Kwa wale tunaohofia usafiri wa anga tukutane hapa

Kwa wale tunaohofia usafiri wa anga tukutane hapa

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Hakuna kitu kinatisha kama ndege inapoanza kupaa aisee.

Yaani unaona tu majengo yalee kama viberiti.

Nakumbuka kuna safari niliwahi kukacha kurudi na ndege nikapanda basi.

Ile kitu acha tu.
 
kuna wakati nashindwa kuelewa mhudumu anapoonyesha kwa vitenda na kutoa maelezo namna ya kujiokoa mambo yakiharibika
hapo angani 😀😀
 
Ukipoga safari mbili tatu utazoea, nakumbuka mara ya kwanza nilitamani nishushwe aisee, baada ya hapo safari zilizofata ndio kwanza nikawa napenda kukaa dirishani kila safari, siku hizi hata nisipokaa dirishani kawaida tu
 
last month bombdier ilishindwa kutua bk sbb ya hali ya hewa mixa kukutana na dhoruba, dada nlokaa nae pembeni alikuwa anapiga sala mwanzo mwisho[emoji3][emoji3]
 
last month bombdier ilishindwa kutua bk sbb ya hali ya hewa mixa kukutana na dhoruba, dada nlokaa nae pembeni alikuwa anapiga sala mwanzo mwisho[emoji3][emoji3]
Haha hiyo nakumbuka ilinikuta safari moja ya mwanza , aisee balaa lake halikua dogo, sijawahi zoea hiyo kitu kabisa.
 
Mungu awarehem fast jet kwa kunifanya nami nipande kunguru kwa mara ya kwanza.
Jamaa wangeendelea kuwepo ingekuwa bata sana yaani.
 
Wakati wa take off ndege ikianza kupaa kuna ka feeling fulani like your stomach is dropping...na ikiwa angani ikianza descent napo haka ka feeling like tumbo lina drop hujitokeza.
 
Ndege inapopaa si changamoto sana, bt inapotaka kutua inakuwa na Stress Sana[emoji1787], unaweza hisi mkojo
 
Ndege inapopaa si changamoto sana, bt inapotaka kutua inakuwa na Stress Sana[emoji1787], unaweza hisi mkojo
Basi kila mtu na changamoto zake, kutua huwa sina changamoto kama take off, acha kabisa.
 
Kuna tetesi mzee mbishi anaogopa sana kupanda ndege!ndo maana hapendi kwenda majuu....
 
Hakuna kitu kinatisha kama ndege inapoanza kupaa aisee.

Yaani unaona tu majengo yalee kama viberiti.

Nakumbuka kuna safari niliwahi kukacha kurudi na ndege nikapanda basi.

Ile kitu acha tu.
Kuna mambo huwa natamani yabadililshwe

Mafunzo ya kujiokoa yafanyike practically, yaani kila mtu ajaribishe namna ya kufunga, kupulika, kukaza, n.k ili wahudumu wajue kama kafanya sahihi ama la.

Halafu badala ya kuweka vifaa vya kujiokolea kwenye juu, vikae sehemu mbele ya sit ili k murahisisha uchukuaji wake abiria akipanic.

Lakini pia ni kwa nini hizo mbinu hazisaidiagi watu linapotokea janga? Nikwamba haziko effective ama ni kwamba heka heka hufanya watu washindwe kuzitumia?

Usafiri wa ndege ni noma ingawa kila mahala pana changamoto

1. bAsi halivuki bahari.
2. Baiskeli haivuki pori refu.
3. Mitumbwi haistahimili mawimbi.
4. Meli zinatekwa na wasomali.
5. Kwa miguu ndiyo kabisa.
6. Bodaboda Mhhhhhhhhh.
7. BAjaji inaimba kihindi.
 
Back
Top Bottom