Kwa waliofeli kidato cha nne.

Kwa waliofeli kidato cha nne.

STRATON MZEE

Member
Joined
Jan 4, 2012
Posts
59
Reaction score
17
As-Salamu Alaykum wana JF.
Wana jamvi wenzangu naomba msaada wenu wa kiushauri.
Kuna vijana walimaliza form four mwaka jana na matokeo yao yametoka mwaka huu, lakini kwa bahati mbaya wakafeli kwa kupata division zero. Sasa wameniomba niwape ushauri kuwa kwa matokeo haya, wanaweza kufanya nini ili kujitengenezea misingi ya maisha yao.
Wanachotamani wao ni kujua masomo au corse ambazo wanaweza kusoma, ili kufikia malengo yao ya maisha.
Tafadhali tuwasaidie vijana hawa, ili tuweze kujenga jamii yenye watu wanaojitegemea. Tukumbuke kwa kumsaidia mmoja kiushauri, tutakuwa tumeisaidia jamii nzima.
Naomba kuwasilisha.:lock1:
 
Pole mkuu kwa kupata zero,nakushauri nenda VETA.
 
Mh kama VETA wanachukua zero ni bora wakaenda pale.
Maana sidhani kama ni madully .
Hii kutaini kwa kuangalia mtihani wa mwisho kazi kwelikweli
 
Hao wajinyonge au wakaanzishe biashara ya kuvua samaki.OVER
 
Bwana dotto, JF si kijiwe cha kutupiana majungu na maneno yasiyo na maana. JF imebeba dhamana ya Watanzania 45,000,000. Wengine wanapoomba ushauri, si vizuri kuwakebehi. Wewe kama ulifaulu shuleni, mshukuru Mungu wako maana ndiye aliyekusaidia. Ingekuwa ni wewe ulifeli, halafu ukaomba ushauri ukajibiwa kwa majibu uliyoyatoa, ungejisikiaje? Kumbuka kumtamkia mwenzako mabaya si jambo la hekima hata kidogo, na halipaswi kufanywa na Intellectuals waliopo JF kama wewe.
Tafadhali jitambue na utambue nafasi yako hapa JF na katika Taifa hili kwa ujumla. Na kama hii ndo tabia yako, Jamii Forum si sehemu yako. Unaweza kuwaomba operators wakakutoa maana utakuwa ulikosea njia.

Mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima kuliko mwerevu akiongea.
Hao wajinyonge au wakaanzishe biashara ya kuvua samaki.OVER
 
Hao wajinyonge au wakaanzishe biashara ya kuvua samaki.OVER

Acha ukilaza wako bkoz hata we mwenyewe umepata viji-crdt viwili alafu unajiona umeweza kweli, Acha majibu ya kipumbafu so kama vp rudi zako 2 fcbk kuna wa2 kama wewe but usisahau kuresit pepa mwaka huu ili upte crdt uende 4m5 mwakani.
 
Serious,nackiackia kuwa sirikali ytu imeruhusu waliofeli warudi kdato cha pili lkn cna uhakika sasa cjui ni kwl? Kama ni kwl,nafac hyo waitumie vizur kwn naamin baada ya miaka mitano ijayo,hata kazi za ndani,vyeti vitatakiwa kw hyo mm nawashaur hyo nafac wakimbizane nayo!
 
sas hao ni vijana wa jinsia gani? halafu kama wanaweza wachukue form mwezi wa nane veta ili mladi uwe na leaving certificate veta unaingia bila chenga halafu wanakozi nzuri mno halafu bei naafuu sana kama ni pm nitakupa maelekezo for what you can do enjoy ur time
 
Back
Top Bottom