Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

UKIFIKA HAPO nitag warumi
 
Duh hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha wao kujifanya wanamwamini Mungu huku ukweli ni kwamba wanatumia matunguli, hiyo ndio tunaita Shirki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Story yangu ya kwenda Kwa mganga ilikua ni hivi
Wakati wa Makuzi yangu sikulelewa na wazazi wangu Bali nililelewa na mdogo wa baba yangu kwa hivyo nilijiwekea malengo yangu kichwani kua lazima nijitahidi sana kutafuta pesa niwe na maisha mazuri na njia pekee niliyokua nayo Kwa kipindi kile ni kusoma Kwa bidii walau niweze kupata connection za watu tofaut
Mwaka 2012 nilihitimu kidato cha Sita nikachqguliwa kwenda chuo fulani jijin dar es salaam nilifurahi sna kwani pia bodi ya mkopo ilinilipia kwa 96% kumbe hii ilikua habari mbaya Kwa watu wangu wa karibu bila mimi kujua
Mwaka 2013 nilipata likizo ambapo tulitakiwa kufanya field Mwenyezi Mungu alinisaidia nikapata field kwenye ofisi kubwa sna huko mkoani ambako ndipo nililelewa nikaona ni bora Kwa Kua nitasave pesa zangu za boom Kwa kuishi nyumbani
Wakati nafanya field housegirl watu hapo nyumbani alinifata akaniambia kua anamjomba wake ambae ni mganga amemsaidia sana hivyo ni vyema na mimi niende nikaangaliwe kama ninatatizo kwanza nilishangaa Kwa nini aniambie niende Kwa mganga hali ya kua mambo yangu yananiendea vizur Kwa kweli nilikataa nikamwambia siendi Kwa mganga hata iweje.Basi yule dada alikasirika sana usiku wa siku ile nilipata ndoto ya kufanya mapenzi na mtu nisiemfaham na nilivyoamka asubuhi akanifata nikajikuta namwambia kuhusu ndoto yangu (hapa najilaumu mpaka leo kwani nilikosea sana kumwambia ile ndoto) basi akaniambia nimpatie huyo mjomba wake mganga jina langu la baba na mama aniangalie kwenye ramli kweli nilifanya vile na majibu yakatoka Eti kuna mtu ananiloga inabidi niende nikatibiwe basi nikachukua namba ya mganga ili kesho yake niende kutibiwa
Usiku wa siku ile sikulala kwani niliota kua kuna mtu ambae ni ndugu yangu ananipeleka Kwa mganga halafu mimi nakataa napigana kabisa nisipelekwe huko nilivyoamka asubuh Kwa ujinga wangu nikamsimulia yule house girl ile ndoto akanijibu ni ndoto tuu wala nisipgope
Nilijiandaa siku ile nikapanda basi mpaka Kwa mganga maarufu ambae anaishi same ajabu ni kua ile sehemu niliyoiota kwenye ndoto ndo ile ile yani kuanzia barabara mpaka nyumba ndo ile ile lakin nikawa nashindwa kuondoka nahisi mganga alinifunga
Basi mganga akajifanya kuniagua halaf akaniuliza majina ya wapenzi wangu na mm nikamtajia akaniambia hawanifai niachane nao nikamaliza nikaanza safari ya kurudi nyumbani ajabu ni kua wakati wa kurudi Basi ilikua ipate ajali Mara tatu nilishangaa nikawa niko na maswali mengi sana kichwani nilivyofika nyumbani nikamkuta housegirl amekasirika sana kana kwamba kuna kitu kimemkera kumbe walitaka kuniua kwenye ile ajali ya gari ikashindikana na kuanzia siku ile ilikua kila ninachofanya lazima nimwambie mganga
Mwaka 2014 nilipata mtu wa kunioa alikua mtoto wa kigogo maarufu dar es salaam Kwa akili ya kitoto Na ndumba ya mganga nikaachana na yule kaka kila siku tulikua tunagombana nikaamua kuondoka bila kufukuzwa aliumia lakni mganga akawa ananipa kichwa.Maisha yakaendelea lakin nikawa napata ndoto mbaya za kulishwa nyama usiku kutolewa nje baharin mambo yangu kuvirugika kila siku ajali za boda boda zikawa ni sehemu ya maisha yanguq na mwaka wangu wa mwisho wa masomo 2015 niligraduate Kwa shida sna nilikua naumwa vitu visivyoeleweka nilikua siwezi hata kutoka ndani
Baada ya graduation nilikaa miezi sita bila ajira na wala siwezi kutoka ndani nilikua naumwa sana nikaamua kuanza kufanya maombi nilikaa wiki mzima nalia namlilia Mungu anionyeshe mlango wa kutokea maana maisha yangu yalikua hayaeleweki basi kuna siku nilikua ndani nimelala nikasikia mtu ananiita akaniambia Tuchki Amka nenda Kwa mtu fulani atakusaidia na utapona kabisa nikashtuka nikaangalia saa ilikua saa Sita nikajisemea rohoni kama hii ndoto ni ya kweli na kama kweli Mungu ananijibu nalala tena ikifika saa nane kamili nitaamka niende ajabu ilivyofika saa nane kamili nilishtuka kutoka usingizin kama vile mtu kaniamsha jamn Mungu yupo kuanzia naoga mpaka namaliza kuvaa kulikua kama kuna mtu ananisimamia nilikua kwenye ulinzi mkali sana
Nilivyofika Kwa huyo mtu niliekua nikienda kupata msaada tuliongea mambo mengi sanaa lakin ajabu baada ya maongezi akaniuliza Tuchki umewahi kwenda Kwa mganga Kwa hofu nilikataa kwani ni mtu ninaemuheshimu sana aliniuliza kama Mara tatu nikakataa basi nikatoka pale nikashika njia ya kurudi nyumbani wakati nimepanda gari yule mganga alipiga simu akaniuliza umetoka wapi? Hapo nikajua Kua Yule mganga ni mchawi na ametumwa kuniangamiza inakuaje ajue nilipotoka? Nilimjibu nimetoka kutafuta kazi nikakata simu nilipokfika nyumbani mganga alinipigia simu akaniambia niende kwake kuna tatizo eti sitapata kazi Kwa wakati ule mpaka nipewe dawa
Alfajir nilipanda bus mpaka kwa mganga sasa ajabu ni kua safari hii ilikua si mimi tena nilikua naona mambo yote Kwa macho ya nyama niliona misukule nyama za watu na uchawi wote niliofanyiwa na yule mganga yani mpaka mtu aliemtuma housegirl anipeleke huko niuwawe nilimjua siku ile yule mganga akataka kunimwagia dawa sijajua ni za nini nikashangaa nimefunikwa mpaka leo sikujua alienifunika ni nani jamn nilitoka mbio nikapanda basi nikarudi nyumbani
Kesho yake nikaenda Kwa yule bwana alieniuliza kama niliwahi kwenda Kwa mganga nikamueleza mkasa wote alilia sana akaniambia yeye aliniona muda mrefu kua nina shida na akaniweka kwenye maombi na ndo maana siku ile aliniuliza kama niliwahi kwenda huko.Basi alinichukua akanipeleka kwenye ibada nikaombewa nikarudi nyumbani kumbe watu wangu wa karibu walitaka kuniua ukweli niliujua na nikakaa kimya wala ndugu zangu sikuwaambia ila yule housegirl nilimwambia mpaka leo akikutana na mimi anakimbia yani hawezi kuniangalia usoni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli aisee, ukienda kwa mganga anakupa na mapepo ili uendelee kurudi mara kwa mara, hataki kuvunja uteja nawe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana ukawa bachelor sugu[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana na uyo housegal bado yupo kwenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi upo, Mzee wa Kanisa kapigwa kombora na mwenziwe kaenda kuponea kwa mganga kisa Uenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Kanisa..
------------------------------------------------------------
++++++++++++++++++++++++++++++++++

Baada ya kupoteza watoto wa kiume wa4 mfululizo lakini wakike wapo safi, mama akamweka Yesu pembeni kachepuka kwa mganga mtoto aliyekuwa anakaribia kudanja sasa hivi yupo nursery...

Uchawi upo, la muhimu omba Mungu mitihani UISHINDE..
 
Aiseee, binti na mtoto wako wp kwa sasa?
Sent using Jamii Forums mobile app
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umeona eeeh


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
please mkuu kama unajua walipo wanganga mbeya naomba unisaidie maana haya maisha nimejalibu kila njia nimeshindwa sasa naona nijalibu kwa wagaganga2
 
Ndo maana ukawa bachelor sugu[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha tunawaangalia tu wanaojifanya oooh sijui waganga siwajui mara tangunnizaliwe sijawahinkwenda kwa waganga na porojo nyiiiingi..Inawezekana ambao hawajaenda kwa waganga wamo kweli ila sio hawa wanaojifaragua humu.

By the way kuna matatizo mengi ktk hii dunia ambayo huwapeleka watu kwa waganga mfano mm mdogo wangu anayenifuata alikuwa anakojoa mpaka kafika darasa la 7 mpaka bimkubwa akakonda akiwaza mwanangu akifaulu itakuwaje??hana uhuru wa kuwatembelea ndugu kwa kuhofia manyanyaso ya ukikojozi ss kuna jamaa mmoja ni mtaalamu wa mitishamba akamwambia bimkubwa mama mbona hilo ni tatizo dogo sana..

Akamwambia tafuta kuku mmoja mchinjeni mkishamkatakata nyie nyama kuleni ila mm niletee yale maji mliyooshea nyama.Bimkubwa akaona utakuwa sio uungwana akachukua kuku mzima akafunga safari na dogo moaka kwa huyo mtaalamu,ile kufika jamaa akamuuliza mbona mmekuja na kuku sasa maza akajibu hapana nimeona itakuwa vizuri tukaja tukamla wote tu.Jamaa akachinja kuku yulle wakaosha nyama jamaa akamwambia mkewe apike pilau yy akachukua maji na kufanya utaalamu wake kisha akampa binkubwa dawa aliyotengeneza na maelekezo yake kisha pilau na kuku vikatengwa mezani wakala wakaenjoy wote kisha mama akaaga na kuondoka na dogo..

Baada ya kutumia dawa siku ya kwanza dogo akakojoa kidogo siku ya pili hakukojoa siku ya tatu hakukojoa siku ya nne hakukojoa bimkubwa akaona huu utani isije kuwa dogo anamzingua akaenda kukagua kweli hata harufu hakuna siku ya tano,sita,aabahakukojoa bimkubwa akampigia simu yule mtaalamu jamaa kwa kujiamini akamwambia mama hiyo ndo aafari hapo kaishaoona usijali huzuni yako imeisha ia wala sihitaklji malipo yoyote toka kwako nimemsaidia mdogo wangu basi bimkubwa huzuni yote ikayeyuka.Sasa hapa unakuta mtu anajificha eti sijawahi kwenda kwa mganga ili aonekane wa kisasa wakati kumbe kuna matatizo mengine ya msingi tu.SHAME ON THOSE WHO HIDETHEMSELVESkuwa hawajawahi kwenda kwa qaganga ilhali wameshaenda mara kibao tena wengine wanaenda kuroga kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kali

l love you mamy .
 
Maadui wengi wapo karibu yako aidha rafiki aidha ndugu

l love you mamy .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…