I see that you are taking these matters too personal! Usitake kusema kuwa una karatasi ya kunote wanaoiunga na kuipinga CHADEMA kwenye hii forum? Watu kuonyesha sentiments kwenye mambo ambayo wana mashaka nayo haimaanishi kuwa wako totally opposed to the whole issue.
Kwa mtaji huu unaweza kushindwa kuipata kura ya mpigakura anayekuuliza maswali kuhusu mustakabali wake akikupa kura yake, badala ya kumjibu utaanza kumwambia ametumwa kukuuliza maswali magumu? Hayo ndiyo tuliyoyasikia yakitokea kwenye primaries za CCM kuwa mgombea aliulizwa maswali na mapandikizi, hawajui kama wanatueleza kuwa wao wanaandaa mapandikizi wa kuwauliza maswali rahisi. Kiongozi thabiti na mwenye upeo atajua namna ya kuhandle situation yoyote. Uliza Gordon Brown na yule mwanamama ambaye miaka yote alikuwa anaipigia labour.
Siasa na ukombozi wa nchi hii si suala lako binafsi, ni ushirikiano wa wote wanaopenda maendeleo. Wengine wanajoin late, wengine mapema, lengo ni moja. Hata kama aliipinga CHADEMA mwanzo, kwani hakuna uwezekano wa kubadili msimamo? Kwa nini uanze kutilia mashaka watu ambao hata hujui kuwa ni chama gani, na uko radhi kuwapokea ambao unawajua kabisa wametoka CCM na siku zote walikuwa wanapiga kura ya kuukandamiza upinzani bungeni?
Watu hatuchangii hapa kwa maslahi binafsi, bali mstakabali wa Taifa, tunajaribu kuwaunga mkono walio kwenye mstari wa mapambano kwa namna tunavyoweza na kwa kadri ya uwezo wetu, na si wote lazima tuwe na nembo. Siasa si suala la kutaka kusifiwa na kuungwa mkono kwa kila utakalosema. Kwa sasa CHADEMA inahitaji msaada wa aina yoyote wa wote wanaoitakia mema nchi yetu, sio muda wa kubagua watu, usije ukaungana na JK kukataa kura za baadhi ya watu katika nchi.
Kwa hili fikiri tena, siasa haiendi hivyo ndugu! Wengine watabadili mwelekeo siku ya kupiga kura, huwezi kukataa kura yao, sasa maana ya kampeni iko wapi? Usichukulie akili ya MS ndio ya wote hapa JF....