Kwa Wahanga Wote Wa Mikopo, CALL FOR MAANDAMANO BUNGENI DODOMA OCTOBER29

Kimbakuli

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
408
Reaction score
435
Leo nilienda Wizarani kufahamu kama Wizara imekuja na jibu lolote kuhusu kilio cha vijana makumi elfu ya watoto wa kimasikini bila kujua hatima yao na nikabaini kwamba Heslb, Wizara na Serikali kwa ujumla wake hawana suluhisho lolote mpaka sasa na wala hawajui watafanyaje. Sasa, sehemu pekee ambapo kilio chetu kinaweza kusikika ni bungeni tu maana wao ndio wanapanga matumizi, Sasa, bunge linaanza vikao vyake octoba29, Huwa kuna pesa ya dharura inatengwa na bunge kwa ajili ya dharura ya nchi, suala hili ni dharura kubwa kwa hiyo tutawaomba wabunge watuidhinishe kiasi ili masikini sisi tukasome, Mapendekezo yangu, WAATHIRIKA wa HESLB wote wenye uwezo wa kufika DODOMA tufanye hivyo lakini pia tunaoomba kuungwa mkono na WanaSEKONDARI wote,wanaUDOM wote, wanaVYUO wote, uongozi wa TAHILISO na DARUSO WanaDODOMA wote, wanaHARAKATI WOTE, VIONGOZI WASITAAFU wa NCHI na WaTANZANIA kwa ujumla wao. ANGALIZO, maandamano yetu hayatahusiana na chama chochote cha siasa. Maandamano ya amani ni haki ya kila mtanzania kikatiba kwa hiyo msiigope njooni tupaze sauti zetu kwa watawala walioitelekeza elimu ya nchi na kuwanyima fursa watoto masikini na mayatima na hata kama hatutapata mwaka huu lakini cha msingi tupate mfumom mzuri wa ugawanyo wa pesa za walipa kodi wa nchi hii na madudu yaliyofanywa na HESLB mwaka huu yasijirudie tena.yote kwa yote TUKUTANE DODOMA TUDAI HAKI YETU. ASANTENI SANA.
 
Huu sasa ni uchochezi, naamini kuna uzembe kwa wengi lakini sidhani kama suala hili limefuata taratibu husika!
BUSARA katika kutatua matatizo ni njia sahihi mno!
 
kiukwel apa ni siasa tyu maana jana wame2andikisha majina yan inauma sana kuona tunafanyiwa ivi
 
hivi wabunge ambao wametoa taarifa kuwa hilo suala linajadiliwa kuwa kwa sasa wanashughulikia mambo mhm (ukaguzi wa hesabu wa vyama vya siasa) hivi ni tofauti na ambao watakuwa huko Dodoma mmmmh! anayejua atoe njia sahihi ili kufanikisha hili suala ila kwa kuandamana kwenda Dodoma nauli kubwa spika Makinda vice Ndugai wote Sikio la kufa ni WAZI HAKUNA CONSENSUS B'COZ KILA STAGE WATU WALIPITA HADI LEO WAMEFIKA KWENYE KAMATI YA BUNGE BADO FLAMBOYANCY NA KUNA WABUNGE WA VYAMA VYOTE SO HOW ABOUT DODOMA WABUNGE NI TOFAUTI NA HAWA TULIONGEA NAO?but if we must die never cry b'coz we provide the way for another generation ,,,anayeweza afike ila nimekubali until now beautiful ones are n't yet born uhuni tu hapa Tz maneno mengi kumbe wote YAHAYA leo wote macho juu juu hot topic Zitto kabwe ila 23,300 walikosa mkopo na uwezo kwenda chuo hawana habari nayo ilihali daily watu wanaenda kwenye hiyo kamati ila that's a simple problem
 
habar ya kwmb wameongeza 36bn ni uongo, habar za kuandka namba na majina ni danganya toto, so kilichobaki ni KUANDAMANA2
 
Huu sasa ni uchochezi, naamini kuna uzembe kwa wengi lakini sidhani kama suala hili limefuata taratibu husika!
BUSARA katika kutatua matatizo ni njia sahihi mno!

Si uchochezi kwa sababu waliokosa mkopo ni wengi mno na hawana kabisa uwezo wa kujilipia university watakwenda wapi hawa? kijana wangu naye amekosa na hamna sababu yoyote iliyoelezwa ya kukosa kwake mkopo licha ya mimi kwenda hadi bodi ya mikopo pale Mwenge.
Serikali isijaribu kunyamazia hili kwani tuna uhakika wa watoto wa wenye uwezo waliopata mkopo huku watoto wengi wa maskini wasio na wa kuwafanyia follow up wakikosa mkopo na hivyo kuzima nyota ya matarajio yao ya kuwa na maisha mazuri. WATAKWENDA KWA NANI?, WATAMLILIA NANI? admission wanayo , mkopo hawana tell us wafanye nini?
 
so what is our standing? we need morale for that,,sio kwenda kwenda tu
 
Ukienda HESLB wameweka jamaa fulani getini, ukisema ww ni 1st year tu wanakufuza km mbwa, wanatamani hata wakupige kabsa
 
Ukienda HESLB wameweka jamaa fulani getini, ukisema ww ni 1st year tu wanakufuza km mbwa, wanatamani hata wakupige kabsa

Poleni Sana ndugu zangu 1st year. Huu ni uonevu wa hali ya juu. Niko nanyi kwa maombi Mungu afanye kitu kwa ajili yenu.
 
ni kweli ata me jana nimeenda pale aisee nimekimbizwa na mlinzi hadi nikasahau sendors zangu kiukweli inauma cha msing ndo icho tyu 2andamane tyu
 
hofu yangu ni ile kauli ya handsome pinda"wapigwe2..tumechoka sasa".Mnaweza mkaandamana kwa amani kabsa lkn serikali lazma itawa misconcept na kudhani mna2miwa na wanasiasa(hasa chadema).
 
hao Chadema si watu walienda huko wamepata kitu gani na kwenye kamati wamo lakini wamesema nini wanasema wao watatoa Elimu bure na ni priority so where's their tension mbona hatuoni wote YAHAYA tu ukombozi wa NCHI hii ni Raia wenyewe sio Chama wahuni wote
 
Kama Chadema tuneishaeenda hakuna hasiyetufahamu,CCM nako pia,bunge dogo tumeingia sana tumekutana na waheshimiwa tofauti tofauti mana walikuwa na kamati zao hapo,Suala la wanafunzi zaidi ya elf 23 kutokwenda chuo kisa kukosa mikopo kwao limeonekana kutowagusa ,tukaamua kurejea tena bodi ya mikopo (HESELB).ili tujue zimetumika vipi bilion 325 kwa watu elfu 29tu,jamaa walidai uongozi wa juu wote hawapo wamesafiri,tukaona wanatuchezea akili,tukatishia kufunga geti na kulazimisha kuingia ofisini mwishowe Mkurugenzi akatoka ila tiyari tumeshaletewa defenda 2 za wale jamaa wa Mh.Pinda ka 20 hivi na bunduki mkononi na mijibwa yao.Tukamuoji mkurugenzi kiukweli jamaa hakuwa na majibu,akajiumauma ila wasaliti uwa hawakosi akatokea Jamaa kutoka TAIRISO akamsaidia mkurugenzi kwa kuwapa vijana ahadi nao wakakubali eti watapewa mkopo."uongo mtupu"tukaishia andika majina kama kawa yetu"siasa tupu". Ila kuna Mh.fulan tumekutana nae tumemweleza suala letu la kukosa mkopo na kunyanyaswa na watendaji wa serikal tena kwa maandishi,akaadi suala ili kulifuatilia na wiki ijayo katwambia linaanza shughulikiwa,hivyo tuwe na subira.nawasilisha
 
kama hamjui kwa nini tunaandikishwa majina ni hivi kama ikitokea fujo o chochote pale nyie ni moja ya watu muhimu wa kutoa ushaidi take care na haya majina
 
kama hamjui kwa nini tunaandikishwa majina ni hivi kama ikitokea fujo o chochote pale nyie ni moja ya watu muhimu wa kutoa ushaidi take care na haya majina
wanachotakiwa kujibu hawa jamaa wa helsb ile bilioni 325 imetumikaje kwa idadi ndogo ya watu waliopewa mikopo kinyume na hotuba ya bungeni,swala la majina sidhani kama ni tatizo.
 

mweshimiwa gan kasema ivo, lini, wap
 
Wazir kivuli kambi ya upinzani Mh.suzan limoh,siku tulipo kutana nae pale Bunge dogo posta.Litakuwa chini ya kamati yamaendeleo ya jamii ya Mh.Magret Sitta. Jamani ni kumwomba MUNGU.tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…