Kwa wale wapenda mbwa tuchukue tahadhari

Kwa wale wapenda mbwa tuchukue tahadhari

Hukufanya sahihi kumua, ulipaswa kufanya jambo moja rahisi, kwanza hakikisha uzio ni imara na si waya, pili asubuhi kabla ya kurudisha bandani avishwe mnyororo na kumtembeza kilometa kadhaa, wakati mnatembea ungehakikisha hakutangulii, kila akienda mbele vuta ile leash au mnyoromnyoro kwa nguvu na ghafla, ukifanya hivo mara mbili tatu atajua hautaki atangulie hivo atatembea sambamba na wewe, mfundishe amri chache za utii, kama acha, kaa, lala chini, njoo, twende, ingia ndani, subiri na ajue amri ya wakati wa kushambulia na wakati wa kuacha. Baada ya hapo utampenda mbwa wako.
Kwa muda ambao nimekaa mbali na sitegemei kurejea kwa kipindi Cha miezi 10 nafkiri nimefanya sahihi ili kuepusha matatizo zaidi.

Kwa upande wa amri/utii nilifanikisha kwa upande wangu ila nilikosea kwa watu walionizunguka maana sikufikiria endapo nitakuwa mbali je wengine wangeishi naye vipi?ndio hapo Sasa umbali ulipopelekea hayo yote maana kwa ukali wake hakutaka kusikiliza mtu mwingine.
Uko kwenye majukumu/mihangaiko unapigiwa simu mbwa kakata nyororo na katoka nje ya uzio/geti kamfunga kimtaa si mchezo ndugu yangu,kesi za ndani ya nyumba mbwa sijui kanikamata mkono,nguo zilikuwa haziishi na nje ndio kabisa kesi serikali ya mtaa zilizid
 
Kwa muda ambao nimekaa mbali na sitegemei kurejea kwa kipindi Cha miezi 10 nafkiri nimefanya sahihi ili kuepusha matatizo zaidi.

Kwa upande wa amri/utii nilifanikisha kwa upande wangu ila nilikosea kwa watu walionizunguka maana sikufikiria endapo nitakuwa mbali je wengine wangeishi naye vipi?ndio hapo Sasa umbali ulipopelekea hayo yote maana kwa ukali wake hakutaka kusikiliza mtu mwingine.
Uko kwenye majukumu/mihangaiko unapigiwa simu mbwa kakata nyororo na katoka nje ya uzio/geti kamfunga kimtaa si mchezo ndugu yangu,kesi za ndani ya nyumba mbwa sijui kanikamata mkono,nguo zilikuwa haziishi
ungemgawa bure kwa mtu mkuu
 
ungemgawa bure kwa mtu mkuu
Ni kweli lakini sidhani mtu kawaida kama ingekuwa rahisi kumtrain/kukaua naye labda ningemrudisha nilipomchukua angali mdogo
Ila waliniuzia mbegu ya ajabu wale field force 😅 nilikuwa najua German shepherd ila sijui ilichanganywa na mbegu gani Ile mbwa miguu ya mbele kama anabeba chuma
 
Hii ni ajenda ya vibaka kutuingiza choo cha kike, hatuyumbishwi, mimi nina mbwa kama 20, na mambo yako shwari tu
Uwezo wa kufikiri umefikia hapo, kumiliki mbwa ishirini unafikiri mchezo. Mbwa si njiwa, pia ukiangalia hoja haijazuia wewe kumiliki hao mbwa wako ishirini. Bali kutoa elimu kwa watu wenye akili timamu na wanaofikiria kumiliki mbwa au tayari wanamiliki mbwa.
 
Mkuu, nimecheka kwa nguvu sana, mbwa si njiwa, asante Mkuu, ila inategemea kila ntu na ntu na akili yake
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, ukiamua kufuga mbwa hasa hawa wakizungu kama Rottweiler, Pitt Bull, Mastif, Belgium Malnoir nk, tenga muda wa kuwa nao karibu. Mafunzo ni muhimu wafanye watambue kuwa wewe ndo mkuu na kiongozi.

Kwanini nasema hivi kuna kipindi nileta habari ya mbwa ya mbwa kumuua kijana wa kazi Dar, nilieleza kwa urefu saana, nikaeleza namna ya kuishi na mbwa kama Rott, Pitbull, Borebull na bila kusahahau GS. Lakini wengi walifanya utani bila kuzingatia somo. Narudia tena kwa ufupi kwa sababu kuna issue ya mbwa kumuua boss wao huko SA.

Chukuwa tahadhari zaidi unapokuwa na cross breed ya mbwa. Nimeyasema kwa sababu kuna mbwa wameua mmiliki wao huko SA, source BBC. Mimi ni mfugaji wa mbwa aina ya Rottweiller ninao wanne lakini wana utii wa hali ya juu.

Usiku inapoktokea wabweka saana nikiamka nitawaita nikiwa ndani watakuja dirishani au mlangoni, baada ya hapo ndo ninafungua mlango ninatoka then wao watanielekeza wapi kuna shida.

Usitoke nje kabla hujawasiliana na mbwa wako hasa kama tayari walikuwa wamechUkia na hakuna umeme, wanaweza kukuvamia na kukua.
Kwani harufu ya tajiri wao hawaijui kama hawa makoko yetu ukiwa hata mita 300 tu kashakutambua.

Hyo mnayomiliki nyie sio mimbwa, ni minyama ya porini sema binadamu mmeilazimisha kuifuga na matokeo yake ndio inawatafuna wamiliki,inakumbuka asili yao.
 
bora kudili na hawa sungura.
Nilieleza kuna mbwa wanavibari mpaka polisi ila sijui polisi inawaza kutetea ccm tu
IMG_0168.jpg
 
Kwani harufu ya tajiri wao hawaijui kama hawa makoko yetu ukiwa hata mita 300 tu kashakutambua.

Hyo mnayomiliki nyie sio mimbwa, ni minyama ya porini sema binadamu mmeilazimisha kuifuga na matokeo yake ndio inawatafuna wamiliki,inakumbuka asili yao.
Uko sahihi wewe unaongelea mbwa koko mimi naongelea mbwa ambao kwa asili ni walinzi. Kifupi unapokuwa unafundishwa kuhusu mbwa unakumbushwa mbwa ni risasi ambayo iko tayari chemba inasubiri kufyatuka. Hivo ni juu kuendelea kubaki na hao koko au kufuga mbwa wa kisasa uendane na kanuni bora za namna ya kuwafuga au uzipuuze siku moja wakutafune
 
Kwa hiyo hao walinzi pua zao hazina uwezo wa kutambua harufu ya bosi wake.Yaani hata panya wa SUA wanawashinda kweli?
 
Kwani harufu ya tajiri wao hawaijui kama hawa makoko yetu ukiwa hata mita 300 tu kashakutambua.

Hyo mnayomiliki nyie sio mimbwa, ni minyama ya porini sema binadamu mmeilazimisha kuifuga na matokeo yake ndio inawatafuna wamiliki,inakumbuka asili yao.
 
Attachments

  • VID-20221206-WA0002.mp4
    1.3 MB
Back
Top Bottom