Vibama hivyo nimevipika sana shule ya msingi.
Pia kwa wale tuliosoma shule za uswazi saa nne tulikuwa tunakula vibama, mabumunda, ufuta, pipi kijiti, sukari guru, vitumbua, andazi, maembe sindano ya chumvi na pilipili kama ni msimu, ufuta aina mbalimbali za matunda kama mapeasi kama ni msimu (Iringa enzi hizo jama wenyewe wanajua hasa wale wa Njombe) misaula, mikusu, mawenge (aka zambarau), mitonvu, mapeasi, zabibu kutoka Dom, maeple, midaha kusugulia meno, matunda damu, mastafeli, matopetope, mifurusadi, embe mafuta (aka avocado) madansi, komamanga, mapichez, mapera n.k
Kweli kuna mikoa imebarikiwa kuwa na matunda mengi ya ajabu nimeyamisi sana hayo ya rangi blue.