Kwa wale wapenda mbwa tuchukue tahadhari

Me ngoja niendelee kukomaa na hawa hawa kina bobi na tiger, wik end nawapeleka mtoni kusaka kenge.
 
Kuna mbwa baadhi ya watu wanavutishwa mineli aka bangi sijui hili mko aware nalo?
 
Sifugi, sitafuga na sitaingia Nyumba wanayofunga Mbwa hawa wa kisasa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie nna wajukuu sahv kwa paka wangu.
Na anazaa yulee, yaan anapenda ngono balaa.

Mi sitakii hiv anabeba mimba umri gani?nimpeleke wapi sitaki wajukuu
 
Daah aisee kumbe pana nyuzi kabisa ya kufundisha jinsi ya kutunza mbwa mimi niliwahi uza mbwa ninaempenda sana kisa alikua mkali kupita kiasi yaani alikua anatutambua watu wawili tuu hapa nyumbani hasa ikiwa usiku ingawaje ilikua ni nadra sana watu kutoka usiku...nilikua na ukuta mrefu ila kutoka kwenda nje kawaida harafu asubuhi ndio anakuwa nje kusumbua wapita Njia nikaamua kumuuza ingawaje nilikua ninampenda sana...nilichogundua ntatafuta mbwa wa kienyeji tuu wawili basi hao waki Germany wamenishinda unakua kama umefuga Simba nyumbani..
 

Haya mambwa ya kizungu mengi wanachanganya mbegu na wanyama pori kama wolves, fisi, mbwa mwitu nk nahisi wengine wanachanganya hadi na mamba manake haiwezekani mbwa mda wote yeye anawaza kung'ata tuu..! Halafu hayana akili yanang'ata hadi watoto wadogo wakati mbwa wetu wanajua kabisa huyu ni mtoto wanacheza nae.
 
Mbwa ni mnyama mmoja anayependa sana urafiki na binadamu, anahitaji muda lakini pia anapenda kudekezwa na kufundishwa toka mwanzo. Ila kuna aina ya mbwa kama Rottweiler anahitaji special interaction, lots of caressing, and games to remain active and entertained.

Ni muhimu pia kupewa elimu na mafunzo kabla hujaanza kuishi naye.
 
Napenda sana mbwa ila mbwa wa vile nimewakataa mbwa akitoka bandani yaani anasimamisha masikio mpaka ajue huyu ndie boss anatulia wakati nina mbwa wangu hapa ukimfungulia ana upendo balaa yaania unaona anashukuru kwa unavyomfanyia sio wale Fisi maji...wao wanajiona wana haki ya kila kitu mbwa gani hao...
 
Pana mbwa aligongwa na boda boda akawa yupo mtaroni sijui alivunjika kiuno naenda Mjini nikamwona nikampotezea niliporudi nikamkuta pale pale analalamika nikasema potelea mbali wacha nikachukue mfuko nikamwita mtoto tukambeba mpaka nyimbani nikamweka sehemu nzuri nikaanza kumnunulia chakula alilala kama siku tatu tuu ya nne akaamka bonge la mbwa harafu ni mkali kagoma kwenda kwao nilitangaza wenyewe wakaja kumfata kila wakimchukua anarudi kazi ninayo kwa jinsi alivyo hata kumpiga mkwara unajifikiria mara mbili mbili...ila ana upendo saana..
 
Sio mbwa tu hata haonwanaoweka umeme kwenye fensi.

Hivi karibuni umeme kwenye geti umempoteza mtoto kwa uzembe wa mzazi wake mwenyewe.
 
Mbwa wakali kwaajili ya matajiri pambaneni
Mi nauliza nimpeleke wapi paka wangu akafungwe kizazi asizae naona katakuwa kamalaya haka
Ni rahisi sana. Nenda duka la madawa ya migugo nunua dawa ya kufunga kizazi Cha paka ,omba wakupe maelekezo namna ya kuchoma sindano. Unaenda kumchoma sindano kwa maelekezo utakayopewa na daktari wa mifugo. Ni sindano tatu tu hatozaa tena.

Ukishindwa mtafute daktari wa mifugo aliye karibu nawe akupe muongozo
 
Chombo kama hii ukifanya mzaha inakumaliza chap
 
Mbwa wakali kwaajili ya matajiri pambaneni
Mi nauliza nimpeleke wapi paka wangu akafungwe kizazi asizae naona katakuwa kamalaya haka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbwa wakali kwaajili ya matajiri pambaneni
Mi nauliza nimpeleke wapi paka wangu akafungwe kizazi asizae naona katakuwa kamalaya haka
Paka fuga dume tu jike ni majanga... maana wakiwa kwenye muda wao wanatoa scent mtaa mzima paka wanaamia kwako😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…