Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Nimefuatilia taarifa zinazosambaa kwamba Zuhura Yunus ni raia wa Uingereza nachelea kuziamini na kama Zina ukweli basi atakuwa ameupata huo Uingereza Kwa Siri sana. Nafasi aliyopewa lazima tukubali mambo makuu matatu;
Kwanza, ni wazi kwamba si nafasi yakufanywa na Raia wa Kigeni hata kama raia huyo ana uzalendo kiasi gani na ikibainika kwamba umedanganya Utaifa wako basi vyombo vinavyohusika mara moja vinatakiwa kumshauri Mhe. Rais atengue uteuzi wako. Tukumbuke Uraia ni siri na uteuzi pia ni siri ila ukishateuliwa pamoja na vetting iliyofanywa awali kabla ya uteuzi lazima uwajibike kutoa taarifa za kweli kuingia kwenye mfumo wa utumishi. Hapa hakuna kudanganya lazima ueleze ukweli hivyo naamini Zuhura anaweza kuondolewa pale ikibainika anazo taarifa za ziada zinazomwondolea sifa.
Pili, kama tunakubaliana kwamba Zuhura hana utaifa mwingine lazima sasa tumpongeze Mhe. Rais Kwamba amemteua mtu sahihi na mwenye sifa. Zuhuru amekubalika na pande zote akiwa ajawaza kwenda kufanya kazi ikulu. Hakuwahi kuwaza angefika alipo na hivyo ni sahihi kwamba jamii ilimfahamu kabla hata mamlaka azijamfahamu. Kama yeye Mwenyewe akufanya juhudi kulikuza jina lake asingepata malipo haya. Tukubali huyu ni zao la utendaji kazi unaoacha alama.
Tati, Kwa vijana na wanafunzi mnalo la kujifunza. Kuna siku nilitoa mada kuhusu umuhimu wa Idara ya Uhamiaji kuhamasisha Watanzania wasambae Duniani wakajifunze na pale watakapochomoka nakuonekana miongoni mwa Mamilioni wa watendaji basi itatusaidia pale tutakapotaka kuwatumia basi tuwatumie vyema. Kuendelea kukaa humu Ndani kusifu na kuandika mitandaoni masuala ya umbea, kuanza kujifunza unafiki wa uzalendo wa vyama vya siasa utotoni ukaacha kujifunza uzalendo wa kitaifa na kimataifa nikuziba mishipa ya fahamu na kudumaza ubongo. Vijana ondokeni nchini katafteni fursa nje, kafanyeni kazi mashirika ya Kimataifa, kafanyeni kazi nchi jirani mtalisaidia Taifa huko mbele. Mtajifunza uzalendo wa nchi KULIKO uzalendo wa vyama.
Mwisho, niwaombe sana mnapofanikiwa msiukatae Utanzania komaeni na Utanzania. Nilitamani sana kumwona Like akitumikia nchi yake anapoelekea uzeeni lakini waliokua naye wananiambia anatumikia Uraia wa Uingereza kwa Sasa. Laiti asingepata fursa ya uraia wa Uingereza naamini few years to come angerudi kuongoza mashirika au taasisizetu na kuleta western and civilized culture ndani ya mashirika yetu akaondoa uvivu na watu kujiandikia madokezo ya fedha za kula na familia zao bila kuangalia mustakabali wa taasisi wanazokabidhiwa.
Hongera Zuhura Yunus, Hongera Hillary na Hongera Kikeke mmetutambulisha.