Kwa wale tulioachwa na wapenzi wetu tu

Kwa wale tulioachwa na wapenzi wetu tu

hango over za kuachwa zitakapoisha, karibu maishani kuendelea na maisha. maisha yanaendelea na hayatasimama eti kwa vile kuna mtu bado anawaza na kuwazua jinsi alivyoachwa!
 
Duh basi unaweza ukawa malaika wewe? hata shule ya msingi hujawai mpiga mtu kibuti? akabaki na maumivu?

yah....hapo penye blue ni sawa kabisa.....
nimejua hayo mambo ya loviduvi...nikiwa na miaka 37......

Kuna Watu
wanakuja katika
maisha yetu baadae
huondoka

Kuna Watu wanakuwa
marafiki zetu kwa muda tu
baadae hutoweka

Kuna Watu
wanakuja katika
maisha yetu baadae
huondokahuku wakiacha Oooo
makovu kwenye
nyoyo zetu

na wote hatupo
sawasawa katika
kufaulu kupata marafiki
wazuri !!!

Ya Jana ni Historia.
Ya Kesho ni Miujiza

Ya Leo ni Zawadi kutoka kwa Mungu.
Tunapaswa kushukuru kwa zawadi hii pekee

Smile utaniacha nilie bana,why this thread.Makovu yalishapona sasa wewe unataka kuyakuna na gunzi tena
 
ahahaaa sina hangover bwana,ila kusahau ngumu

Pole sana Smile,

Hata hivyo, unaonekana uko kwenye advanced stages of healing.

Mie niliachwa wakati nimebeba ring mkononi..ila nilimshukuru Mungu, kwani nadhani alijua kuwa kule kulikuwa siko ninakotakiwa kwenda!!

Babu DC!!
 
ahahaaa sina hangover bwana,ila kusahau ngumu

Umeonaee, ngumu hasa pale ww ulipokuwa mwema na muaminifu ukiamini na yy yuko hivi. Na inakuwa ngumu zaidi pale anapokuachia kitu kitakachokupa kumbu kumbu zake daima.

Pole sana mpendwa, but maisha lazima yaendelee.
 
Pole sana Smile,

Hata hivyo, unaonekana uko kwenye advanced stages of healing.

Mie niliachwa wakati nimebeba ring mkononi..ila nilimshukuru Mungu, kwani nadhani alijua kuwa kule kulikuwa siko ninakotakiwa kwenda!!

Babu DC!!

Mungu alikuwa na makusudi nawe, akukutanishe na bibi yetu, upate mapenzi matamu milele.

Ila kumbe na ww babu kash kash za mapezi zimekupata ujanani kwako?
 
kuachwa/kuacha ni kawaida kabisa katika ulimwengu wa mapenzi. hili huwa funzo kwa muhusika ila huwa linaima sana hasa pale unapokuwa umeivest vya kutosha. chukua kuachwa kama changamoto
 
Umeonaee, ngumu hasa pale ww ulipokuwa mwema na muaminifu ukiamini na yy yuko hivi. Na inakuwa ngumu zaidi pale anapokuachia kitu kitakachokupa kumbu kumbu zake daima.

Pole sana mpendwa, but maisha lazima yaendelee.

Kitu gani Koku?

Mtu ambaye hamjazaa pamoja...nadhani ni rahisi kumsahau kabisa, au nakosea?

Babu DC!!
 
Mungu alikuwa na makusudi nawe, akukutanishe na bibi yetu, upate mapenzi matamu milele.

Ila kumbe na ww babu kash kash za mapezi zimekupata ujanani kwako?

Hayo mbona ni kawaida sana?

Ila mie namshukuru Mungu kwani sijawahi kumpatia mtu hazina yangu yote..Akiwa na bahati kama ya Bibi DC anaambulia 60-80%!!! Huko nyuma nilikuwa najitahidi sana kuegesha na ilinisaidia kwa kiasi kikubwa.

Kama nilivyosema huko nyuma..ni hatari kuwekeza kiasi kikubwa kwa mtu hata akiwa mume au mke...!!

Babu DC!!
 
Kitu gani Koku?

Mtu ambaye hamjazaa pamoja...nadhani ni rahisi kumsahau kabisa, au nakosea?

Babu DC!!

Babu hujaona post yangu tittled NIMEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME?

Yule mshkaji aliniacha nikiwa mja mzito wa 2months, Nimejifungua mtoto kamfanana baba yake balaa.

Na siku zinavyozidi kwenda ndo sura ya baba yake inazidi kuja, mimi sijapata hata pua.

So when ninapomwangalia, i just remember his father.

Ndo maana nasema km una kitu permanent kinachokukumbusha yeye, ni ngumu kusahau.

Babu nimekuletea KITUKUU cha KIUME.
 
Sikuona Koku,

Kwanza hongera sana.....na pili, issue yako sasa iko juu zaidi. Ni tofauti na kuachana tunakozungumzia!

Nitakutafuta unitumie walu picha ya katoto kazuri ka mjukuu wangu!

But one thing...Kadri utakavyozidi kuizoea hadhi ya kuwa mama na kujenga bond zaidi na mtoto...I am sure story itakuwa tofauti kabisa. Ipo siku anaweza kuanza kulalamika kuwa anahitaji muda wa kuwa na mtoto wake!

Take care,

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom