Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Siri kubwa ya mafanikio hapa ulimwenguni ni ushirikina/ nguvu za giza , sema kikundi flan cha watu kinataka kiwapumbaze watu kwa kuwaaminisha kwenda kwa waganga ni dhambi au laana Sijui , wakati wenyewe ndo washirikina wakubwa, tena wengine uchawi wao wa kutisha, ila kwenye jamii wanaonekana wacha mungu , wanasaidia jamii ila ndani ni mbwa mwitu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Warumi katika ubora wako nakuelewa sana! Kama ni kuua nyoka basi umesaga kichwa kabisa.

Kiukweli nimeanza kwenda Kwa waganga kwa mara ya kwanza Mama yangu ndyo alinipeleka baada ya baba kuwa kichaa!
Hapo mama alinipambania sana japo nilikuwa sipendi ila kadili nilivyokuwa nakua ndyo naona mama alikuwa sahihi kabisa Hadi sasa Bado najipambania na naendelea kutafuta mganga atakaeweza kutegegua mtego aliowekewa baba yangu mzazi.

Ni story ndefu sana lakini kw ufupi Bado baba ni kichaa anapata unafuu Kwa kutumia dawa za hospital Milembe nilishampeleka akarudi , Tanga nimezulula nae Kwa waganga wakanyosha mikono, ndipo nilipoamua kumpeleka Milembe Dodoma, huko alikaa miezi 2 akaruhusiwa.

Kwa ufupi kichaa cha baba ni Cha muda mrefu sana tangia 1996 mwezi July, wamezaliwa wadogo zangu wawili wamekuta hiyo hali lakini ugonjwa wake unalipuka kutokana na mwandamo wa mwezi, mwezi mkuu full moon, anakuwa na wenge sana, hapo anachanganya maneno mapigo ya moyo yanakwenda Kasi sana anakuwa na huruma na hasira ghafla. Kuna mengi nataka kuzungumza lakini naona siyo wakati wake.
Nipenda kutoa shukrani za dhati Kwa Mshana Jr na Ngulukizi, jamani Hawa siyo waganga ila wamekuwa karibu sana na Mimi katika nasaha na ushauri.

Ngoja nishie hapo ila IPO siku nitakuja na Uzi, Mwenye kuweza kunisaidia kimawazo karibu Dm IPO wazi, ila Kwa sasa najipambania kwanza nikijiapa kidogo naendelea kumpambania Baba Kwa sababu Bado anateseka.
NB: Usije Dm ukaniambia nimpeleke Kwa Mwamposa.
 
Dah huu Uzi bado unatembea.....Yong na yang...mchana na usiku ulozi upo.....ila Mungu pia yupo
 
Mmmmmh
Msema kweli mpenzi wa mungu.nilishakwenda kwa mganga.kwa ajili ya demu.tulikuwa wapenzi ghafla aka badilika.akawa mgumu kinomaaa.hanipendi tena.niliumia.kuna rafiki yangu yeye ni mganga nikamueleza akasema tulia atarudi.
Tukafanya Mandingo mixer kuoga njia panda usiku.kuchoma sana UDI.kupasua Nazi n.k
Kiukweli demu alianza kubadilika na kuanza kuongea na Mimi.Mara salam n.k.
Siku zikapita tukarudi tena kwenye penzi.ila hatukudumu tuliachana.
Ushauri kama MTU hakupendi ACHANA NAE.MADAWA HUISHA NGUVU.
h Kumbe unaweza kumwendea mtu kwa mganga
 
Kila mtu huwa ana imani yake

Kila mtu ana mbinu zake za kutatua matatizo yake.

Wapo ambao wakipata shida kidogo tu ni kwa babu sangoma wanakimbilia.

Tujuzane, vipi gharama huko? Shida zinatatulika? Permanently or temporarily?

Na pia nasikia every dark magic comes with a price, ni kweli..? Ni price zipi mnalipa kupata magic nyeusi hizo

Tujuzane

Binafsi mimi sijawahi kukanyaga kwa sangoma na sitakaa nikanyage huko
So why you need the in and out
 
Kila mtu huwa ana imani yake

Kila mtu ana mbinu zake za kutatua matatizo yake.

Wapo ambao wakipata shida kidogo tu ni kwa babu sangoma wanakimbilia.

Tujuzane, vipi gharama huko? Shida zinatatulika? Permanently or temporarily?

Na pia nasikia every dark magic comes with a price, ni kweli..? Ni price zipi mnalipa kupata magic nyeusi hizo

Tujuzane

Binafsi mimi sijawahi kukanyaga kwa sangoma na sitakaa nikanyage huko
Bado hujakua, ukikua utakanyaga
 
Duuuuu
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.

Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.

Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.

Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .

Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.

Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.

Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.

Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.

Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.

Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308




Sent from my iPhone using JamiiForums
uh haya mambo yanatisha
 
Duuuu
Juzi nipo na ndugu yangu mmoja yeye ni dereva wa shirika linamilikiwa na dini flani ananiambia huwa kuna padre anampelekaga kwa mganga kwa siri nilistaajabu mno mno ananiambia nyie acheni haya maisha
uh
 
Kuna rafiki mmoja ni mtu mkubwa mahali fulani yy anapingana sana na mambo ya waganga kwani kakulia kwenye imani kali ya kisabato, mwaka jana mwezi wa tatu wakapanga kumuondoa kwenye cheo alichokua nacho bodi ikakaa na yy akajulishwa alivyoona maji yako shingoni akaniomba nifanye juu chini kama kuna uwezekano tumnusuru, so tukaenda tabora kwa fundi mmoja hv yy hafanyi kazi mchana ni usiku alitupokea akasema tumsubiri babu atakuja saa tatu usiku, ilipofika saa tatu tukimsubiri huyo babu mara akatwambia tuingie ndani kwenye kichumba kdogo chenye mlango wa bati, tulipoingia akatuambia babu atakapokuja kuja tusiigope, du akachoma Ubani na kuanza kuongea ghafla tukaanza kumuona yeye mwenyewe akibadilika na kuwa kibabu yaan tulitoka nduki kwa uoga, baadae mkewe akasema huyo ndo babu yule aliyewapokea ni mjukuu wake ila akianza kazi anakua ni babu, alimfanyia kazi huyo rafk yangu kaz moja ya kibabe mno na alisema asilipwe kwanza mpaka tuone matokeo, yaani tunaamka asubuhi jamaa uamuzi ukatenguliwa akarudishwA KWenye cheo chake, kuna watu walifanya sherehe kabla, kusikia jamaa anarudi hawakuamini macho yao, baada issue kukaa vizur jamaa slumps1.5m,
Mganga wa kweli hupokea pesa baada ya kufanikiwa mambo Yako,wengine ni wahuni tu.
 
Hahaha umenikumbusha mbali saana ,
Enz naanza maisha niliwah kwenda kw bingwa mmoja ila mapigo yake ctayasahau mpaka naondoka dunian.
Jamaa alkua na kibuyu anakiulza swali kinatoa majibu kw mlio kama mluzi hvi Kisha jamaa anatafsri huo mlio,
Ila hamna chochote nilcho fanikiawa mpaka nikagundua kumbe jamaa ni matapeli tuu hamna lolote
 
Mkuu hiyo inatokea sana huku Usukumani, unakuta Ng'wana Luhanya ameenda kuloga usiku kumbe jamaa limezindika ile nyumba, anajifalaguafalagua mpaka kunakucha yuko hapo hapo na masempele yake. Mpaka mwenye nyumba anaamka! Sasa hapo nikiamua kumfanyia mauaji?
😂😂😁😁😁😁😁😁daaah hizi ni movie au ukweli?
 
Tulienda kwa mganga ili timu yetu ishinde , basi mganga akatupa dawa tukaichimbie kwenye goli atakalokaa kipa wetu hapo hakuna goli litakaloingia. Basi tukafanya kama alivyoangiza mganga, kipindi cha kwanza kikaanza kwa kasi sana wapinzani wetu wakifanya mashambulizi ya hatari sana lakini yote yaliishia kugonga mwamba na kutoka nje, sisi tukafanikiwa kupata goli moja.
Kipindi cha pili baada ya kubadilishana magoli tukasahau kuhamisha dawa, na hapo ndipo iliposhuka mvua ya magoli.
Full time tumepigwa 5 - 1.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Yule jamaa mshenzi sana.. Nilipanda basi mpaka Mnazi huko nikiwa na mpangaji wangu.. Natafuta dawa ya biashara .. Kufika huko yule mshenzi alinichanja machale mwili mzima na kunipaka midawa yake inawasha balaa.. Akanipiga laki tatu..

Niliporudi hakuna nilichouza na mtaji ukakata.. Mshenzi sana yule msambaa..
 
Back
Top Bottom