Kwa wanandoa!!

Kwa wanandoa!!

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
2,469
Reaction score
284
We na mkeo mmeanza maisha na wote, mwafanya kazi sehemu tofauti na huwa mnaondoka alfajiri kwenda mihangaikoni na mnatumia daladala. Kila siku kuna jama anapita na gari lake na mkeo anakuambia anamfaham na anafanya shughuli zake jirani anapofanya kazi na anamsifia alivyo mkarimu. Siku moja mpo kituoni asubuhi anapita huyo jamaa na gari lake nae anajitolea kumpa lifti mkeo...
Kama mumewe utafanyaje?
 
Akimpa mkeo lifti wewe unakuwepo au? Kama upo naye basi mnapanda wote.Tatizo liko wapi hapo?
 
Cha msingi uaminifu tu. Kama mkeo si mwaminifu, atagawa tu, hata bila ya lift.

Wakati mwingine kugawa ni hobby, haiitaji sababu!
 
NA WEWE UNAPANDA TENA MBELE unaweka na kishoka babu haaaaaaaaaaaaa wenyewe safari inaenda!!!!!!!
afu unamwomba kidogo akupitishe apo kona kuna kitu waenda cheki wasmama km dk 20 ivi then unarudi unawaambia sor
kesho hatarudia tena akikuona umesimama na mkeo atapita uyoooooooooooooo atajua haupendi!!!!
 
sijaona tatizo so far,
au labda maelezo hayajitoshelezi
 
Cha msingi uaminifu tu. Kama mkeo si mwaminifu, atagawa tu, hata bila ya lift.

Wakati mwingine kugawa ni hobby, haiitaji sababu!
Ni kweli ila ikipatikana sababu huenda asiye mgawaji naye aweza shawishika kugawa....Pa1 sana.
 
NA WEWE UNAPANDA TENA MBELE unaweka na kishoka babu haaaaaaaaaaaaa wenyewe safari inaenda!!!!!!!
afu unamwomba kidogo akupitishe apo kona kuna kitu waenda cheki wasmama km dk 20 ivi then unarudi unawaambia sor
kesho hatarudia tena akikuona umesimama na mkeo atapita uyoooooooooooooo atajua haupendi!!!!
Yaani hapa Rose u nailed it. Hii ndo solution haswaaaaaaaaaaa.
 
Unamuacha apande that day manake ndo kijana mwema keshatoa ombi but mkifika home unampiga stop aache kupanda lift ya huyo kaka au mwengine yoyote

usipende kujiweka katika mazingira yatakayo mruhusu mkeo kuwa karibu na njemba hata mkeo awe mwema vipi
 
Akimpa mkeo lifti wewe unakuwepo au? Kama upo naye basi mnapanda wote.Tatizo liko wapi hapo?

...Wos, nadhani alisema wanafanya kazi sehemu/maeneo tofauti. I can imagine wapo magomeni usalama, mume anafanyakazi Nyerere road, mke Sayansi-mwenge!
mnh,....uwezo mtihani, yataka moyo!
 
Hebu fafanua kidogo, wakati anapita hakumwona na yule kaka? pia huyo dada alimfahamia wapi huyo bwana?
 
Unamuacha apande that day manake ndo kijana mwema keshatoa ombi but mkifika home unampiga stop aache kupanda lift ya huyo kaka au mwengine yoyote

usipende kujiweka katika mazingira yatakayo mruhusu mkeo kuwa karibu na njemba hata mkeo awe mwema vipi

...aaarrghhh, kuna wengine ukimpiga stop ndio atakuwa anapanda hiyo lifti na kushushwa kwa kujificha ficha.
Binafsi; "nitamkabidhi 'mchawi' mtoto amlee!",....aje amchukue asubuhi na jioni amrudishe hapo nyumbani.
 
Hahaha mbu wachawi wa zamani wangeona haya kumtoa kikoa 'mtoto ulokabidhisha Ila wachawi wa sasa wanaona ndo wamerahisishiwa njia. Sikushauri kufanya hivyo hata kidogo
 
Hebu fafanua kidogo, wakati anapita hakumwona na yule kaka? pia huyo dada alimfahamia wapi huyo bwana?
Swali limelenga upande mmoja. naona hebu tuchangie pia ikiwa mwanamke ndo ana gari na mume anamsifia mkewe kuwa dada yule tunafanya nae kazi karibu ni mkarimu kama nini na asubuhi anawakuta wanandoa hao anawapa lift. Hii imekaaje. Maanaake naona watu wanawashambulia tu wanawake
 
Kwanza, mimi ningemwambia mke wangu sitaki kusikia tena habari za huyo jamaa - mkarimu n.k. je, kabla ya lifti alimkirimia nini? Lunch? Pili, kama mke wangu atataka hiyo lifti basi ahamie kwa huyo jamaa mpaka mwisho wa maisha yake duniani ili aweze kufaidi hiyo lifti vizuri. Tatu, nikigundua wanapeana lifti bila mimi kujua nitamchukua mke wangu na kujifanya kumtembelea huyo jamaa nyumbani kwake na kumwacha huko mke wangu - yaani kumkabidhi kwa huyo bwana. Nne, wanawake wengi upenda magari aidha kumiliki au lifti. Na mwisho, ni wote wawili ni kuka chini na kutafuta la kwenu kama si ya kwenu; maanake kama anatamani gari, lazima atatamani na vingine!!! Mwisho kabisa wake wanatakiwa kuangaliwa na kuelekezwa na waume zao kama mzazi anavyomwelekeza mwanaye!!!!!!!
 
Swali limelenga upande mmoja. naona hebu tuchangie pia ikiwa mwanamke ndo ana gari na mume anamsifia mkewe kuwa dada yule tunafanya nae kazi karibu ni mkarimu kama nini na asubuhi anawakuta wanandoa hao anawapa lift. Hii imekaaje. Maanaake naona watu wanawashambulia tu wanawake

Hii ni mbaya zaidi; mume kutamani lifti au gari la mwanamke ni aibu!!!
 
sijaona tatizo so far,
au labda maelezo hayajitoshelezi

Tatizo lipo , we huna gari lakini jamaa analo, Si unajua tena kwa mtu mwingine hiyo ni sababu toosha ya kumpunguzia confidence.
 
Akimpa mkeo lifti wewe unakuwepo au? Kama upo naye basi mnapanda wote.Tatizo liko wapi hapo?
WOS,
Hapo mi naona mambo mawili ya msingi , moja ni kwamba jamaa hana gari, na hiyo inamfanya analoose confidence kwenye ndoa yake, Pili huyo mwanamama na jamaa mwenye gari wanafanya kazi pamoja, kwahiyo hiyo inamfanya jamaa ashuku kuwa jamaa mwenye gari anaweza kumuiba mkewe na kwenda naye kokote.
 
Back
Top Bottom