Kwa wale wenye magari na ambao hampandi daladala, hivi ndo vioja tunavyopata kwenye daladala wenzenu tusio na magari!

Kwa wale wenye magari na ambao hampandi daladala, hivi ndo vioja tunavyopata kwenye daladala wenzenu tusio na magari!

Huku mambo ni moto,sijui ndio kuvurugwa na maisha...

Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!? Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado hajatoa album...

Abiria: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia ndoo?! "

Abiria: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako!? hebu tupunguzie misheria"

Mmama: "Bwana ondoa gari joto sana!!",
Konda: "Usituzingue wewe, shuka upande fridge...."

Konda: "Anti, kuna siti pale nyuma, ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"

Sister duu: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa huzisemi, kama ulitaka kujiachia ungekodi treni peke yako!!!"

Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa kiti si ungebeba cha kwako!!?"
Konda anatangaza, wenye hela kubwa (elfu kumi) au inatokea unampatia noti ya elfu kumi, then anakuambia atakupa chenji, mnafika kituo unachoshuka unamwambia nipe chenji yangu, anakuambia, dah nimekosa chenji basi wewe chukua tu hela yako (ile elfu kumi) acha mi nile hasara, basi unafurahi unaondoka zako na kumshukuru konda, kumbe umepewa noti feki, hiyo ndiyo bongo dari salama
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom