Kwa wanaojua protokali ni Sahihi mtu mwenye umri mkubwa kumsalimia mtu aliyemuzidi cheo (status), mkubwa kicheo?

Kwa wanaojua protokali ni Sahihi mtu mwenye umri mkubwa kumsalimia mtu aliyemuzidi cheo (status), mkubwa kicheo?

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Wakuu habari za Muda huu?

Naomba mwongozo juu ya yupi anayepaswa kumsalimia mwenzake ikiwa mmoja ana umri mkubwa kumliko bosi wake,mfano Mimi niwe na umri wa miaka 50 harafu bosi wangu ninaye mzidi umri awe na chini ya umri wangu,Je yupi anapaswa kutoa salamu ya shikamoo Kwa mwenzake?

Nimeuliza hili swali kwani juzi kazini kwangu tulitembelewa na mkuu wetu wa idara ,alipofika hakuweza kumsalimia mkuu wetu ambapo Kwa umri amebakiza miaka miwili astaafu,na mkuu wetu wa idara umri wake hauzidi miaka 45. Nilibaki kushangaa bila majibu!

Lakini pia Kuna siku nilitembelea ofisi za umma Kwa wakuu wangu wa kazi ,nilipofika ndani nilikuta watu wa rika langu ,Kiufupi sikutoa salamu ya shikamoo ,niliwasalimia habari za kazi tu,Lakini kitendo kile kiliwakera baadhi Yao,

Hivyo napenda kufahamishwa kipi ni sahihi juu ya salamu ya shikamoo Kwa mkubwa wa umri na mkubwa wa cheo!!!

Wasalaamu!!
 
Habari ya Asubuhi/Leo ndiyo Salamu yangu kuu..

Shikamoo nampa Mtu ninayeona kabisa amenizidi umri tena by far.. Mtu nikimkadiria kuwa huenda tumelingana kiumri siwezi mwambia Shikamoo, hata kama nitaambiwa huyu ndiye Rais au Mfalme wa Dunia yote....

Shikamoo - Umri ✓
Shikamoo - Cheo ×
 
Senior hawezi msalimia junior,hiyo kesi zipo maafisi mengi utakuta Kwa mfano kwenye walimu,Kuna mwalimu aliwahi kuwa head akaja kakatolewa kawekwa mwingine Sasa huyu mpya hua anatakaga kumpelekesha yule wa zamani.
Hapo ndo unakuaga mtiti.
 
Sema waalimu wako petty(wana gubu) sana

Hata mleta mada ni mwalimu

Shida nini?
 
Mimi mabinti wazuri wakiniamkia nawaambia Asante! Maana hizo ni dariri za kunyimwa vitu vizuri.
 
Wakuu habari za Muda huu!!!?

Naomba mwongozo juu ya yupi anayepaswa kumsalimia mwenzake ikiwa mmoja ana umri mkubwa kumliko bosi wake,mfano Mimi niwe na umri wa miaka 50 harafu bosi wangu ninaye mzidi umri awe na chini ya umri wangu,Je yupi anapaswa kutoa salamu ya shikamoo Kwa mwenzake!!?

Nimeuliza hili swali kwani juzi kazini kwangu tulitembelewa na mkuu wetu wa idara ,alipofika hakuweza kumsalimia mkuu wetu ambapo Kwa umri amebakiza miaka miwili astaafu,na mkuu wetu wa idara umri wake hauzidi miaka 45. Nilibaki kushangaa bila majibu!

Lakini pia Kuna siku nilitembelea ofisi za umma Kwa wakuu wangu wa kazi ,nilipofika ndani nilikuta watu wa rika langu ,Kiufupi sikutoa salamu ya shikamoo ,niliwasalimia habari za kazi tu,Lakini kitendo kile kiliwakera baadhi Yao,

Hivyo napenda kufahamishwa kipi ni sahihi juu ya salamu ya shikamoo Kwa mkubwa wa umri na mkubwa wa cheo!!!

Wasalaamu!!
Binafsi
Salam ya shikamoo nimeanza kutoipenda. Ninaitumia kwa watu wachache sana kinafki and selectively.
 
Kuna taasisi mnaoneanaga kijinga sana sababu mnaleteana mafadhaiko yakijinga sana. Ulivyosalimia ilitosha sana mkuu🙂🙂 .

Thus, Sehemu za watu wengine Salam ya shikamoo ni wewe kupenda. Aliyeweka Jambo Sir/af. alimaliza vizuri😊😊😊.
 
Binafsi namsalimia yoyote aliyenizidi umri bila kujali cheo,kipato ama Elimu,mfano nina wafanyakazi anawake wamemzidi umri mama yangu kwa takribani 8 years why nisiwape heshima yakula chumvi?,Cheo au uboss ni dhamana yakawaida sana kwa waliopevuka
 
Jiulize tu, kule G8, kuna viongozi wenye umri mdogo ukiringanisha na wengine, je wakikutana kwenye vikao vyao, mdogo kiumri huwa anamsalimia mkubwa?
 
Kutoa salamu kwa wakubwa waliokuzidi kiumri, inatafsiri wewe ni mstaarabu na unayejali utu.
Unaweza kumwamkia ''shikamoo mzee, familia iko powa lakini....'' baada ya hapo unampa majukumu anaendelea na kazi yake.
 
Back
Top Bottom