Kwa wanaofuatilia muvi za Kibongo.

Kwa wanaofuatilia muvi za Kibongo.

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Kwa wadau mnaofuatilia muvi za kibongo.
Huyu jamaa ni maarufu sana kwenye ulimwengu wa muvi za kibongo anaitwa Rey.
Nashangazwa na kitu kimoja tu.
Hivi hawezi kuigiza katika hali ya kawaida ya maisha au hata kuigiza fukara?
Kila muvi zake ni lazma aigize tajiri tu?


file486.jpg
 
tatizo la muvi za kibongo hazina uhalisia na hapo ndo wanapokosea sana
 
Heeee heeee wasanii wa Bongo wana mambo, kuna mmoja huyo huwa yupo kwenye tangazo la channel 5 eti anasema yeye akipewa kucheza kama house girl abadani hatofanya huo ujinga kwa hiyo wenyewe wanataka scene za kitajiri au kichangudoa lakini za ukulima au upolisi uhaousegirl au ufungwa hawataki ndio maana daima movi zetu hazitokaa zifike mbali. Kanumba daima anaiga mambo ya kinaija eti anashika na bakora na makobazi kama wa 9ja na jinsi ya kung'aka ni exactly kama wa 9ja. Movi zenyewe zatoka kila week hadi zachosha maana hujaangalia toleo jipya mara zishatoka 3 juu yake.
 
Kitu kimoja kuhusu Ray, akiact anasound ana act, yaani too superficial, hawezi kuigiza reality. Pia ugonjwa mwingine mkubwa unazikabili movies za kibongo, ukiachilioa madhaifu mbalimbali ya quality na ulipuaji, pia wanaiga mno za Nigeria majumba ya kifahari, magari etc, life style ambao sio ya Mtanzania wa kawaida.
 
kwa kifupi watunzi na wakiigizaji wa muvi za kibongo wamefirisika kimawazo, kwani ukiangalia muvi tatu tofauti laikini scene nyingi zinafanana tofauti iliyopo ni title.
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa la muvi za kibongo!hazina uhalisia kabisa wa maisha ya kawaida ya mtanzania wa hali ya chini,ambaye hana uhakika wa milo angalau mitatu kwa siku!
 
Mimi nadhani ni stage of maturity ya industry.

Mpaka pale wasomi watakapoingia kwenye hii fani ndipo tutakapoanza kuona mazuri kwa sasa ni njaa na kujisifu zaidi. Lakini tatizo kubwa la wasomi wanadahani kuigiza huwezi kuwa na digiriii - kila mtu anawaza kuajiriwa - this is bulllll shit !!!!!!!!!!!!!!!!!!! the CCM effect
 
nadhani ni mwanzo tu baadae mambo yatakaa sawa kila kitu mwanzoni kinakuwa kigumu sana kutokana na upya kwa hiyo nadhani ni mwanzo mzuri na si movie zote ni mbaya mm uwa naziangalia hizi movie kuna baadhi ni nzuri tu kama "this is it" ya Kanumba ni nzuri ukiiangalia na nadhani mpk sasa ndio movie nzuri kwa movie nilizoziona Bongo, pia kuna nyingine ilinivutia inaitwa Perfect wife ya Nice nayo ni nzuri

unajua hii industry bado ni mpya na inakua hivyo inatakiwa tuipe support kama tulivyofanya kwenye Bongo Flava ili nayo ikue na kupata kusimama kama ukienda nchi kama Rwanda au Burundi hizi movie zinakubalika na zinauzika haswa kwa hiyo nadhani haya mapungufu madogo yafanyiwe kazi ili tuweze kupiga hatua

ukiangalia DSTV African Magic Movies utakuta ni za Nigeria na Tanzania ndio zinaonyeshwa kwa wingi kwa hiyo ni hatua kubwa sana wamepiga ktk hii industry na hata haya majumba ya kifahari yanayoonyeshwa kuna funzo pale tunapata kuhusu aina za nyumba nzuri na facilities zake mimi binafsi zimenisaidia sana kujua kuhusu ujenzi wa nyumba bora

kwa maendeleo ya hii sekta naomba tuiangalie katika jicho chanya ili iweze kukua na kufunika Africa nzima na nina imani sekta hii inalipa kuliko muziki na pia ni rahisi kuitangaza kwa kuwa movie zetu zinapata sana shavu DSTV

Watanzania tujaribu kusifu na vyetu kwani kupenda vya nyumbani ni mwanzo mzuri wa kuwainua hao wasanii ili wakue na kujulikana dunia nzima tukianza kuponda watakata tamaa na kukosa nguvu ya kuendelea
 
kitu kanumba ndio maana anafagiliwa ukilinganisha na hao wengine.aanaigiza mkulima,dereva big up kanumba.
 
Hapa leo mmejadili jambo constractive. Sasa ninyi wahusika wa industry ya filam kamni hapa msome hizi koments af mzifanyie kazi.
 
Jamani kwa nini muvi za kibongo Title zake nyingi sana ni za kiingereza wakati muvi ni ya kiswahili? Pia wanachomekea sentesi za kiingereza broken. Kuhusu ubora wa picha siku wanajitahidi sana ukilinganisha na miaka iliopita.
 
Huwa sipendi kumuangalia kwani ni too superficial!
 
Ndibalema, ameshaigiza fukara movie moja alicheza na johari, yeye alikuwa mvuvi masikini, akamuoa johari, baadae akapotelea baharini wakajua amekufa, kijana tajiri akamtokea Johari akamuoa, ndipo baadaye Ray akaibuka na umasikini wake ule ule kutaka kumkomboa mkewe.
correction plz!
sio johari ni irine uwoya na muvi iliitwa shakira.
 
Mimi nadhani ni stage of maturity ya industry.

Mpaka pale wasomi watakapoingia kwenye hii fani ndipo tutakapoanza kuona mazuri kwa sasa ni njaa na kujisifu zaidi. Lakini tatizo kubwa la wasomi wanadahani kuigiza huwezi kuwa na digiriii - kila mtu anawaza kuajiriwa - this is bulllll shit !!!!!!!!!!!!!!!!!!! the CCM effect

hata mvua isiponyesha utasema ni C.C.M effect........sio kihivyo!
 
Jamani kwa nini muvi za kibongo Title zake nyingi sana ni za kiingereza wakati muvi ni ya kiswahili? Pia wanachomekea sentesi za kiingereza broken. Kuhusu ubora wa picha siku wanajitahidi sana ukilinganisha na miaka iliopita.

title za kiengereza zina mvuto kuliko za kiswahili.............wengi tunavutiwa na title..........mfano...MORE THAN PAIN...INGEKUWA ZAIDI YA MAUMIVU ISINGEVUTIA KUNUNUA.
 
Back
Top Bottom