Ni iron tablets au vidonge vya kuongeza damu.
Kwanza kabisa folate or folic acid sio Iron tablets .
Ni B vitamin ambayo inasaidia ukuaji wa mtoto miezi mitatu ya mwanzo. Kama unajitayarisha kupata mimba huwa Dr wana recommend kuchukua folic acid mwezi kabla hujashika mimba na mpaka wiki 12 ndani ya ujauzito. Lakini kama umeshapata mimba na iko chini ya miezi mitatu huwa wakupa folic acid ya miezi mitatu na unachukua kidonge Mara moja kwa siku kwa muda wa miezi mitatu.
Folic acid inasaidia nini ?
Inasaidia ukuaji na uungaji wa viungo vya mtoto ndani ya ile miezi mitatu ya mwanzo. Ukuaji wa vitu muhimu kabisa kama brain, spinal cord, etc. ugonjwa mkubwa unaotokea Mara kwa Mara unaitwa Spina bifida. Huu unatokana na spinal cord kutojiunganisha vema. Na hii itasababisha mtoto kuwa paralysis of their lower limbs na watoto wengine huwa kwenye wheelchair na pia mtoto anaweza kuwa na tatizo ya njia kubwa na njia ndogo .
anencephaly Ni ugonjwa unaotokana na ubongo ambao haujakuwa na watoto wengine wanazaliwa na fuvu ndogo (incomplete ) watoto wanaoAliwa na huu ugonjwa wengi wao wanaishi masaa machache tu na wanaofikia ukubwa huwa wana kuwa na disability fulani.
Kwa kifupi kabisa kila siku binadamu tunachukua folate/ folic acid kwa sababu tunakula mboga za majani, machungwa na citrus fruits nyinginezo, wholemeal bread, yeast, maini etc .
Mtu mzima anatakiwa kuchukua 400 micrograms Ya folic acid kwa siku . Lakini ukiwa mjamzito unatakiwa kuchukua 600 micrograms. Na saa nyingine ni vigumu kujua kama unachukua kiasi hicho ukiwa mjamzito ndio maana wanakupa vidonge kuhakikisha unachukua the right amount kwa ujauzito .
Nchi zote zilizoendelea ukienda tu kumuona Dr. Mara ya kwanza ukiwa mjamzito au kama unajiandaa kupata ujauzito wanakupa (Folic acid na iodine tablets)
Nitaaeleza kuhusu iodine kwa kirefu baadaye.