Kwa wale tuliopteza wazazi wetu, tupeane pole hapa, nikikumbuka moyo unaniuma sana.

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,174
Reaction score
5,658
Za siku wanajf,

Ni mnamo 20/11/2018 majira ya 11: 26 asubuhi, siku ya jumanne nilipopata taarifa ya kufariki kwa mama yangu mzazi.

Nilipata taarifa nikiwa mkoa wa simiyu wilaya ya meatu kikazi.

Mama yangu alikuwa na umri wa miaka 50+.

Jinsi kifo kipoanzia:

Ilikuwa siku ya alhamisi, alisafiri kwenda kwenye harusi ya mdogo wake wakiume ambye alikuwa anamuoza binti yake siku ya ijumaa.

Harusi ikaisha salama, safari ya kurudi nyumbani kwake kondoa ikaanza, mwanaye wakiume ( mama) akambeba kwenye pikipiki wakaanza safari, kutembea hatua chache tu ujuba ukaning'inia kwenye tairi ya nyuma ukajizungusha kwenye panga za pikipiki, ujuba ukamkaba shingoni hadi pikipiki ikasimama yenyewe.

Akadondoka chini na kuzimia palepale, wakamkimbiza kwenye zahanati ya wilaya , akapata fahamu na kuongea kwa sauti ya chini sana,hali ikaanza kugeuka siku ya jumapili usiku , kumbe mama yangu alikuwa kashaparalize mikono na miguu, sababu walikuwa wakimbeba tu.

Na kitu kingine kilichochangia kifo chake ni kwamba mama alikuwa na pressure, alikuwa akisikia tukio lolote la kuhuzuniaha pressure ilikuwa ikimpanda sana, na baada ya tukio kutokea pressure ilikuwa ikipanda hadi 187.

Na ilipofika 20/11/ 2018 mungu akamchukua.

Nikikumbuka ndo nguzo yangu ilikuwa hii kwa jambo lolote naumia sana.

Mungu amfanyie wepesi katika maisha yake ya kaburini,

Amiiiin.

Karibu tupeane pole kama nawewe ushampoteza mzazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma chanzo hadi nimesisimka,kila mtu ana namna yake ya kumuondoa katika hii dunia...sad!
Pole sana mkuu sote njia yetu ni moja,Mungu aendelee kukutia nguvu na mama apumzike kwa amani...Amen
 
Pole sana mkuu,namshukuru Mungu mama yupo mzima ila baba zaidi ya kumuangalia kwenye picha sina njia nyengine.

Mzee wangu kulingana na kumbukumbu nilizopewa alipotea duniani nikiwa na 1½ year akiwa aged 36.

Mungu awarehemu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu! Hata Mimi mama yangu ana pressure nilivyosoma nimeona uchungu sana
 
Za siku wanajf,

Ni mnamo 20/11/2018 majira ya 11: 26 asubuhi, siku ya jumanne nilipopata taarifa ya kufariki kwa mama yangu mzazi.

Nilipata taarifa nikiwa mkoa wa simiyu wilaya ya meatu kikazi.

Mama yangu alikuwa na umri wa miaka 50+.

Jinsi kifo kipoanzia:

Ilikuwa siku ya alhamisi, alisafiri kwenda kwenye harusi ya mdogo wake wakiume ambye alikuwa anamuoza binti yake siku ya ijumaa.

Harusi ikaisha salama, safari ya kurudi nyumbani kwake kondoa ikaanza, mwanaye wakiume ( mama) akambeba kwenye pikipiki wakaanza safari, kutembea hatua chache tu ujuba ukaning'inia kwenye tairi ya nyuma ukajizungusha kwenye panga za pikipiki, ujuba ukamkaba shingoni hadi pikipiki ikasimama yenyewe.

Akadondoka chini na kuzimia palepale, wakamkimbiza kwenye zahanati ya wilaya , akapata fahamu na kuongea kwa sauti ya chini sana,hali ikaanza kugeuka siku ya jumapili usiku , kumbe mama yangu alikuwa kashaparalize mikono na miguu, sababu walikuwa wakimbeba tu.

Na kitu kingine kilichochangia kifo chake ni kwamba mama alikuwa na pressure, alikuwa akisikia tukio lolote la kuhuzuniaha pressure ilikuwa ikimpanda sana, na baada ya tukio kutokea pressure ilikuwa ikipanda hadi 187.

Na ilipofika 20/11/ 2018 mungu akamchukua.

Nikikumbuka ndo nguzo yangu ilikuwa hii kwa jambo lolote naumia sana.

Mungu amfanyie wepesi katika maisha yake ya kaburini,

Amiiiin.

Karibu tupeane pole kama nawewe ushampoteza mzazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
pole mpendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu alifariki nikiwa mdogo sana, lakini kwa matendo ya nduguze huwa nashukuru Mungu hakuanza Mama!..
Alale salama huko alipo baba Wick
 
  • Thanks
Reactions: amu
Pole mkuu nakuelewa sana, ninapitia hali hiyo kwa sasa nakuelewa sana
Mzee wangu alifariki nikiwa mdogo sana, lakini kwa matendo ya nduguze huwa nashukuru Mungu hakuanza Mama!..
Alale salama huko alipo baba Wick
 
Pole mkuu nakuelewa sana, ninapitia hali hiyo kwa sasa nakuelewa sana
Hakuna hali nayopitia kuhusu mambo hizi, ila ni hayaa matendo ya wakubwa zangu nikicompare na mzee najua leo hii bimkubwa angekuwa na stress kama wenzie so bora aliwahi ondoka tu!..
 
dimaa
Sijaelewa maana ya neno "ujuba" naomba msaada katika hilo tafadhali.
 
Back
Top Bottom