Kwa waishio na VVU tu, Karibuni kupeana experience na life styles

Snitchertz

Member
Joined
Dec 15, 2014
Posts
26
Reaction score
13
Karibuni Wana Jamvi waliopata ajali hii.Siku izi VVU ni kama magonjwa mengine ambayo yanaitaji kuwa kwenye dawa through out your life.Kwangu binafsi magonjwa ambayo nayaogopa yanatisha kuliko ni Cancer na Kisukari.ingawa ukiwa na VVU usipokuwa makini basi kisukari na hata cancer unaweza pata.hapo hiyo cocktail ni deadly.

Sasa kwa sisi ambao tunaishi kwa dawa huwa hatuna forums ambazo tunakutana kujadili hizi issue,kupeana experience,taarifa hata ushauri kwa kuwa umepita na unajua.

Mie ndo mgeni kwenye hili Janga,leo nimepiga kimoja naona nyota saa izi...Napenda mtu anielezee siku yake ya kwanza kuanza pills,how did you feel...ulipitia yapi mpaka ukawa stable leo hii.Na pills gani unatumia.

Kama kuna forum kama hii somewhere naomba link ili niwe nafuatilia.

Karibuni No jokes,serious educative discussion.
 
Hapa humuoni mtu labda waje na ID ngeni ingawaje wapo wengi.
 
mi naona ambao hawana vvu wapitie tu hapa wajifunze nini changamoto za hii kitu ili wajikinge zaidi
 
Mkuu mleta mada,

Wazo lako ni zuri sana sana sana. Lakini hemu tuwe realistic kidogo, humu ndani kwa kutumia hizi ID zetu uwa kuna muda tunapiga sound hawa warembo wa humu.

Katika hali hiyo, sidhani hata kama mtu anatumia hizo pills atakuwa tayari kusema wazi wazi hapa kuhusu uzoefu wake?

Humu sidhani kama utapatiwa ushirikiano wa kutosha mzee.

By the way, nikupe pongezi kwa ujasili wako, ijapokuwa nahisi utakua na ID nyingine humu tofauti na hii uliyokuja nayo, just saying.
 
Kushiba nako kunashida ungekua na njaa wala usingewaza haya
 
du mkuu kwanza hongera kwa kupata wazo hili nahisi watakuja tu time will telll
 
Duh hili gonjwa si la kufanyia masihara.

Rafiki yangu mwaka juzi alipata TB akalazwa Kibong'oto miezi miwili hivi.Kumbe TB yake ilikuwa na HIV nadhani kuna mahusiano makubwa baina ya haya magonjwa mawili kwasababu karibu wagonjwa wote wa TB waliotibiwa na kupona kabisa baada ya muda unakuta ngoma inawasumbua sijui ni kwanini labda mtaalam wa afya Dr Riwa anaweza kutusaidia.
 

haya ameshakuelewa
 

Kama kweli uko serious angalia huo uzi hapo chini na usome reply zangu zote(nikisema zote namaanisha zote) kwenye huo uzi.Fanya hivyo wakati umetulia sana bila kubughudhiwa na mtu.Kaa peke yako usome kwa makini.Na kama kweli umezianza hizo dawa leo lazima utaziacha kama kweli utanielewa.

Inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?
 
Binafsi nadhani angelipeleka suala hili katika JF Doctor, labda angepata ushauri na msaada huko, hasa tokea kwa madaktari. Halafu kama wamiliki wa JF wanaona na naamini hivyo, wangeweza wafanye tathmini na utafiti juu ya wagonjwa kama hawa, kama wanataka jukwaa lao wawekewe, na hakuna na kusiwe na kuwanyanyapaa, maana wadau (baadhi humu), kila jambo kwao ni utani.
Ahsante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…