Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Kwahiyo jamaaa anajua mtoto ni wakee.
 
hhahaaaaaaaaa tema mate chin wew!mm dhambi nnazo sikatai (uuaji wa viumbevisivyo na hatia)i..lakini kuna zile dhambi kubwa kubwa(ingawa dhambi zote zinafanana)..hapa tunaongelea zile kubwa kubwa!..sasa ww unaangukia kwenye zile kubwakubwa!UNALO
Teh teh, eti uuaji wa viumbe visivyo na hatia. Ulicheza rafu itakuwa. We tubaki tu duniani na dhambi zetu tule ya dunia.
 
Tehetehe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], acha kwanza kiundanishe mbavu zangu nisije nikavunjika,
 
hakuna siri ya watu wawili. Yangu itabaki yangu. Nikiisema watu watanichukia daima. Ngoja ibaki kwangu.
 
Siku moja usiku mnene nimekaa nyuma ya nyumba nakula kitu changu, nikasikia kama vishindo nyumba ya jirani nikapanda ukuta nichungulie ile natoa kichwa nikakutana uso kwa uso na Mzee wa ile nyumba akiwa na mwanae wa kiume, mke wake na jamaa wengine wawili wote waliona kuwa niwewaona bangi yote ilikata kichwani nikarudi ndani mbio, hawakuwahi kuniuliza chochote na mimi sikumwambia mtu yeyote yule hadi mwaka jana nilienda nyumbani nikawa naongea na mama stori za mtaani nikajikuta namwambia nilichokiona siku ile ila nikamwambia kuwa makini walijua kuwa nimeona usije kumwambia mtu hii habari!
 
Walikuwa wanafanya nini kwani mpaka uogope?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe ngoja tukutafute wewe...ulifanya ubakaji wa dhahiri kabisa.
 
Mtu mmoja marehemu Kwa sasa, nikiwa Fundi wa radio za magari. Aliniletea gari yake Isuzu trooper niifunge spika za ubavuni,miaka ya 2008, akaiacha kuwa anamizunguko angeiludia badge.

Kwani nilikuwa na kazi nyingine nikiifanya. Hivyo nikamaliza kazi ya kwanza na kuanza kazi yake. Nikafungua mlango wa kushoto wa mbele, ubavuni kuna silingboard ili nichonge duara ya kufunga spika. Ile kufungua nusu body tu nikaona suruali [emoji158] Jeans ikiwa imekatwa mguu mmoja ikiwa imelowa mafuta, huku imefungwa na mipila ya baiskeli.

Nikashangaa!! Nilipoamua kuitanua ndani sikuamini nilichokiona!! Ilikuwa imejaa risasi!!. Ndugu yangu msomaji nililudishia bila kufunga spika. Nikaona wasijue. Nikawaza hawa ni majambazi tu na wamejisahau. Nikahamia mlango wa kulia. Nilichoona ni bunduki fupi!! Nikaludishia body. Nikaamua kurudi ndani ya workshop nikaendelea na kazi zingine bila kuwaeleza wenzangu.

Ghafla mmoja akaja na gari Tex speed. Akaniuliza kazi tayari? Nikamwambia bado ndio nataka kuianza nilibanana. Akasema natoka na gari robo saa nakuja. Aliporudi akawa amefungua zile body akidai ameona anilaisishie. Nikamwambia asante kwani nimebanwa na kazi.

Nikafunga wakachukua. Badae miaka mingi nilikuja kumuona ameuwawa na polisi. Ndio jambazi waliovamia ndege ya madini mgodini.
 
Nenda ka confess kwa rafiki yako
 
Duuh aisee...!! Ilikuwa balaa mkuu na wewe usingepomaa wangekusakaaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…