Kimbakuli
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 408
- 435
Leo nilienda Wizarani kufahamu kama Wizara imekuja na jibu lolote kuhusu kilio cha vijana makumi elfu ya watoto wa kimasikini bila kujua hatima yao na nikabaini kwamba Heslb, Wizara na Serikali kwa ujumla wake hawana suluhisho lolote mpaka sasa na wala hawajui watafanyaje. Sasa, sehemu pekee ambapo kilio chetu kinaweza kusikika ni bungeni tu maana wao ndio wanapanga matumizi, Sasa, bunge linaanza vikao vyake octoba29, Huwa kuna pesa ya dharura inatengwa na bunge kwa ajili ya dharura ya nchi, suala hili ni dharura kubwa kwa hiyo tutawaomba wabunge watuidhinishe kiasi ili masikini sisi tukasome, Mapendekezo yangu, WAATHIRIKA wa HESLB wote wenye uwezo wa kufika DODOMA tufanye hivyo lakini pia tunaoomba kuungwa mkono na WanaSEKONDARI wote,wanaUDOM wote, wanaVYUO wote, uongozi wa TAHILISO na DARUSO WanaDODOMA wote, wanaHARAKATI WOTE, VIONGOZI WASITAAFU wa NCHI na WaTANZANIA kwa ujumla wao. ANGALIZO, maandamano yetu hayatahusiana na chama chochote cha siasa. Maandamano ya amani ni haki ya kila mtanzania kikatiba kwa hiyo msiigope njooni tupaze sauti zetu kwa watawala walioitelekeza elimu ya nchi na kuwanyima fursa watoto masikini na mayatima na hata kama hatutapata mwaka huu lakini cha msingi tupate mfumom mzuri wa ugawanyo wa pesa za walipa kodi wa nchi hii na madudu yaliyofanywa na HESLB mwaka huu yasijirudie tena.yote kwa yote TUKUTANE DODOMA TUDAI HAKI YETU. ASANTENI SANA.