Kwa wafugaji wa kuku wa mayai

Ndio maana sitajihusisha kwenye kilimo na ufugaji, bora niwe mnunuzi wa bidhaa za kilimo na ufugaji
 
wapi huko wanauza 4000? nahitaji tray 100 kwa 3500
 
tatizo la kukariri soko la jirani. vukeni mipaka, ya vijiji/miji tafuteni maajent muwarundikie mizigo. uzuri ni kuwa sasa hivi mitandao ya barabara ni safi nchi nzima. licha ya vipande vichache nyenye ukorofi kulingana na mvua.

pia kuna haja ya kuchagua aina tofauti za biashara sio biashara mkumbo. eti jirani kafuga kuku, au kanunua taxi nawe bila abc za biashara husika unaingia ati kwa vile kuna miundombinu wezeshi-mfano chakula, vifaa vya ujenzi, madawa. hawafikirii nani atauziwa mazao ya mradi wao.
wazo zuri saana ndugu
 
tafuteni masoko nje ya maeneo mliyopo. niko ngara Kagera. tray ya mayai tunauziwa minimum 9,000. kuna wakati inapanda 10,000-11,000. yanatolewa nje ya ngara.

sio story maana nina kijiwe cha chips.
Kweli kanisa niliwahi panda basi Arusha to Dodoma nilishudia mayai yakishushwa kondoa yakitokea Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…