kwa walimu wenzangu mnaosubiri ajira kutoka serikalini

kwa walimu wenzangu mnaosubiri ajira kutoka serikalini

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
kwanza lazima tumshukuru Mungu kwa kupata elimu hii tulioipata!! umepata degree,diploma au chet yote ni Mungu Amekusaidia! Kumbuka Wale Wenzako Ambao Wameishia Darasa La 7 Na Leo Hii Wana Familia Na Maisha Yanasonga! We Uliepata Cheti Je Si Zaidi? Najua Utasema Umesomea Kazi Ya Ualimu Sasa Utafanyaje Issue Zingine? Iko Hivi Kila Jambo Lina Makusudi Yake! Mimi Sasa Silalamiki Au Kujilaumu Kwanini Ajira Hizi Zinachelewa!! Kama Mhanga Wa Ajira Hizi Niwashauri Wenzangu Mambo Kadhaa.
~tuache Kusikiliza "tetesi" Kuwa Ajira Ziko Hivi Au Vile...Kama Ipo..Ipo Tu.
~kama Unaweza Kupata Mahali Ukajishikiza Kufanya Kazi Hata Kwa Mshahara Mdogo Ni Bora...something is better than nothing.
~tumuombe Mungu Atusaidie Na Aisaidie Nchi Yetu Tukikumbuka Kuwa Tumeacha Wadogo Zetu Vyuoni Ambao Wanasomea UALIMU!
~mwisho tuRELAX tuache mawazo...

sikiliza wimbo wa Tom Walker...He Knows My Name.


Allan.
 
Na kweli kama ipo ipo tu Bwana watabiri wamekuwa wengi sana mtu anaruka na katopic kake tu unakuta hakana hata source ya waandishi wa habari waliosajiliwa
 
Mungu akubariki sana kwa kunifariji ,
Nimepata tempo nalipwa 150000
 
Mungu akubariki sana kwa kunifariji ,
Nimepata tempo nalipwa 150000

its better mkuu! ungekaa home ungeipata wap iyo? ajira zikitoka unapata hela ya nauli za mazaga mengine!
 
Ushauri mzuri ila binafsi sipendi mtu aseme kama ipo ipo tu, inamaanisha huyo mtu amekata tamaa na anasubiri bahati itokee, if you wait for the lucky means you dont have skills.
 
Mmmh yani mi nikae niiombee nchi? Nchi ni nani? Ni nini?viongozi wenyewe hawana muda wa kuombea nchi yao ndo miye loh kila mtu na msalaba wake Ntajiombea mwenyewe na familia yangu khaa!
 
Mungu akubariki sana kwa kunifariji ,
Nimepata tempo nalipwa 150000

Hakika ww ni mwalimu kwa andiko lako mwanana na lenye kila buheri hakika umenikosha kwa mawazo yako, mm nimepata tempo nalipwa 362,000.
 
Hakika ww ni mwalimu kwa andiko lako mwanana na lenye kila buheri hakika umenikosha kwa mawazo yako, mm nimepata tempo nalipwa 362,000.
Hongera sana,tambua kupata kazi ni bahati kubwa sana na usinikebehi kwa kuwa mshahara wko mkubwa kwangu,
Wapo wanao lipwa zaidi ya milion tena unawazidi elimu so usitambe sana bwana mdogo.
 
Hongera sana,tambua kupata kazi ni bahati kubwa sana na usinikebehi kwa kuwa mshahara wko mkubwa kwangu,
Wapo wanao lipwa zaidi ya milion tena unawazidi elimu so usitambe sana bwana mdogo.


mwałimu kwa mwalimu USO KWA USO
 
Back
Top Bottom