Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Mkuu Zamiluni mi nimesoma St Joseph Mwalimu wangu mkuu alikuwa Mrs Simkoko! Snow cream na Fish and Chips maeneo ya Shesh Mahal na Topaaz ndiyo anga zangu. Beano,Dandy,Topaaz ndiyo Comic zangu. Unataka ni kwambie kitu! sikukuu ya Idd nilikuwa natembelea wapi utotoni? Mji umeharibiwa! kidongo chekundu ndiyo maeneo yetu! Mnazi mmoja garden pamevurugwa hata chemchem hazirushi maji na samaki hakuna kwenye ile sanamu inatoka maji! Viatu nilivyokuwa navaa ni Prefect za Bata![emoji23] mi nilikuwa hodari wa kutengeneza kishada/tiara[emoji324]
Lakini klabu yangu ni ile ya mitaa ya Mafia na Nyamwezi [emoji460]
Mi ni kama Robinson cruise
Namshukuru Mwenyezi Mungu nimeona mengi alhamdulillahi.
Je yule mwalimu wa madrasa pale mtaa wa mafia na sikikuu bado yupo na madrasa inaendelea?
 
Naikumbuka Dar enzi hizo stand ya mabasi ya Arusha / Moshi ikiwa Kisutu. Ilikuwa raha sana unaanza safari Arusha saa 9, unafika Dar alfajiri unafanya shughuli zako na kugeuza saa 9 kurudi Moshi
 
Je yule mwalimu wa madrasa pale mtaa wa mafia na sikikuu bado yupo na madrasa inaendelea?
Mama Chupaki pale Madrasa panatambulika kama Al-jumaa, Maalim wa pale sijui unamzungumzia Marhum Sharrif Juneid. Siku hizi pale kuna Zahanati (Dispensary).
 
Mama Chupaki pale Madrasa panatambulika kama Al-jumaa, Maalim wa pale sijui una mzungumzia Marhum Sharrif Juneid. Siku hizi pale kuna Zahanati (Dispensary).
Naulizia ile madrasa aliyokuwa inafundishwa maalim Abubakar Mzinga.
 
Mie nakumbuka siku za sikukuu tulikuwa tunaenda kidogo chekundu kumuangalia farook mkata viuno.
Na yule shoga maarufu sana marehemu Kitwana wa mitaa ya kariakoo.
 
Mkuu Umechemsha sio Kichwele hapo huo ni Mtaa wa Nkuruma kushoto ni Petrol Station ya Total au Esso kipindi hicho na hilo Jengo mbele ya Petrol Station kwa Sasa ni Duka la National Tyre. wahindi wanauza Matairi na mambo mengine kwa bei kubwa kuliko maelezo. Upande wa kulia kuna jumba la Sinema la New Chox..

Kichwele Mtaa wake ulibadilishwa jina na Ukaitwa Indira Gandhi kipindi hicho alipoitembelea Nchi akazawadiwa Mtaa. na Jina la Mtaa wa Market nadhani ndio wa kwanza and then soko likafa ukaitwa Kichwele and the Indira Gandhi.

So huo Nkuruma kama nao uliitwa Kichwele nirekebishe. Maana Mimi nilikuwa Mkazi wa City center miaka ya mwanzo ya 80's so nilikuwa nazunguka sana kutafuta company ya watoto mitaa yote kucheza maana ilikuwa ni shida watoto kupatikana mitaani kucheza.

Watoto wa Kariakoo enzi hizo Matusi na wizi yaani wanakupora wazi wazi and then walikuwa wachafu even kina FaizaFoxy

Basi matusi ni asili ya Faiza Foxy.
 
e0ad3c0aa440ec1a7e3b74a136e0678a.jpg

Huyo twiga aliuzwa wapi
ilikuwa wapi hiyo mtaa gani?
 
Mkuu upo Dar? Kama upo Dar pita hilo eneo mchana wa kesho piga picha kisha ilete hapa hiyo view ya kutokea mnara wa saa kulia mwa picha hayo majengo ni tofauti na picha ya kale.
Hebu tazama hii picha nyingine ya jana
2083a47bd48499d16324888e3f0abcac.jpg

c7281619d4b00abd5a66b6259185ed35.jpg

34d5a3af42ad94169b65264f6576f5b0.jpg

Angalia mpaka nguzo za umeme bado ni zilezile za kale [emoji15] [emoji15]
Mkuu hapa sasa umempa uhakika huyu jamaa uliposema hadi nguzo za umeme na hata taa ni zilezile kabisa kwa kweli umeitendea haki picha yako katika kufananisha, hongera sana
 
Angalia picha ya tarehe 1/3/2017
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
b07bcdbb8004df4c5c0b2d3b0a4f9ec3.jpg

42ab892bff87c33b27762b73dd2a2cbf.jpg

Picha ya kale
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
fb7c7382c8f731ee931f88033b18b077.jpg


Mkuu Mlaleo karibu utoe maoni yako picha ulizozitaka umeziona?
 
Mkuu Mlaleo
Tunaendelea kueleweshana kuhusu picha za Dar-es-salaam

Angalia hapo hizo picha tatu

Picha ya kale
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
84fff7590f5c7dc285fadf211c5bdbe0.jpg

Picha ya 2017 Mtaa wa uhuru/kichwele
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
2354fede23a7610ff0775ba61ebccd56.jpg

Picha ya 2017 Mtaa wa Nkurumah
[emoji116] [emoji116] [emoji116]
80aace88c54a70137b7beca3401b57f4.jpg
 
  • Thanks
Reactions: bbc
Sina picha za kuweka lakini 1962 kulikuwa na Peugeot Mgongo wa .... Kisha pale Mnazi Mmoja Hospital palikuwa na chemchem ikirusha maji, watoto tukipenda kuogelea lakini maaskari walikuwa wakitutimua, tulitoka nduki na nguo zetu mkononi!
 
Jamani mmenikumbusha class mate wangu Mussa Simba tulisoma wote Tambaza nae akiichezea Congo United miaka hiyo.Mwenye taarifa zake tafadhali anicheki inbox.Natanguliza shukrani.
Mie nilisoma na Aluu Ally wa Simba pale Azania ila alisoma kwa muda mfupi sijui yuko wapi huyu jamaa
 
Back
Top Bottom