Kwa wanachama wa NSSF Hakiki michango yako kupitia namba hii

Kwa wanachama wa NSSF Hakiki michango yako kupitia namba hii

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Kwa wanachama wa NSSF, hakikisha unakwenda sambamba na mwajiri wako kwa michango yako ya kila mwezi' kwa kufuata utaratibu
huu hapa chini:
KUJUA KIASI ULICHO CHANGIA KWA WANACHAMA wa NSSF:
Fuata maelezo yafuatayo;
welcome to NSSF MOBILE
To register' write the word REGISTER leave space, enter your NSSF ID then send to 15747
Karibu NSSF MOBILE,
Kujisajili tuma neno SAJILI acha nafasi, andika namba yako ya NSSF, kisha tuma kwenda 15747

Utapata ujembe unaosema:
Welcome NSSF member to NSSF MOBILE!
Send BALANCE to get your balance, STAT. to get STATEMENT. send to 15747
utapatiwa:
your last ten contributions
Source: NSSF "PA"
 
Asante mkuu kwa info, walau nimejua fuba nililo nalo nssf. Lakinni michango 10 ya karbuni imeanzia mwezi was 9 2012 kurudi nyuma lkn Sio ishu ishu labda hawajaingiza ya karibuni
 
ishu labda hawajaingiza ya karibuni[/QUOTE]
Vp fao la kujitoa nssf procedure zikoje wajameni?
 
Mkuu asante kwa taarifa mimi binafsi nimejaribu kutuma na nimepata majibu ambayo yameniwezesha kuhakiki michango yangu lakini ni mpaka Dec. mwaka jana tu,mwaka huu hawajatuma
 
Pole sana NSSF yaani hata mkihamia digitali nyie kwisha habari yenu,wezi wakubwa mnataka kutumia hela za maskini wa Tanzania kupatia umaarufu na sasa kwa taarifa yenu ni kwamba tunahamasishana kila kona ya nchi kuwachukia nyie na kazi zenu.Hata kama mrahisishe vipi kujua salio na kila kitu nyie mnabaki kuwa mfuko wa kipumbavu katika mifuko yote ya hifadhi ya jamii humu nchini Tanzania.That is my story you take it or leave it
 
Hawa NSSF wana huduma Mbovu kuwahi kushuhudiwa. Ofisi zao za Arusha hata Vyoo hazina na Ofisi ya ajabu ajabu tu huku wao wakishusha Majengo makubwa, na kuna wamama nilikutana nao wanalalamika sana, wanaanza kufuatilia Fao la kujifungua wakiwa na Mimba ya miezi saba (7) mpaka mtoto ana anza kutembea mtu hajapata hilo fao.
 
Mkuu nashukuru sana kwa hii kitu mambo nimeyaona.

ila ingekuwa vizuri kama hii kitu ingekuwa yakupa balance na tarehe ya mwisho kuletewa mchango.

PS: Sorry; STAT statement includes the above suggested
 
Wanaonyesha michango yako peke yako au na faida fedha yako iliyopata kwa kipindi hicho?
 
NSSF ni janga la kitaifa ukitaka kujia hilo shirika ni bovu kiasi gani nenda ofisi zao popote hakunauwajibikaji kabisa kila mfanyakazi ni kama kambare hakuna mkuibwa hakuna mdogo wote hovyo.
 
Ndg wana jamii ninaomba msaada wa kuangalia michango ya NSSF kupitia simu ya mkononi.
mtu mmoja aliniambia jinsi ya kujisajili niandike Neno (SAJILI acha nafasi NSSF namba ya MWANACHAMA kisha nitume
kwenda namba 15747,:A S 576: lakini nimejaribu mara nyingi wananiambia niangalie namba yangu vizuri, nami ninauhakika na namba yangu naombeni kama kuna njia nyingine mnisaidie ,
 
wadau heshima kwenu
samahani, naombwa kujuzwa kama kuna mdau anafahamu jinsi ya kuangalia michango yako iliyopo nssf kwa kupitia simu yako ya mkononi, msaada tafadhali.

Natanguliza shukrani.

Andika (SALIO number ) tuma 15747, kama hujasajiliwa watakupa maelezo ya kujisajili.
 
Pole sana NSSF yaani hata mkihamia digitali nyie kwisha habari yenu,wezi wakubwa mnataka kutumia hela za maskini wa Tanzania kupatia umaarufu na sasa kwa taarifa yenu ni kwamba tunahamasishana kila kona ya nchi kuwachukia nyie na kazi zenu.Hata kama mrahisishe vipi kujua salio na kila kitu nyie mnabaki kuwa mfuko wa kipumbavu katika mifuko yote ya hifadhi ya jamii humu nchini Tanzania.That is my story you take it or leave it
Duh! Kweli mvinyo wa kale ndio ulio bora. Maneno haya umeyasema 2013 leo ni 2016 bado yamebeba ujumbe ule ule!
 
hivi naweza pata mafao yangu bila barua toka kwa mwajiri wangu wa zaman, maana nimeangalia salio nina chochote na mm kwa sasa cpo dsm, mwenye ufaham juu ya hili naomba anipe maelekezo.
 
Iv inakuwaje mfuko huu unawakata wateja wake 10% na wakati mifuko mengine ni 5% tu japo mwajiri ni mmoja?
 
Back
Top Bottom