huoni waKenya walivyopiga hatua? tuwape heshima ndugu zetu waKenya kwa kuwa mfano mwema Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla
Heshima unayoongelea ya vipi inayotakiwa kupewa kwa Kenya?
 
Unarudi kule kule nilikoanza mwanzo "mnauza kuku kununua mayai". Huko kwenu Kenya ni bora kumpedezesha tajiri anayeshikilia ardhi kuliko kumpa chakula cha kutosha mwananchi wa kswaida.

Hao unao wazungumzia wa Dodoma walisha shughulikiwa siku ya pili tu baada ya habari kuchapishwa.

Linganisha tarehe katika hizi taarifa mbili. Tanzania sio Kenya
Wala viwavi jeshi kuikabili njaa

Chamwino yapata msaada wa Chakula | East Africa Television

Sijatoka huko tulikoanzia, wewe ndiye unayumba yumba. Sio ajabu kumuuza kuku ili ununue mayai, inategemea na soko lilivyo na kama una akili na ujanja wa kilimo biashara.

Kaka Tanzania yenu hadi mfikie kula viwavi kwemye mjii mkuu lazima mlipitia pagumu, hayo mengine nimekwambi ni blabla za reactionary leadership, eti hadi pale wanahabari wataangaza shida za njaa ndio mnakimbiza mahindi huko kwenye nchi kubwa hiyo yenye rotuba.
Kuna wengi sana ambao hawajafikiwa na vyombo vya habari, ripoti ya Twaweza imeonyesha asilimia 84% ya Watanzania wamekumbwa na uhaba wa chakula halafu unaleta blabla za kukimbza kimbiza mahindi pale vyombo vya habari vimeangaza
Uchungu wa Njaa: Upungufu wa chakula Tanzania :: Machapisho :: Twaweza.org
----------------------------------------------------------------------------------------------------------

Idadi kubwa ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wameripoti uhaba wa chakula katika maeneo wanayoishi. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 84 wameripoti uhaba wa chakula ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo ya mijini.

Zaidi ya nusu ya kaya za Tanzania (yaani asilimia 69) zinahofia kuishiwa chakula. Aidha asilimia 51 ya kaya zimeripoti kwamba hakukua na chakula cha kutosha kulisha kaya nzima, au mwanakaya ameshinda na njaa kwa sababu hakuweza kupata chakula (asilimia 50).

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika muhtasari uitwao Uchungu wa njaa: Upungufu wa chakula Tanzania. Muhtasari huu umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia njia ya simu. Takwimu za muhtasari huu zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania bara (Zanzibar haikuhusishwa kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 14 na 26 mwezi wa tisa, 2016 na kutoka kwa wahojiwa 1,610 kati ya tarehe 9 na 15 mwezi wa pili 2017.

Kwa mujibu wa wananchi wengi, uhakika wa kupata chakula umepungua kati ya mwezi Septemba 2016 na Februai 2017: Mwezi wa pili 2017, asilimia 65 ya wananchi walikuwa na hofu ya kaya zao kukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na asilimia 45 waliosema hivyo mwezi Septemba 2016. Mwezi Februari 2017, asilimia 51 ya wananchi waliripoti kwamba kuna wakati hawakua na chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Kabla ya hapo, mnamo mwezi Septemba 2016, asilimia 43 ya wananchi iliripoti kwamba hali kama hiyo iliwatokea katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita. Mwezi Februari 2017, asilimia 35 ya wananchi waliripoti kuwa na mwanakaya angalau mmoja alieshinda na njaa siku nzima kwa sababu ya kukosa chakula katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Hili ni ongezeko kutoka asilimia 21 walioripoti kwamba hali hiyo iliwatokea katika kipindi cha miezi sita tangu Aprili mpaka Septemba 2016.

Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kwamba bei ya mahindi (halisi, jumla) imeongezeka mara mbili (baada ya kuirekebisha na kiwango cha mfumuko wa bei wa wakati huo) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutoka shilingi 400 kwa kilo mwanzoni mwa 2015 mpaka shilingi 852 mwezi wa kumi na mbili, 2016. Wahojiwa wa Sauti za Wananchi wameripoti kwamba kwa wastani kilo moja ya mahindi inawagharimu shilingi 1,253. (Bei zilizoripotiwa kwenye masoko ya ndani).
 
Sema mahindi tu. Ni chakula gani tena tunaagiza!
Kwa nini tuagize mahindi wakati tuna maziwa kibao tunaweza fanya irrigation ambayo wenzetu hawawezi. Lake tanganyika, Victoria, nyasa, Rukwa, maziwa madogo kama Eyasi, Ikimba, Singidani, Burigi sijui nitaje mangapi na hapo mito kibao eti tunalia njaa?? Si hilo tu, watu wetu wanaotoka Arusha ndo walikuwa mabingwa duniani enzi za mwalimu, kulitokea nini mpaka riadha tukafutika, ndondi, mipira ya vikapu. Ona wacheza mipira wa Kenya na wacheza sinema wanavyong'ara huko kenya ina maana unadhani ili ujulikane unahitaji siasa?? Watu tunapata shida kujieleza tunatoka wapi. Ukisema Tanzania wanauliza Tasmania? unasema no, wanauliza where inabidi useme south of Kenya and Uganda. Hapo ndo watu wanaanza kutafuta ramani wajue hii tasmania ups Tanzania ipo wapi. Jamani Tunapata shida wenzenu kujieleza ila hatukati tamaa nchi yetu penzi tunaitangaza. Huku nilipo wenzetu wanapata visa kwenye mtandao lakini nchi yetu hata haimo. Wakenya na waganda kibao wanafundisha, wengine mamanager kwenye makampuni makubwa duniani wengine wanacheza mipira kama wanigeria. WaTz mpaka uwe UN ndipo ufike nchi nyingi.
 
Sijatoka huko tulikoanzia, wewe ndiye unayumba yumba. Sio ajabu kumuuza kuku ili ununue mayai, inategemea na soko lilivyo na kama una akili na ujanja wa kilimo biashara.

Kaka Tanzania yenu hadi mfikie kula viwavi kwemye mjii mkuu lazima mlipitia pagumu, hayo mengine nimekwambi ni blabla za reactionary leadership, eti hadi pale wanahabari wataangaza shida za njaa ndio mnakimbiza mahindi huko kwenye nchi kubwa hiyo yenye rotuba.
Kuna wengi sana ambao hawajafikiwa na vyombo vya habari, ripoti ya Twaweza imeonyesha asilimia 84% ya Watanzania wamekumbwa na uhaba wa chakula halafu unaleta blabla za kukimbza kimbiza mahindi pale vyombo vya habari vimeangaza
Uchungu wa Njaa: Upungufu wa chakula Tanzania :: Machapisho :: Twaweza.org
----------------------------------------------------------------------------------------------------------

Idadi kubwa ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wameripoti uhaba wa chakula katika maeneo wanayoishi. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 84 wameripoti uhaba wa chakula ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo ya mijini.

Zaidi ya nusu ya kaya za Tanzania (yaani asilimia 69) zinahofia kuishiwa chakula. Aidha asilimia 51 ya kaya zimeripoti kwamba hakukua na chakula cha kutosha kulisha kaya nzima, au mwanakaya ameshinda na njaa kwa sababu hakuweza kupata chakula (asilimia 50).

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika muhtasari uitwao Uchungu wa njaa: Upungufu wa chakula Tanzania. Muhtasari huu umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia njia ya simu. Takwimu za muhtasari huu zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania bara (Zanzibar haikuhusishwa kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 14 na 26 mwezi wa tisa, 2016 na kutoka kwa wahojiwa 1,610 kati ya tarehe 9 na 15 mwezi wa pili 2017.

Kwa mujibu wa wananchi wengi, uhakika wa kupata chakula umepungua kati ya mwezi Septemba 2016 na Februai 2017: Mwezi wa pili 2017, asilimia 65 ya wananchi walikuwa na hofu ya kaya zao kukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na asilimia 45 waliosema hivyo mwezi Septemba 2016. Mwezi Februari 2017, asilimia 51 ya wananchi waliripoti kwamba kuna wakati hawakua na chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Kabla ya hapo, mnamo mwezi Septemba 2016, asilimia 43 ya wananchi iliripoti kwamba hali kama hiyo iliwatokea katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita. Mwezi Februari 2017, asilimia 35 ya wananchi waliripoti kuwa na mwanakaya angalau mmoja alieshinda na njaa siku nzima kwa sababu ya kukosa chakula katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Hili ni ongezeko kutoka asilimia 21 walioripoti kwamba hali hiyo iliwatokea katika kipindi cha miezi sita tangu Aprili mpaka Septemba 2016.

Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kwamba bei ya mahindi (halisi, jumla) imeongezeka mara mbili (baada ya kuirekebisha na kiwango cha mfumuko wa bei wa wakati huo) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutoka shilingi 400 kwa kilo mwanzoni mwa 2015 mpaka shilingi 852 mwezi wa kumi na mbili, 2016. Wahojiwa wa Sauti za Wananchi wameripoti kwamba kwa wastani kilo moja ya mahindi inawagharimu shilingi 1,253. (Bei zilizoripotiwa kwenye masoko ya ndani).
Inafurahisha kuona unahangaika kutafuta uhaba wa chakula Tanzania. Tanzania sio Kenya haitatokea tukafa njaa kama Kenya.

Soma tena huo utafiti wa twaweza kabla ya kukimbilia kubadika ubaoni. Utafiti unasema watu wana hofu, ni tofauti ya kuwa na njaa. Neno la muhimu ni "hofu" ya njaa kutokana na wanasiasa uchwara kujenga hoja isiyo kuwepo. Zingatia neno HOFU
 
Jameni hivi umesoma hiyo taarifa kweli???? Watanzania huwa mnatia huruma sana likija suala la kusoma data kwenye survey au analysis. Hili nimeliona sana miongoni mwenu huko Bongo.
Hii ripoti ya Twaweza ina majibu ya maswali aina nyingi walizoulizwa Watanzania, neno hofu limekujia pale walipoulizwa kuhusu uhakika wa chakula, sasa soma walichojibu baada ya kuulizwa kuhusu matukio ya uhaba wa chakula, kwamba wangapi wamejikuta katika hali hiyo.
Survey hufanywa kwa kuuliza maswali kadhaa halafu unayafanyia analysis.
 
Kwahiyo upo hapa kutuaminisha kuwa Tanzania kuna njaa, haha....mbona unakazi. Tanzania ina akiba ya chakula kilicho limwa miaka mitatu iliyo pita, wewe unahangaika kupekenyua taarifa zisizo rasmi na kujidanganya. Neno ni HOFU kama hofu mliokuwanayo wakenya ya kupitwa na watanzania.

http://www.kilimo.go.tz/index.php/sw/resources/view/hali-ya-chakula-nchini-kuelekea-mwaka-2017

Serikali kusambaza mahindi tani mil. 1.5
 
Silk Smartphone.....proudly Kenyan!

Silk Patriot: Smartphone Made In Kenya By Kenyans

TOPICS: Silk Patriot
POSTED BY: WABTECH ONLINE
APRIL 21, 2016
Let’s face it,the Kenyan market is currently flooded with smartphones, which mostly originate from the East.
This trend will probably be a thing of the past given that a Kenyan company has come up with a new smartphone which they say employs the latest technology and comes at more affordable rates.
Silk1-777x437.jpg

silk3.png

Synergy Innovations are the brains behind Silk Patriot, a five and half inch touch screen Android phone with the latest 4G internet capabilities.

Michael Asola, the company’s chief operations officer explains: “Silk Patriot uses a qualcom chipset as opposed to the inferior mediatech processor.”

He reveals that 80 per cent of all phones in Kenya use mediatech processors, which is responsible for overheating and other problems phone users experience.
The reason these cheap phones, which he says are expensive in the long run, are flooding our market is becasue of the high demand.

“There is a huge demand for smart phone which most Kenyans cannot afford,” he explains adding that, “The Chinese simply give you what your pocket can afford. They also make high quality products.”
Kenyan consumers Asola says, “buy price, without checking quality. When they feel a product is affordable, they go for it.”
With Silk – which is an acronym for Synergy Innovations Kenya Limited, Asola says Kenya will now be at par with major innovators, just like Koreans have their Samsung.
Though the phone is designed in Kenya, it is currently being assembled in China.

“As we speak we have acquired property along the Thika Superhighway, next to Safaricom’s M-Pesa Academy, where we are planning to set up our assembly plant,” explains Asola.

vmtwbnaxupmr3l5lo6i56f646272715c.jpg

Mr. Asola, the brains behind the Silk Patriot smartphones
 
Wakati huo hiyo hiyo Tanzania nchi kubwa yenye rotuba kila mahali yenye madini ya kila aina yenye raslimali zaidi ya nchi zote Afrika yenye amani bila kuwahi kuwa na ugomvi wa kindani yenye vivutio bora vya utalii zaidi ya nchi zote Afrika ndio hiyo hiyo yenye watu wake wanaoishi kwenye mji mkuu Dodoma wanakula viwavi kukabili njaa Wala viwavi jeshi kuikabili njaa
Jamani haya maajabu ya ulimwengu! Hivi mtu yuaweza kula viwavi ngapi hivi ndio ashibe? Te te te!....
 
Ndio tunaagiza mahindi kwa sababu hizi
- Hela tunazo na uwezo tunao
- Nchi yetu asilimia 80% ni kame

Nyie pamoja na liinchi lenu lote hilo lenye rotuba kila mahali bila eneo kame hata moja mbona kuna wakati huwa mnaagiza mahindi kutoka Zambia, mumelaaniwa kwa uzembe na uvivu wa kufa mtu Tanzania Imports from Zambia of Corn (maize)
Sijawahi sikia Tz imeagiza mahindi toka nje labda sukari ila huku mahindi tunalisha ng'ombe
 
Back
Top Bottom