Haya sasa , kwa wale wenye tabia ya kula nauli nawashauri muache 😂😂😂😂, maana dawa yenu imepatikana, mtanyooshwa hadi muombe poo 😂😂.......
Na wale wauzaji wa yale mavumbi ya kwa kina Fally Ipupa na Papaa Mobimba pia nawashauri waanze kutafuta shughuli mbadala ya kufanya mapemaaaa...🤣🤣🤣🤣
Mazoezi ya Kegel ndio ninachozumgumzia hapa...., kama ulikuwa mwanachama wa Chaputa, basi usijali, fanya KG.
Ili uweze kufanya mazoezi haya inabidi uutambue msuli wako wa Pc (pc muscle), jinsi ya kuujua fanya hivi, wakati umeenda haja ndogo, bana mkojo katikati ya kukojoa, ule msuli utakaoutumia kukatisha mkojo usiendelee kutoka ndio msuli wako wa pc.
Namna nyingine ya kuujua msuli wako huu ni wakati umeenda haja kubwa, pale wakati unamaliza haja kubwa, kuna msuli ambao hubana ile 'ringi' ili iweze kukata 'gogo', ule msuli uaokusadia kukata lile ’gogo’ ni msuli wako wa pc. Sasa umeshaujua msuli huu, tunaingia hatua ya mazoezi yenyewe.
Ili uweze kufanya haya mazoezi inabidi ujue namna ya kubana na kuachia msuli wa pc. Unabanaje? ni rahisi sana, fanya kama unavyofanya wakati wa kukatisha mkojo au wakati unakata gogo, hicho kitendo ndio tunaita kubana msuli wa pc. (Muhimu: Hutumii mkono wa kidole kubana). Mazoezi yenyewe sasa yako hivi:-
- Bana msuli wako wa pc kwa sekunde 10, kisha uachie. (Mwanzoni utapata tabu kuubana ila kadri unavyozoea itakuwa rahisi zaidi).
-Subiri sekunde 20 zipite, kisha bana tena kwa sekunde 10 na uachie.
- Rudia huo mzunguko wa kubana kwa sekunde 10 na kupumzika kwa sekunde 20, rudia hadi uwe umefanya mizunguko 10. (Tumia stop watch ya simu kufanya hivi)
- Ukishamaliza mizunguko 10, bana na kuachia msuli wa pc kwa haraka haraka kwa muda wa sekunde 10, na hapo umemaliza session moja ya mazoezi.
- Siku inayofuta pumzika usifanye, hadi kesho yake tena, yaani uwe unaruka siku moja moja.
- Matokea baadhi utaanza kuyahisi almost immediately, ila itabidi usubiri wiki kadhaa kuona matokea, matokeo halisi unaweza ukayaona baada ya miezi 6.
Best of luck