Kwa wakristo wale wanaounganisha nywele je wakifa ziondolewa?

Kwa wakristo wale wanaounganisha nywele je wakifa ziondolewa?

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,174
Reaction score
5,658
Kwa waislam, ni lazima mtu akifa na nywele za kuunganisha awe mwanamke ama mwanamme ni lazima ziondolewe.

Hata kama ni ndefu lazima zipunguzwe tu.

Vipi kwa wakristo, kwa wale wanaojua watupe elimu
 
Kwa waislam, ni lazima mtu akifa na nywele za kuunganisha awe mwanamke ama mwanamme ni lazima ziondolewe.

Hata kama ni ndefu lazima zipunguzwe tu.

Vipi kwa wakristo, kwa wale wanaojua watupe elimu
inaleta tofauti gani kwa marehemu au wafiwa au waombolezaji zikiachwa?
 
Mwili siku zote ni kwamba huharibika ndiyo maana Biblia inaona kwamba apandaye katika mwili atavuna uharibifu,mtu akifa ule mwili ni mzoga tu hata uweke kwenye kaburi lipi la thamani kiasi gani bali roho ya mtu ndiyo utakaomkomboa kama alitenda mema mbinguni panamhusu
 
Wanazikwa hivyo hivyo na nywele zao za bandia. Kwasababu hata wakiondolewa hakutakuwa na tofauti yoyote huko aendako.
 
Mtu akifa ule mwili unakuwa ni bure tu hizi process za mazishi ni kama heshima tu...
Kwahio hata wakimzika na make up haiwezi kumzuia kwenda mbinguni
Au wakimzika na wigi lake halimzuii kwenda motoni
 
Nywele zinaunganishwaje? sijaelewa
ana maana zinyolewe zote (km kaweka weaving au Rasta) na hata zile za sehemu nyingine
mwishowe naona hawa watu wanataka mtu azikwe uchi sasa
jamani mfu ni mfu tu mzikeni hata na mawig adhabu au heri sote hatujui
maana walioenda hawajarudi
 
Mwili siku zote ni kwamba huharibika ndiyo maana Biblia inaona kwamba apandaye katika mwili atavuna uharibifu,mtu akifa ule mwili ni mzoga tu hata uweke kwenye kaburi lipi la thamani kiasi gani bali roho ya mtu ndiyo utakaomkomboa kama alitenda mema mbinguni panamhusu
Mnawaacha waende na laana Zao?
 
Back
Top Bottom