Kwa wajuzi wa magari naomba msaada

Kwa wajuzi wa magari naomba msaada

Mkiu Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Posts
261
Reaction score
278
Habari za mchana wanajamvi.

Gari yangu ni automatic na lina tatizo ambalo bado sijalielewa, kila ninayemuuliza ananipa majibu yake.

Tatizo lenyewe ni hili: Ukiingiza gia (D) au ( R) inatoa kishindo na gari linashituka hapo gia inakuwa imeingia, halafu inachelewa kubadili kutoka namba moja kwenda namba mbili, na ikibadili gari linashtuka, tatizo ni nini?

Naomba msaada wajuzi wa mambo haya.
 
Boss. Mi sio fundi ila kwa uelewa nimeelewa kwamba gear zinavoingia hazipo smooth.

Naomba nikuulize. Mara ya mwisho ulibadirisha lini Gear Box oil (ATF)?

Kama ni hivi karibuni uliweka ipi?

Kama hujawahi badirisha nadhani ungeanza na ilo.

Kama gari ni Toyota, chomoa dip stick utaona wameandika recommendation yao (mara nyingi ni ATF Type IV kwa Toyota).

Kama upo Dar nenda kanunue Toyota pale Msimbazi Kkoo inauzwa kama Elfu 95 hivi.

Nilikua na tatizo kama lako kwenye mlima gear ikiingia nilikua naisikia kabisa.

Pia tuwe na tabia ya kufanya preventive maintenance sio hadi gari lijaribike kama vile: Oil change, Breki zile pad na fluid, Coolant, ATF, etc.

Magari yetu yatadumu sana. Kinga ni Bora na cheap kuliko Tiba.
 
Hili ndio tatzo
20191101_221815.jpeg
 
Mad Max,

Umemaliza basi inatosha haina haja ya kuongezea tutaongopeana safi kama sio fundi basi unaelekea kuwa fundi
 
Gari inashtua kijoti?.. Huu ugonjwa upo kwa rav4 sana kulingana na experience yangu.. Ni gari gani hyo?
 
Habari za mchana wanajamvi.

Gari yangu ni automatic na lina tatizo ambalo bado sijalielewa, kila ninayemuuliza ananipa majibu yake.

Tatizo lenyewe ni hili: Ukiingiza gia (D) au ( R) inatoa kishindo na gari linashituka hapo gia inakuwa imeingia, halafu inachelewa kubadili kutoka namba moja kwenda namba mbili, na ikibadili gari linashtuka, tatizo ni nini?

Naomba msaada wajuzi wa mambo haya.
Bila shaka hiyo ni Rav 4 old model
 
Mkuu sie gari lako hatulifaham mara nyingi ukitaka kupata msaada au unapoomba msaada online jitahidi taarifa yako iwe imejitoshereza..aina ya gani make na model..

Mfano kwa hilo tatizo lako kuna sababu kuu mbili laweza kuwa tatizo upande wa umeme au machenical/hardwere..

Sasa hapo ndio ungesema ni gari aina gani..some times unaweza ukaona hupewi msaada au hujibiwi coz ufikishaji wa shida yako haijakaa vizuri
 
Mkuu, kwanza nilikuwa sijui kama na wewe ni kati ya member kwenye wanamiliki chuma.
Sasa....
Naomba nikupongeze kwa kumiliki chuma in town, na pili naomba nisiseme neno maana sina ninacho kiujuwa kuhusu magari.
Ahsante
 
Back
Top Bottom