Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Je yule mwalimu wa madrasa pale mtaa wa mafia na sikikuu bado yupo na madrasa inaendelea?
 
Naikumbuka Dar enzi hizo stand ya mabasi ya Arusha / Moshi ikiwa Kisutu. Ilikuwa raha sana unaanza safari Arusha saa 9, unafika Dar alfajiri unafanya shughuli zako na kugeuza saa 9 kurudi Moshi
 
Je yule mwalimu wa madrasa pale mtaa wa mafia na sikikuu bado yupo na madrasa inaendelea?
Mama Chupaki pale Madrasa panatambulika kama Al-jumaa, Maalim wa pale sijui unamzungumzia Marhum Sharrif Juneid. Siku hizi pale kuna Zahanati (Dispensary).
 
Mama Chupaki pale Madrasa panatambulika kama Al-jumaa, Maalim wa pale sijui una mzungumzia Marhum Sharrif Juneid. Siku hizi pale kuna Zahanati (Dispensary).
Naulizia ile madrasa aliyokuwa inafundishwa maalim Abubakar Mzinga.
 
Mie nakumbuka siku za sikukuu tulikuwa tunaenda kidogo chekundu kumuangalia farook mkata viuno.
Na yule shoga maarufu sana marehemu Kitwana wa mitaa ya kariakoo.
 

Basi matusi ni asili ya Faiza Foxy.
 
Mkuu hapa sasa umempa uhakika huyu jamaa uliposema hadi nguzo za umeme na hata taa ni zilezile kabisa kwa kweli umeitendea haki picha yako katika kufananisha, hongera sana
 
Angalia picha ya tarehe 1/3/2017
[emoji116] [emoji116] [emoji116]


Picha ya kale
[emoji116] [emoji116] [emoji116]


Mkuu Mlaleo karibu utoe maoni yako picha ulizozitaka umeziona?
 
Mkuu Mlaleo
Tunaendelea kueleweshana kuhusu picha za Dar-es-salaam

Angalia hapo hizo picha tatu

Picha ya kale
[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Picha ya 2017 Mtaa wa uhuru/kichwele
[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Picha ya 2017 Mtaa wa Nkurumah
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
 
Reactions: bbc
Sina picha za kuweka lakini 1962 kulikuwa na Peugeot Mgongo wa .... Kisha pale Mnazi Mmoja Hospital palikuwa na chemchem ikirusha maji, watoto tukipenda kuogelea lakini maaskari walikuwa wakitutimua, tulitoka nduki na nguo zetu mkononi!
 
Jamani mmenikumbusha class mate wangu Mussa Simba tulisoma wote Tambaza nae akiichezea Congo United miaka hiyo.Mwenye taarifa zake tafadhali anicheki inbox.Natanguliza shukrani.
Mie nilisoma na Aluu Ally wa Simba pale Azania ila alisoma kwa muda mfupi sijui yuko wapi huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…