Kwa wale wanao fanya biashara ya mahindi naomba msaada hapa.

igihumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2017
Posts
529
Reaction score
483
Habari za kutwa wadau.?
Naona fursa katika hii biashara ya mahindi kutoa shamba na kuleta mjini. Nilikuwa nahitaji kuanza hii biashara nilikuwa naomba mwongozo juu hii biasha.
Ni mtaji kiasi gani naweza anza nao?
Ni changamoto gani inayo zinazo ikumba hii biashara?
Wapi naweza pata mahindi kwa bei ya chini kiasi?

Asanteni karibuni sana..
 
Hivyo vitu ni vigumu mtu kukueleza hayupo anaetaka kuongeza ushindani kwenye chimbo lake la kupata mzigo kwa bei nafuu vinginevyo uwe unataka mawazo kwa mtu asiyeifanya hii biashara

Boss unasema umeiona fursa ktk biashara ya mahindi. Sasa unaanzaje kuuliza inahitaji mtaji kiasi gani???? Ikiwa umeona fursa ni kwamba umeona tofauti kati ya kununua na kuuza ni kiasi kadhaa kwa gunia sasa sijiulize hicho kiasi ulichokiona itakubidi uchukue gunia ngapi ili ufikie faida shs kadhaa... Weka malengo

Kingine boss ebhu edit uzi wako kidogo walau uwe na mvuto,,, na jaribu kupitia nyuzi nyingine zinazohusu mahindi utapata ABC zaidi

Mwisho mkuu, watu wanaonufaika ktk chochote na kuleta tofauti ni wale wenye taarifa sahihi kwa wakati sahihi hivyo boss taarifa ni mali usitegemee kuipata ovyo ovyo na kirahisi kihivyo, usiogope kuchoma nauli kwenda morogoro au tanga kusoma ramani ya mahindi we jilipue tu bt with caution
 
Upo sahihi!
 
asante sana Mungu akuzidishie kiukweli wewe uko tofauti sana asante sana tena sana
 
Ni biashara mzuri lkn inachangamoto zake. Afadhali wale wanaonunua mahindi Na kusaga sembe na kuanza kusambaza kuliko kununua mahindi na kuleta mjini. Wateja wa mahindi mjini wanasumbuwa Sana, unaweza kuznguka na gari kutwa mzima wanakumbua tu. Kila sehemu ukipeleka wanapiga bambo na kukupa bei ndogo, au wanataka kwa mkopo, ambapo kulipa wanasumbua sana.
 
asante sana mkuu.
 
Nairobi gunia ksh 4300=Tsh 96,000 approx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…