grand millenial
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 3,943
- 5,550
Mwenyezi mungu (subhanna huwata allah ) amewapa majini sheria zao kutokana na maumbo yao yalivyo.Shirki ni kuabudu chochote kisichokuwa mwenyezi Mungu kukitegemea kama muumba.
Kukiri kuwa hakuna Mungu isipokuwa chenyewe na kuomba au kusali kwa imani kama sanamu, mizimu, majini, jua n.k
Lakini kuwa karibu au kuzungumza na hivyo shirki yake inakuja kwenye kukiabudu.
Pia neno shikri sio uchawi.
Uchawi ni kitu kingine na shirki ni kitu kingine na pia shirki sio miujiza. Miujiza ni jambo lingine na shirki ni jambo lingine,
Achilia mbali Shirki na Ushirikina kwa waswahili wenyewe hawawezi kukupa maana ya utofauti wa maneno haya shirki ikisema maana yake ni kuabudu asiye kuwa Mungu na USHIRIKINA wanakwambia ni uchawi.
Hali ya kuwa ni neno moja likiwa na mitajo tofauti lakini linalazimishwa kuwa na maana mbili tofauti.
Rakims
Vile vile sisi tumewekewa sheria zetu ambazo nadhani unazijua.
Sheria walizowekewa majini ni hizi hapa kwa uchache.
1.kutokuvuka mipaka(boundaries ) waliyowekewa na kuchanganyana na binadamu walaa kushirikiana nao kwa lolote.
Jini atakayevunja sheria hii moja kwa moja ataingia kundi la masheitwani (jua kuna masheitwani ya kibinadamu na kijini) sasa wewe una sheitwani ambalo lipo ndani ya mwili wako .
2.kumuabudu Allah (subhana huwataallah).
Sasa point yangu hasaa ni hapo namba moja,majini hayatakiwi yaingiliane na kushirikiana na binadamu kwa lolote .
Maana kufanya hivyo kutapelekea kumuasi Allah (subhanna hu wataallah)
Maana ili Jini akusaidie kuna masharti anayotaka itabidi ufuate yaani nipe nikupe na hii tumeona kwenye visa vingi vya kiislamu.
Sasa wewe unaye watumia hao majini labda nikuulize unataka ilmu ipi hasa au unayatumia kwa kipi ambacho Allah hawezi kukupatia ?
Kumbuka yenyewe ni viumbe pia na vinahitaji kula , kulala na kuzaliana sasa unapomuweka kwenye mwili wako unadhani atakula nini? Kama sio ndo kuanza kuwekewa masharti mpaka ya kuvaa , kula na kafara nyenginezo?
Naomba majibu hapo ☝.