Kwa wale wapenzi wa soka tu, pitia hapa (inaweza ikakusaidia)

Kwa wale wapenzi wa soka tu, pitia hapa (inaweza ikakusaidia)

Simbamteme

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
804
Reaction score
2,131
Kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuchizika sana na mipira....najua tunavyopata tabu kulipia DSTV kuangalia mipira mbalimbali ya ulaya..vifurushi bei ghali, inatulazimu tu kwenda kuangalia kwenye vibanda umiza..sasa leo nimeonyeshwa mbinu 1 na mzee flani sijaamini..ikabidi anipeleke kwake(ni mfanyakazi mwenzangu)eeeh bhana eeh..Mzee anakamata.

1..Beinsport 1,2,3 zote HD
2..CANAL SPORT 1,2,3,4,5
3..CANAL SPORT HD na CANAL HD
4.AZAM SPORTS 1 na 2
5.RCM SPORT 1 na 2
6.EURO SPORT 1 na 2

Na nyinginezo nyingi(kama 7+ hv za michezo za Ulaya). Pia channel za kibongo za FTA zote anazishika ikiwemo Animal planet... na wale wazee wa MINYANDUANO kuna Channel kama 2 hivi zenyewe ni 24/7 minyanduano...kifupi zipo nyingi, nyingne nimezisahau.

Amenambia hii mbinu alianza nayo kitambo sana,sema kipindi hicho kwa vile MODERM hazikuwepo walikuwa wanakamatika kirahisi hvyo ilimlazimu awe anabadili uelekeo wa Dish mara kwa mara,pia channel zilikuwa zina stuck stuck sana,lkn kwa sasa hayo mambo hakuna...huyu mzee anaangalia mipira yote ya Ulaya,America(ikiwemo Copa America inayoendelea kwa sasa)na Africa kwa bundle la buku 10 tu kwa mwezi

ANAFANYAJE!?

Kwanza unatakiwa uwe na dish la futi 8-10,ila futi 10 ni zuri zaidi..haya madishi yanapatikana sana madukani ila pia yametelekezwa sana kwenye nyumba za watu waliokuwa wanatumia FTA Enzi hizo

Pili unatakiwa uwe na Moderm ya 4G ya mtandao wowote(inategemeana na ulipo mtandao upi una kasi ya internet)

Tatu unatakiwa uwe na kin'gamuzi cha aina ya STARSAT(Nime attach picha yake)..Vinapatikana sana Kariakoo kwa bei isiyopungua laki 2 na kitu..au unaweza kuagizia hata ALI EXPRESS kwa bei nafuu au hata ebay

Nne unatakiwa uwe na LNB..kwa maelezo yake amesema ukipata ile ya ZUKU ya KENYA ipo strong sana kwenye kunasa..ila hata hizi nyingine hazina shida sanaa ila alipendekeza hiyo

Baada ya kuwa na hivyo vitu unamuita Fundi..anakusetia..awe fundi mwenye kile kifaa cha ku search signal...sio hawa wa kubabaisha

Ukishapata signal..unachotakiwa kufanya unaingia kwenye mtandao wako..unajiunga na kifurushi cha mwezi cha internet(yeye anatumia zantel/halotel) so kwa 10000 anapata GB 10 kwa mwezi na anasema zinatosha kabisa(haziishi) hata kama utaangalia 24/7

Baada ya hapo utaanza kula mambo vizuri kabisa tena kwa mwonekano an'gavu(HD) kwa baadhi ya channel

Anasema kama internet ya mtandao husika itakuwa inazingua huwezi ona hizo channels ila za KIBONGO utaoziona bila ya hata kutumia MODERM

Hiko kin'gamuzi kina sehemu ya kuchomeka moderm

NB..Nilishindwa kupiga picha kwani sikwenda na simu ya camera

Kama kuna mdau atakuwa na SWALI uliza hapa hapa,kama ntaweza kulijibu ntalijibu,kama ntashindwa ntamuuliza huyo mzee(maana ni mfanyakazi mwenzangu)

UPDATES

Kwa sasa wameleta akaunti mpya ya FOREVER ambayo unanasa channel zote za michezo za DSTV kwa tsh 15000 tu kwa mwezi...uwe na dish tu la DSTV kazi imeisha

Channel za azam wamezifuta kwa sasa sijajua tatizo n nn

Adios
20210703_211102.jpg


20210703_211102.jpg
 
Hayo ndo Mambo ya IKS
Mtwara watu wanakula maisha kwa madish madogo tu. bando ni kidogo sana gb 2 kwa mwez haiishi, ukiwa ukanda wa kusin mwa nchi package simple Ni hiyo anayotumia huyo mzee Ila Kuna channel za Israel nazo zinatunguliwa kwa mtindo huo hasa wale wa mikoa ya magharibi na Kanda ya ziwa. Tusiongee sana hii kitu ni ilegal
 
Kama a natumia internet ina maana haina tofauti na mtu anaetumia app ya android ama website wanazotumia kwenye pc. Hio ni iptv.

Hapo itakuwa tu hio decoder ina support iptv.
No, sio iptv
 
Hayo ndo Mambo ya IKS
Mtwara watu wanakula maisha kwa madish madogo tu. bando ni kidogo sana gb 2 kwa mwez haiishi, ukiwa ukanda wa kusin mwa nchi package simple Ni hiyo anayotumia huyo mzee Ila Kuna channel za Israel nazo zinatunguliwa kwa mtindo huo hasa wale wa mikoa ya magharibi na Kanda ya ziwa.
Ni uelekeo gani huo plz kwa sie wa kanda ya ziwa..??
 
Hayo ndo Mambo ya IKS
Mtwara watu wanakula maisha kwa madish madogo tu. bando ni kidogo sana gb 2 kwa mwez haiishi, ukiwa ukanda wa kusin mwa nchi package simple Ni hiyo anayotumia huyo mzee Ila Kuna channel za Israel nazo zinatunguliwa kwa mtindo huo hasa wale wa mikoa ya magharibi na Kanda ya ziwa. Tusiongee sana hii kitu ni ilegal
Fafanua mkuu niko nachingwea maumivu ya dstv yananitesa sana Sana
 
Fafanua mkuu niko nachingwea maumivu ya dstv yananitesa sana Sana
Kuna risiva maalum zenye uwezo huo, mfano star sat, mediastar, gt media, n.k, ukinunua mpya inakuja na account ya forever server ya mwaka 1 isipokua gt media ambayo inasupport cccàm. Kuna wauzaji/mawakala wanaoshughulika na accounts
Dishi lielekeze uelekeo husika 16e kwa Kanda ya kusini wakati huo Receiver inaungwa na internet, na freq husika ziingize kwenye receiver

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ndo Mambo ya IKS
Mtwara watu wanakula maisha kwa madish madogo tu. bando ni kidogo sana gb 2 kwa mwez haiishi, ukiwa ukanda wa kusin mwa nchi package simple Ni hiyo anayotumia huyo mzee Ila Kuna channel za Israel nazo zinatunguliwa kwa mtindo huo hasa wale wa mikoa ya magharibi na Kanda ya ziwa. Tusiongee sana hii kitu ni ilegal
Ungefunguka kidogo mi naomba maelezo hata pm
 
Back
Top Bottom