Hakuna kitu kinatisha kama ndege inapoanza kupaa aisee.
Yaani unaona tu majengo yalee kama viberiti.
Nakumbuka kuna safari niliwahi kukacha kurudi na ndege nikapanda basi.
Ile kitu acha tu.
Kuna mambo huwa natamani yabadililshwe
Mafunzo ya kujiokoa yafanyike practically, yaani kila mtu ajaribishe namna ya kufunga, kupulika, kukaza, n.k ili wahudumu wajue kama kafanya sahihi ama la.
Halafu badala ya kuweka vifaa vya kujiokolea kwenye juu, vikae sehemu mbele ya sit ili k murahisisha uchukuaji wake abiria akipanic.
Lakini pia ni kwa nini hizo mbinu hazisaidiagi watu linapotokea janga? Nikwamba haziko effective ama ni kwamba heka heka hufanya watu washindwe kuzitumia?
Usafiri wa ndege ni noma ingawa kila mahala pana changamoto
1. bAsi halivuki bahari.
2. Baiskeli haivuki pori refu.
3. Mitumbwi haistahimili mawimbi.
4. Meli zinatekwa na wasomali.
5. Kwa miguu ndiyo kabisa.
6. Bodaboda Mhhhhhhhhh.
7. BAjaji inaimba kihindi.