Kwa wale wote tusiokua na bahati, tukutane hapa kupeana moyo.

Kwa wale wote tusiokua na bahati, tukutane hapa kupeana moyo.

Unajisomea kuanzia mwezi wa kwanza ili kuja kuukabili mtihani wa mwezi wa tisa.

Kisha unafaulu.

Huku kufaulu kulikotokana na maandalizi ndiyo bahati yenyewe?

Nashindwa kuunganisha kati ya maandalizi na bahati. Kwa watu wengi bahati hua siyo chaguo hauwezi kuchagua ni inatokea tu ghafla.

Wanaosema "Wish me luck" wanamaanisha "Wish me I get to prepare for this and wait for the right opportunity"?
Nasema hivi, tengeneza mazingira rafiki ya kupata bahati.

Kama unataka kushinda bahati nasibu, angalau soma mchezo ukate tiketi.

Sio hujasoma mchezo, hujakata tiketi, unasubiri radi ipige ofisi za bahati nasibu ipasue milango halafu upepo upeperushe tiketi, uvunje dirisha lako na kuiweka tiketi iliyoshinda mezani mwako.
 
Mm kila demu nayetongoza ananiambia ana MTU tyr tena wa malengo kabisa....gundu hili...nmeamua niachane kwanza na mambo ya wanawake
Tafuta kwanza maisha. Ukiwa vizuri milango itafunguka yenyewe. Utaona wanavyo jigongesha kwako
 
  • Thanks
Reactions: k29
Back
Top Bottom