Tunataka Bodi ya mikopo waweke wazi vigezo wanavyotumia kutoa mikopo, kwani inaonekana form zinazojazwa hawazisomi.
Mtoto unakuta kuanzia nursary hadi advance kasoma private na kozi aliyochaguliwa ni non priority kapewa mkopo asilimia 100. na mwingine kasoma shule za kata kuanzia mwanzo hati mwisho advance kasoma kigonsela nae let say kachagua non priority unakuta kanyimwa.
n mwingine unamkuta kachagua Priority na kapata mkopo ila pesa aliyopewa its not 100% au kapewa fees yote ila kwenye meals, stationary kapigwa bao na dogo niliyemuelezea mwanzo
Pia nikadhani labda wamezingatia division, kuja kucheck wala hakuna isue ya division, kuna wenye div 1, 2 kali wamekosa.
sasa sielewi vigezo gani wanatumia kutoa hizo loan, maana kama vitakuwa wazi hawatopata mtu anayelalamika.