Kwa wale tunaolala sebuleni kwa ndugu njooni tupeane mbinu za kivita

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Kuna muda unaweza kwenda kwa ndugu kuwasalimia iwe likizo au kutalii mji, ila bahati mbaya wakawa wana chumba kimoja tu na sebule, hivyo ukaambiwa utakuwa unalala sebuleni na watoto wadogo pale.

Sasa wale wahanga njooni mtuambie ukitaka kwenda bafuni kuoga unafanyaje, na vipi ukitaka kubadilisha nguo ilihali pale sebuleni ni vurugu tupu; majirani hawakatiki kuja kuangalia movie ya Huba na Chakorii.

 
Mbinu Gani za kivita? Unataka uelekezwe namna ya kukwangua jungu kimyakimya wakiwa wamelala usiku?

TOKA HAPO KWA SHEMEJI MUME WA DADAAKO
 
Mimi Nilienda Kijiji Kimoja Kinaitwa Ilangali Karibu Na Manda Kwa Babu Mwaka Jana..Aisee..Babu Alikuwa Anaingiza mademu Usiku..Nilikaa Siku 4 ya tano Nikasepa Kurudi Zangu Manda.
Hhhahaha njoo nipo apa kijiji cha huzi
 
Mwanaume mzima unaenda kulala kwa dadako kwa zaidi ya siku Moja ili iweje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…