Kwa wanaofuatilia muvi za Kibongo.

like you name, faithful. unadhani wangapi tanzania hii wanaojua kiingereza. market yao kubwa iko bongo na wengi ni waswahili waliokosa fursa ya kusoma kama, hebu toa upuuzi wa mvuto and be real F..ful.
 
Waigizaji wapo hakuna watunzi. Story za kitoto sana.
 
Naskia waigizaji wa bongo wana pesa kuliko wanamuziki (wabongo).
 
like you name, faithful. unadhani wangapi tanzania hii wanaojua kiingereza. market yao kubwa iko bongo na wengi ni waswahili waliokosa fursa ya kusoma kama, hebu toa upuuzi wa mvuto and be real F..ful.
binafsi mimi napenda sana muvi za kibongo....na mara nyingi napita madukani kununua jina la muvi linanivutia sana....kwa upande wangu na hayo ma title ya kidhungu yanani shika.....kwa mfano best wife...ingekuwa mke bora nisingenunua.....huyo ni mimi faithful na huo ndio ukweli wangu
upuuzi wangu mimi kwa raha zangu!
 
halafu mavazi yao wanayovaa haswa wadada kama uwoya,anti ezekiel,jacky wa chuzi etc hayaridhishi ni nusu uchi hata kama ni uzungu wanatia aibu!
 
Hapa ndipo penye point, huwezi kurekodi movie kila week na ukaweza fit scene zaidi ya moja. Watu huwa wanachukua muda sana kama vile kufanya diet ili uendane na scene ya movie hiki si kitu cha wiki moja. Sasa haiingii akili mtu mwenye kitambi na nywele za relaxer huku amenyoa O aweze kuleta uhalisia kwenye scene ya mtu masikini au mtu wa kijijini ni dhahiri akifanya hivyo ataonekana too acting.
 
all in all wanajitahidi .. sana tu! ... mi napenda kweli movie zao, wakiigiza umaskini / utajiri bt kila mwaka wanaimprove badala ya kurudi nyuma
 
title za kiengereza zina mvuto kuliko za kiswahili.............wengi tunavutiwa na title..........mfano...MORE THAN PAIN...INGEKUWA ZAIDI YA MAUMIVU ISINGEVUTIA KUNUNUA.

Sikujua - kumbe!
 

...Kuna muandishi mmoja anayeReview movie kwenye gazeti la Guardian Jumapili aliwahi kuireview hii sinema unayosema na kuikososa kuwa jamaa aliekti kama mvuvi masikini lakini alikuwa haonyeshi kabisa kama ni masikini sababu mojawapo ikiwa ni kuwa na nywele zilizowekwa curl!

 

...kilele cha inferiolity complex yetu sisi wabongo na lugha yetu ya kiswahili! Sinema moja ya Kiswahili lakini title ikiwa ya kizungu itanunuliwa zaidi kuliko ile yenye title ya kiswahili!
 
pamoja na muonekano wake siyo mbaya kama akiigiza kama bosi au tajiri, sasa fikiria ray na muhogo mchungu wanaigiza pamoja nani atafaa kuwa tajiri na nani atafaa kuwa mkulima?
 
movie zipi? Hizi wanazopenda mahousegirl huku kwetu?

Nimejaribu kuangalia baadhi lakini kila moja inaniondolea sababu ya kuzipenda. Ukiangalia movie kama NERIA ni ya zamani lakini unajisahau kama ni movie.
Kutumia tittle za kiingereza haina maana mbona Nsyuka,Mama mwenye Nyumba,Misukosuko(angalau ina mvuto),Mtoto wa Mbwa,Baraka,Odama,nk. Zinafanya vizuri tu?

Pia ukiritimba ni mkubwa. Mtu awe starring,producer,director,mmiliki wa kampuni,writer/editor,halafu akubali kuigiza umasikini?

Hivi Arnold Schwarzeneger au Rambo wana Filamu ngapi. Hapa si ajabu mtu kucheza filamu 6 ndani ya mwaka 1.

Na kuhusu mada husika kwani hamna zaidi ya mapenzi na uchawi? Mbona sioni picha inahusu siasa,michezo au vita?
Matukio yana uongo kuliko picha za kihindi. Hivi,ile damu yao wanatumia tomato sauce au fruto? Siielewi.

Bongo hatuna filamu tuna picha za maigizo ndio maana huwa hazina mwisho. Pia kuna uhaba wa mawazo na creativity.
Ninavyojua ukiangalia filamu hadi mwisho hupaswi kubaki na maswali. Wanachukulia mambo kirahisi mno nadhani ni kutokana na uhaba wa bajeti.
 
Ilitoka mada fulani juu ya MUVI ZA BONGO humu, tukaweka maoni yetu tukaambiwa TUNAWAONEA WIVU!!

Kwa kifupi senema za kibongo ni aibu tupu; hakuna uhalisia wa matendo, halafu sasa hivi wanachofanya ni kuangalia movies za kinaijeria kisha wanabadilisha mazingira na kuzifamya za TZ....Ni aibu na inasikitisha!! Tuwaombee waelimike, maybe watachange!!
 
Mimi binafsi kinacho nichosha hawa jamaa ni hadithi za mapenzi tu amna lingine la maana. Hivi wanaelewa impact za hizi senema zao kwa watoto au la Kha. Si ajabu ndio kitu watanzania wanachofikiria all the time ngono tu, na mambo ya kipuuzi puuzi leo ndio unakuta mijitu ina mitoto hata uwezo wa kuiangalia aina kisha social pressure kwa upande wetu huku welfare. Ujinga mtupu hizi sinema hazi funzi bali zina stigimatize the lifestyle of pathetic people.

Its about time people have to tell different stories sio huu upuuzi wa hawa jama na yule Majuto na kundi lake. Kha ebu angalieni hata sinema za kenya zina afadhali lakini bongo ni pumba na mwenye kukasirika akasirike hila ndio ukweli wenyewe. Hadithi za sijui mke wangu apati mimba, sijui mume kamtema mkewe baada ya hela and so forth along the love lines and matrimony issues. Kha yaani amna different na jukwaa la mapenzi JF upuuzi mtupu.
 
Mi huwa huyu jamaa ananiacha hoi linapokuja suala la kiingeledha...kwani lazima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…