Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jana Jumamosi habari zilianza kuenea katika maeneo mbalimbali nyumbani hasi miongoni mwa vigogo kuwa Balali amefariki. Simu zikapigwa na sisi wengine ambao tunaelewa hali ya mgonjwa tukashtushwa. Labda ni kweli mnataka afe ili aende kwa muumba na siri zenu. Bahati mbaya mpango huo hadi hivi sasa ahera madukani wameuharisha na akirudisha namba yake itakuwa ni kwa kibali cha Aliye Juu. Sasa acheni kumchuria msije mkalazimisha kutimiza unabii wenu wenyewe. Kule kwetu huo unaitwa uchuro! Nawashauri mtangulie nyinyi kwanza lakini baada ya kusema siri zenu! Na mtake msitake atarudi nyumbani na kama kuna mashtaka yoyote ambayo mko tayari kuyaandaa mjue kabisa hatasimama kizimbani peke yake! Mmelikoroga wenyewe, sasa mtalinywa! Tuliwaambia mkatuona siye tuna wivu..
Invisible na Mwanakijiji mnatuchanganya jamani nani mkweli kati yenu.
mwangine ana sema hatunaye,mwingine anasema kuwa kaibuka na kusema.
Jamani trusted source kama hii haiwezi kuwa na habari zinazokinzana kama hizi...hasa kwa wanachama nguli kama hawa?Please
Gavana wa Benki kuu Tanzania