Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Warumi katika ubora wako nakuelewa sana! Kama ni kuua nyoka basi umesaga kichwa kabisa.

Kiukweli nimeanza kwenda Kwa waganga kwa mara ya kwanza Mama yangu ndyo alinipeleka baada ya baba kuwa kichaa!
Hapo mama alinipambania sana japo nilikuwa sipendi ila kadili nilivyokuwa nakua ndyo naona mama alikuwa sahihi kabisa Hadi sasa Bado najipambania na naendelea kutafuta mganga atakaeweza kutegegua mtego aliowekewa baba yangu mzazi.

Ni story ndefu sana lakini kw ufupi Bado baba ni kichaa anapata unafuu Kwa kutumia dawa za hospital Milembe nilishampeleka akarudi , Tanga nimezulula nae Kwa waganga wakanyosha mikono, ndipo nilipoamua kumpeleka Milembe Dodoma, huko alikaa miezi 2 akaruhusiwa.

Kwa ufupi kichaa cha baba ni Cha muda mrefu sana tangia 1996 mwezi July, wamezaliwa wadogo zangu wawili wamekuta hiyo hali lakini ugonjwa wake unalipuka kutokana na mwandamo wa mwezi, mwezi mkuu full moon, anakuwa na wenge sana, hapo anachanganya maneno mapigo ya moyo yanakwenda Kasi sana anakuwa na huruma na hasira ghafla. Kuna mengi nataka kuzungumza lakini naona siyo wakati wake.
Nipenda kutoa shukrani za dhati Kwa Mshana Jr na Ngulukizi, jamani Hawa siyo waganga ila wamekuwa karibu sana na Mimi katika nasaha na ushauri.

Ngoja nishie hapo ila IPO siku nitakuja na Uzi, Mwenye kuweza kunisaidia kimawazo karibu Dm IPO wazi, ila Kwa sasa najipambania kwanza nikijiapa kidogo naendelea kumpambania Baba Kwa sababu Bado anateseka.
NB: Usije Dm ukaniambia nimpeleke Kwa Mwamposa.
 
Dah huu Uzi bado unatembea.....Yong na yang...mchana na usiku ulozi upo.....ila Mungu pia yupo
 
Mmmmmh
h Kumbe unaweza kumwendea mtu kwa mganga
 
So why you need the in and out
 
Bado hujakua, ukikua utakanyaga
 
Sasa na nyie kwanini mliamua kumchoresha mwenzenu? kama mlijua anachoumwa si mngempeleka sehemu atakayopata tiba sahihi. au mliamua kumgeuza mwenzenu futuhi?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Duuuuu
uh haya mambo yanatisha
 
Duuuu
Juzi nipo na ndugu yangu mmoja yeye ni dereva wa shirika linamilikiwa na dini flani ananiambia huwa kuna padre anampelekaga kwa mganga kwa siri nilistaajabu mno mno ananiambia nyie acheni haya maisha
uh
 
Mganga wa kweli hupokea pesa baada ya kufanikiwa mambo Yako,wengine ni wahuni tu.
 
Hahaha umenikumbusha mbali saana ,
Enz naanza maisha niliwah kwenda kw bingwa mmoja ila mapigo yake ctayasahau mpaka naondoka dunian.
Jamaa alkua na kibuyu anakiulza swali kinatoa majibu kw mlio kama mluzi hvi Kisha jamaa anatafsri huo mlio,
Ila hamna chochote nilcho fanikiawa mpaka nikagundua kumbe jamaa ni matapeli tuu hamna lolote
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜daaah hizi ni movie au ukweli?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Yule jamaa mshenzi sana.. Nilipanda basi mpaka Mnazi huko nikiwa na mpangaji wangu.. Natafuta dawa ya biashara .. Kufika huko yule mshenzi alinichanja machale mwili mzima na kunipaka midawa yake inawasha balaa.. Akanipiga laki tatu..

Niliporudi hakuna nilichouza na mtaji ukakata.. Mshenzi sana yule msambaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…