Kwa wale mnaopenda kula hotel ya Aljazeera

Kwa wale mnaopenda kula hotel ya Aljazeera

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari wakuu

Nikiwa safarini kutokea Songea kuja Jijini Dar ili kupata Mlo wa mchana imebidi tupitie hotel ya Aljazeera, kwa wale wanaotokea Iringa, Njombe na makambako wanajjua.

Huduma za vyakula ni mbovu kupita maelezo nikimaanisha ubora wa chakula chenyewe ni mbovu kwani kidogo waniuzie kiporo cha wali kuku nikawaambia huo ujanja wenu naufahamu time na kama hakuna chakula kilichopikwa Leo basi rudisheni hela Yangu.

Mdada akaja juu ananifokea nikamwambia chakula chenu hicho hapo kwenye Meza nawaachieni mle Mimi naendelea na safari.

Nikatoka zangu nje nataka kuingia kwenye Gari Mara MTU ananivuta shati chukua hela yako, ilikuwa shilingi elfu tano, nikacheka kimoyomoyo nikaondoka zangu. Huwa sina tabia ya kula safarini ila kwa sababu natumia dawa ilinibidi.
Nitaenda kula mbele ya safari.

Nilikuwa nikisikia watu wakilalamika kuhusiana na hii hotel kuhusiana na chakula kibovu na lugha chafu za wafanyakazi ila Leo nimeshuhudia mwenyewe.
 
mimi huwa inaniwia ngumu kutofautisha mgahawa na hotel, hivi aljazeera ni hotel? bora hata ukale gengeni kwa mama ntilie unauona kabisa ubwabwa huo hapo unapikwa! huwa sili ovyo njiani, nikilazimika kula basi nitanunua hata biskuti na juice tu.
 
Kipindi kidogo cha nyuma nilipokuwa active kwa mazoezi nilikuwa nanua kifuko cha keki pale ubungo ama huko nitokako.. njiani nakamata soda ama juice naepukana na haya majanga.Tamaa za pesa zinafanya tunalishana vitu vya ajabu sana. Ni vyema kuepuka kula vyakula vya kupikwa pia nyama.
Wahindi wanautamaduni mzuri anaye safiri huandaliwa chakula home nakufungiwa kwenye hot port.
 
Migahawa mizuri na yenyewe huduma nzuri ipo road ya dar-arusha i mean Korogwe mpaka mombo (high way restaurant ya Dar xpress, blue parrot, hill top restaurant, Liverpool restaurant na kuna nyingine ya KLM xpress ambayo itafunguliwa soon, na moja nimeisahau jina) kwanza zipo nying so lazma huduma ziwe nzuri kwa ushindani
 
zote poa isipokuwa liverpool..
 
Pale ni majanga wale waarabu wanaangalia hela tu!!hawana utu kabisa!!eti wameweka na nyumba ya ibada pale wanaomba kwa zamu ili wapate wateja.Mimi nikienda mikoa ya huko hata soda sinunui pale wana lugha mbaya sana.
 
Liverpool chafu ajabu chakula kibovu watumishi wachafu cjui serekali yetu ina shea hapo
 
hahaha, nyumba ya ibada imeingiaje tena mkuu?!! ile wameweka kwa ajili ya wasafiri kupata mahala pa kutimiza matakwa ya imani yao.
 
1.Vipi unatambua kiporo cha wali au supu ambayo imehidhiwa kwenye freezer na kupashwa moto kwenye micro wave?
2. Chakula kilichohifadhiwa kwenye freezer kinayo madhara ya kiafya.
 
Suluhisho ni kubeba chako kwenye rambo tu,
 
Uko kama mimi Mkuu naogopa sana kula hovyo hovyo hasa katika hotel/mkahawa ambao hali ya usafi hairidhishi machoni.

mimi huwa inaniwia ngumu kutofautisha mgahawa na hotel, hivi aljazeera ni hotel? bora hata ukale gengeni kwa mama ntilie unauona kabisa ubwabwa huo hapo unapikwa! huwa sili ovyo njiani, nikilazimika kula basi nitanunua hata biskuti na juice tu.
 
Yaani pale hawajali ubora wa chakula halafu bei kubwa... nilikula yale mapande ya nyama nilojutraaaa
 
Liverpool chafu ajabu chakula kibovu watumishi wachafu cjui serekali yetu ina shea hapo
Ooh!! Umenikumbusha hii kidogo nitaapike wale ni majanga na balaa.Sana sana wanachafua jina la timu ya watu.
 
Nilikuwa napenda sn kula chips kuku pale halafu nafungiwa ili nile ndan ya gar. Kuna siku nikanunua ile nafungua ili nile naona kuna kamende. Ilibid nimwambie dereva asimamishe gari niirudishe japo new force ni wabish kusimama iliwabid maana nilikuwa na hasira na ukichanganya na njaa we acha tu. Walirudisha hela yangu, tangu siku hiyo nimekoma kula vyakula njiani.
 
hahahahaa, hako ka mende kalikuwa moja ya viungo, ushamba wako tu mkuu!
 
Uko kama mimi Mkuu naogopa sana kula hovyo hovyo hasa katika hotel/mkahawa ambao hali ya usafi hairidhishi machoni.

ni hatari mkuu, unaweza kujikuta unaendesha njia nzima! lakini kuna watu wanakula njiani mpaka unashangaa, kila anachoona mbele yake ye anatafuna, gari ikisimama atanunua chipsi, kuku, mikachumbari, vitu gani sjui ye anafakamia tu...loh! huenda tunatofautiana kinga huko tumboni..lol!
 
Umeniwahi Liverpool ni kama Aljazeera afadhali ule gengeni kuliko hapo,hawa waarabu tamaa zimewazidi uchafu wao wanauleta hadi kwenye biashara

Liverpool na Aljazeera ni DUGU moja!
 
Pale Aljazeera kwa chakula hovyo kabisa. Wasafiri wanaotumia mabasi wanalazimika kula pale sababu huwa wanapitishwa pale kwa lazima.
 
Back
Top Bottom