Kwa wale wa Ngala na Karagwe, hiki ni nini?

Kwa wale wa Ngala na Karagwe, hiki ni nini?

wewe hukula sadaka maana kuna kaka yako huku aliniambia alikuwa anakula hela ya sadaka kisa hizi kabaragara..

hamna bana hiyo ilikuwa ni sh 50 ninayopewa kula shule ndo nakula hivo vitu.....
 
kila mtu anaongelea shule ya msingi kweli vya kitoto zaidi..

ahh ahh aah ,ndugu vinaitwa kabaragara kwa kihaya, kiswahili ni jamii ya mabumunda,kama wanajf wasemavyo ni mchanganyiko wa ndizi kisukari na unga wa muhogo au mahindi, vikiwa vya muhogo tu havipendezi maana huwa vyeusi sana ila ukichanganya unga ila ukaacha wa muhogo uwe mwingi utavipenda...ila kwa bukoba huwa ni vya watoto zaidi ndo maana wengi wamekual enzi za primary mpaka fomu ii , ila hata watu wazima wanakula kwa kujificha si hadharani, ni sawa na kula ugali adharani kwa wahaya utajishushia p, hasa kama ni mchana...ila vidude ni vitamu balaa...zaidi ya andazi.
 
Duh jamani umenikumbusha hizo bonda/kabaragara. Nikifika mitaa hiyo ntazisaka.
 
hiyo hapo ukipiga tano tu unashiba. mabimunda inaitwa. mia
 
Dah! Umenikumbusha aisee hizo kabaragara ukitaka uzipende zaidi basi uwe unashushia kwa mramba,ni noumaa!
 
Dah! Umenikumbusha aisee hizo kabaragara ukitaka uzipende zaidi basi uwe unashushia kwa mramba,ni noumaa!

mramba ndo nini tena mkuu full kunichanganya..
 
Vibama hivyo nimevipika sana shule ya msingi.

Pia kwa wale tuliosoma shule za uswazi saa nne tulikuwa tunakula vibama, mabumunda, ufuta, pipi kijiti, sukari guru, vitumbua, andazi, maembe sindano ya chumvi na pilipili kama ni msimu, ufuta aina mbalimbali za matunda kama mapeasi kama ni msimu (Iringa enzi hizo jama wenyewe wanajua hasa wale wa Njombe) misaula, mikusu, mawenge (aka zambarau), mitonvu, mapeasi, zabibu kutoka Dom, maeple, midaha kusugulia meno, matunda damu, mastafeli, matopetope, mifurusadi, embe mafuta (aka avocado) madansi, komamanga, mapichez, mapera n.k

Kweli kuna mikoa imebarikiwa kuwa na matunda mengi ya ajabu nimeyamisi sana hayo ya rangi blue.
 
Back
Top Bottom