Kwa wafanyabiashara wenzangu

dabluz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
2,456
Reaction score
1,672
Naombeni mnipe maujanja jinsi mnavyoweza kusonga mbele pamoja nakuwa na malundo ya kodi.. Hasa biashara ya MAFUTA

1. Corporate tax
2. Services levy
3. Jamaa wa OSHA
4. Fire
5. Rental tax kama umekodi
6. Business license kila mwaka una renew
7. Kodi ya bango yani hii imeniuma sana nimelipa 1.2M jamani?!!
8. Bado Ewura hawajaja kung'ata
9. Bado jamaa wamazingira hawajavamia ( Nemc)
10. Vipimo nao wapo
11. Halafu hapo kulipa mishahara bado
12. Namalizia na majambazi ndio funga kazi.
Nisaidieni ujanja jamani pale juu nimesahau.
13.Payee

Mnawezaje kusonga mbele maana naona kiza kimeanza kutanda kwangu.
 
changanya na maji hayo madizel na petrol...
_Tanzania ukifanya biashara kihalali hutakaa upate pesa
_tena tz biashara haramu ndio inalipa kwasababu hakuna ofisa yeyote wa serekali asiyekula rushwa
 
Mkuu Marire sasa sintakosa wateja!! Halafu Ewura ndio watanifungia kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Weka bendera ya magamba tu hapo hata mgambo hasogei!
 

KUNA MABO MATATU YANAWEZA KUWA MSAADA KWA KIPINDI CHA MUDA MFUPI,WAKATI AU MREFU.
Kupanga ni kuchagua

1.Tafuta wenye fani zao unaweza pata unafuu lakini ukienda kienyeji utaumia mfn. tafuta watu wanaotoa ushauri wa mambo ya kodi ( Tax Consultants )

2. Wekeza kwenye elimu hasa upande huo wa mambo ya kodi kwa wanao,au binafsi kama vigezo vipo ama hata ndugu ili waje wakukomboe ama ujikomboe mwenyewe.

3. Tumia vizuri nafasi ya sanduku la kura 2015
 
Mkuu 10Shoka14 hapo namba 3 ngoja nikae kimya.. Ila mengine nayafanyia kazi na asante kwa ushauri mzuri.
 
Last edited by a moderator:
katika ushauri wote huu ndio mzuri ila usiwaweke moyoni

Mkuu kama mimi kimwili niko ccm ila ki roho CHADEMA na michango nawachangia wakipita kwa ofisi.Nita wapendaje magamba wakati wana nitesa sana na kodi zao?
 
Kwakweli hawajamaa ukijidai mjuaji imekula kwako naanza kutafuta urafiki na bendera yakijani aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…