Nakupa siri ya Massey ambayo wengi hawaijui. Yaliyosemwa hapo juu yote ni sahihi kuhusu MF. Ugonjwa mkubwa wa MF ni Hydraulic system yake (mikono ya kuinua jembe) inachoka mapema na ikichoka haina dawa.
Mimi nina MF,New Holland na John Deer na zote nilimenya mpya. Huo ndio ugonjwa wa Massey ambao kila mtu alie na Massey analia bila kujali ni U.K au Agroasia. Chukua New Holland (NH) TT75 DV series injini ya Iveco hutajuta. Au kama mfuko hauruhusu chukua Shangai New Holland CNH yenye injini model ya Boomer,Case DX series. Utaipata kwa bei chee kutoka China ikiwa mpya.
Mimi nipo Kalambo ranch ni mkulima nakupa experience sio maneno ya kusikia.