Kwa walimu wote.

Kwa walimu wote.

Ushauri wa MTUMISHIDC angeupeleka serikalini ungefaa zaidi. Laiti ungefanya utafiti wa hata saa moja katika shule za sekondari zilizo nyingi ni zaidi ya FUKAMA, labda ni LIBIKU yaani LIPWA BILA KUFUNDISHWA kabisa. Kuna maticha mwaka mzima anatoa tu notis, tena notis za hesabu na fizikia, inatisha. Bila kujifunza kutoka NCHI KAMA ZA NORWAY hatuwezi kufika. NORWAY walimu ndo wanaolipwa vizuri zaidi ya kada zingine hata kama scale za watumishi waliowengi hazitofautiani sana. HATA WAKITUNGA SILABUS NZURI BILA KUWAWEZESHA WALIMU NI KAZI BURE. Mfano mzuri unatoka shule za Private ambako kidogo wanavimishahara vikubwa wanafanya vizuri.
 
Kutokana na Serikali kuwadharau Walimu, Kila mwalimu ajiunge na sera inayoitwa FUKAMA yani FUNDISHA KULINGANA NA MALIPO, mda unaobaki kafanye shughuli zako.

wewe ndio unagundua sasa? mbona wenzako tunaitekeleza sera hii siku mingi? ndio maana hata mshahara ukiwa mdogo hatulalamiki kwani tunahakikisha tunatengeneza mshahara mwingine ili kwenda sammbamba na wenzetu wa kada zingine mambo ukiyapangilia utajikuta unamzidi hata BANK TELLER mwisho wa mwezi ila ukijifanya 'MZALENDO' kwenye nchi ya kifisadi utakufa siku sio zako!
 
watakazana wakati wana njaa??? matokeo ya kukazana kwao yataonekana baada ya muda gani?? Kwa nini sekta nyingine wakikohoa kidogo tu wanasikilizwa na sio waalimu????

na hilo ndilo tatizo la serikali hii ya kibaguzi lakini walimu huwa wananiumiza wakati wa kuihukumu ukifika wao wanabaki kuwa makada na kuacha kuuhamasisha umma kuiondoa madarakani!
pamoja na kubaguliwa haiwapasi kuwahukumu watoto kwa kutoifanya kazi kwa bidii, naendelea kuwashauri wakiona ualimu haulipi badala ya kutofanya kazi kwa bidii ni vyema kuiacha kabisa na kuangalia mustakabali mwingine wa kimaisha!
 
Mahonzelo serikali hii si sikivu, pili ina ajenda ya siri ya KUKUZA UJINGA TANZANIA ILI IWE RAHISI KUTAWALIKA, tatu wanalo kundi la wachache wanaloliandaa ili kuwatawala watanzania nalo ni watoto wao na jamaa zao.
Nafahamu vyema yanayofanyika mashuleni hasa kwenye shule za msingi na za kata ukijaribu kuyasemea kwa bidii wanakuandalia kitu chenye ncha kali na kwa sababu wamegoma kupokea ushauri na kuruhusu watendaji wenye nia njema na elimu ya tanzania wafanye kazi basi umefika wakati wa kuwaondoa madarakani ili kuujenga mfumo mpya maana uliopo ni mfumo mfu ulio kwenye jeneza tayari wasuburi kuzikwa!
yapo mambo mengi ya kujifunza kwa wenzetu walioendelea kwa mfano hilo la kuwalipa vizuri walimu lakini pia kuchukua walio na uwezo ndio wawe walimu na si wasio na uwezo kitaaluma na hii pia ni sababu nyingine inayowafanya walimu wasijiamini na kujisimamia wengi wao ni dhaifu kitaaluma na kiweledi na ndio maana wananyenyekea hata hiko kidogo wakipatacho!
 
Last edited by a moderator:
wewe ndio unagundua sasa? mbona wenzako tunaitekeleza sera hii siku mingi? ndio maana hata mshahara ukiwa mdogo hatulalamiki kwani tunahakikisha tunatengeneza mshahara mwingine ili kwenda sammbamba na wenzetu wa kada zingine mambo ukiyapangilia utajikuta unamzidi hata BANK TELLER mwisho wa mwezi ila ukijifanya 'MZALENDO' kwenye nchi ya kifisadi utakufa siku sio zako!
uzalendo ndio utakalo liokoa taifa, ukishindwa kuwa mzalendo hata hao watoto unaowanyima haki yao ipo siku watakufungia darasani na kukutenda ambayo hutaamini waulize walimu wa kilwa na kibiti wakufahamishe matunda ya kutotimiza wajibu wao kama wazazi, walezi na walimu!
 
Nakumbuka kauli alioitoa Edward Lowasa mwaka 1994 nikuwa chuo cha ualimu Monduli akimtetea mkuu wa chuo wakati huo (Def) Kuwa "if you are looking for the green pasture then you are in wrong way".Sakata lenyewe lilikuwa linahusiana na kula ugali mfululizo wakati fedha za kununulia mchele zikiwa zimefisadiwa.
Sasa hilo linadhihirika waalimu wakiwa wanataabika na familia zao,wanadharaulika na jamii ambayo wanatarajia watoto wao watafundishwa na walimu hao hao.
Na wasihi walimu wajiendeleze na fani zingine bila kusahau ujasiria mali ambao utawatoa kimaisha na waache kukopakopa ovyo kwenye vyombo vya fedha vya mafisadi kule unapokopa 1million na unalipa 4million.Na kule tunapoacha kadi za benki rehani.
Tuwasaidie watoto wa wakulima maana hao wanao tufanyia ufisadi watoto wao wanasoma shule za bei mbaya na pengine nje ya nchi,hivyo wanaweza wasiathirike na "FUKAMA" ikawa ni sawa na unajipiga na bastola kwenye mguu wako mwenyewe.
Tushirikiane kudai haki zetu kila moja kwa nafasi yake,wilayani ofisi za elimu ndo usiseme Mafisadi wa kutupwa,miungu watu,wana wahujumu walimu wenzao.

Kama haki inadiwa na haipatikani tufanyaje?
 
"tatizo ni kwamba wakaguzi wa shule wanakula viyoyozi maofisini lakini laiti wangekuwa wanapita kwenye shule za kata maarufa kama "saint kayumba" wasinge rudia tena kucheza game maofisini maana hali ni mbaya" na mbaya zaidi wanaoumia ni watoto wa mkulima kama mimi" walimu baada ya kutishiwa wakitaka kuandamana kudai stahiki zao,sasa kila mmoja ameamua kugoma kwa style anayoweza wengine wanaishia bustanini,wengine kwenye mazizi ya ng'ombe,na wengine wanaumwa mafua miezi mitatu,sijui miaka ishirini ijayo tutavuna kizazi cha aina gani kama si majambazi wasomi"
 
Mimi ni mwalimu wa sekondari lakini nilisha acha kufundisha,nasubiri mwisho wa mwezi nichukue hicho kiduchu ambacho mafisadi serikalini weanakifanyia kwa dakika.
 
Nasikia Walimu na wauguzi wanaongoza kucheza kamari aka JACKPOT.hasa huku DOM sijui na kwingine vp
 
"tatizo ni kwamba wakaguzi wa shule wanakula viyoyozi maofisini lakini laiti wangekuwa wanapita kwenye shule za kata maarufa kama "saint kayumba" wasinge rudia tena kucheza game maofisini maana hali ni mbaya" na mbaya zaidi wanaoumia ni watoto wa mkulima kama mimi" walimu baada ya kutishiwa wakitaka kuandamana kudai stahiki zao,sasa kila mmoja ameamua kugoma kwa style anayoweza wengine wanaishia bustanini,wengine kwenye mazizi ya ng'ombe,na wengine wanaumwa mafua miezi mitatu,sijui miaka ishirini ijayo tutavuna kizazi cha aina gani kama si majambazi wasomi"
Wakaguzi hawapendi kucheza game maofisini,Hawatengewi fedha za kutosha kukagua,magari yao hayana mafuta,mpaka wakajipendekeze kwa wakurugenzi,unatarajia watakagua?kuna walimu feki wengi kwenye private schools,wageni toka nchi jirani mradi anaongea kiingereza anaajiriwa.
 
Mimi nilianza muda mrefu hiyo FUKAMA.ndio maana nilichukia mukoba kutangaza mgomo(aliniharibia dili zangu)
 
sasa mwaka unataka kuisha tangu nilipo anza kuidai serikali ya magamba mishahara yangu ambayo kwa uzembe wa viongozi waliopewa dhamana ya kutumikia ilisimamishwa kimakosa, nawashauri vijana walionje ya kadahii kuuliza maswahibu yanayo tukuma walimu kabala hawajaigia kwenye kada hii na kujuta milele.
 
tatzo ni sera yetu ya elimu, huwez ukachukua failures ndo wakafundishe taifa la kesho (tutaangamia), ndo maana elmu ya sasa ni tofaut na zaman. Mi naamin mwalim anatakiwa awe m2 mweny akl kupta wengne ktk darasa analosoma. Alaf ikitumika hiyo system ya FUKAMA anaeumia ni serkl au ni nani? 2nazd kujiddmiza, fundsha kwa juhud na moyo il mwanafunz wako aje kukuokoa. FUKAMA itasababsha watoto wa wa2 wa kpto cha vhini wazd kuddmia
 
Back
Top Bottom