Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 200
RAIA MWEMA
Septemba 15, 2010Nchi, demokrasia inayumba kwa Katiba iliyopitwa wakati [1]
NIANZE kwa hitimisho kwamba Tanzania, tangu uhuru hadi sasa, haijawahi kamwe, kuwa na Katiba inayotokana na ridhaa ya wananchi; kwa maana, Katiba zote nne zilizowahi kutumika, ikiwamo ya sasa, zilitokana ama na shinikizo la watawala madarakani, au la vikundi vya kitabaka visivyowasilisha matakwa na hisia za wananchi, lakini vyenye kuhodhi mamlaka ya kuamua mustakabali wa Taifa.
Na kwa kuwa Katiba zote zimewakilisha daima matakwa na maslahi ya kitabaka, kwa sababu hiyo zimeshindwa kudumu kama zilivyo kwa muda mrefu kwa sababu ya kuzua mitafaruku ya ndani na kuashiria mabadiliko yasiyoepukika. Marekebisho ya Katiba hizi kwa njia ya viraka lukuki, yameshindwa kuziokoa kwa sababu ya wakati ukuta.
Tanzania imepitia Katiba nne tangu uhuru, ambazo, licha ya viraka zilizofanyiwa kujaribu kuokoa hali, ni nyingi mno kwa idadi kwa viwango vya mabadiliko ya Katiba barani Afrika kuashiria hamkani si shwari tena. Kila badiliko (lisiloepukika) liliashiria kupitwa wakati kwa Katiba hiyo na kwa aina fulani ya mfumo wa utawala na mustakabali wa Taifa kwa ujumla.
Katiba hizo ni kuanzia na Katiba ya Uhuru [1961], Katiba ya Jamhuri [1962], Katiba ya Tanganyika na Zanzibar [1964], Katiba ya Muda ya Tanganyika na Zanzibar [1964], na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, ambayo nayo, kwa shinikizo la mazingira ya sasa kisiasa na kiuchumi, haina budi kupisha Katiba mpya, tena haraka sana.
Katika makala haya, nitaelezea chimbuko la kila Katiba na sababu za kufutwa ili kupisha Katiba mpya; na kwa nini Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kusimama kwa miguu miwili.
Tujiulize: Kwa nini tabaka la sasa la watawala na wanasiasa uchwara wanatetea kuendelea kwa Katiba hii, wakati wakielewa na kuamini fika, kwa roho na mwili, kwamba haikidhi matakwa ya sasa ya wananchi, lakini wanaropoka juu ya paa kutetea wasichokiamini? Na kabla hatujaendelea tujiulize pia: Katiba ni nini?
Kwa mtazamo na fikra za Kileberali, Katiba ni vitu viwili: Kwanza, ni ramani ya mamlaka inayotoa na kufafanua jinsi mamlaka ya nchi yanavyopaswa kuwa na kugawanywa ndani ya vyombo vya nchi.
Pili, Katiba ni mandhari (terrain) ya mkataba wenye kuhalalisha uhalali wa kutawala na utawala; ndiyo pia inayotoa itikadi na misingi ya Kikatiba na Kanuni (doctrines) kama vile mgawanyo wa madaraka, uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria na kadhalika.
Kuzingatiwa kwa mambo haya yote kunajulikana kama constitutionalism, kwa maana ya imani kwamba serikali (kwa kupenda au bila kupenda) inazingatia misingi na matakwa ya Katiba kwa manufaa ya wananchi wote.
Kanuni za Katiba na constitutionalism zinaungana ndani ya Katiba, na hivyo kufanya Katiba kuwa si tu sheria mama (sheria ya msingi) ya sheria zote, bali pia msingi mkuu wa uhalali wa kutawala.
Watawala hupata mamlaka na uhalali wa kutawala kutokana na Katiba; na kwa sababu hiyo Katiba hufanya utawala ukubalike na kuheshimiwa.
Tanganyika (sasa Tanzania) ilipata Uhuru kutoka kwa Waingereza Desemba 9, 1961 chini ya Jumuiya ya Madola na kuridhia aina ya mfumo wa utawala wa Uingereza ujulikanao kama Mfumo wa Westminster.
Kwa mazingira hayo, Katiba mwafaka wakati huo ilizingatia na kujikita kwenye hali ya kumalizika kwa kipindi cha ukoloni mkongwe na kuhamishia madaraka kwa uongozi wa kizalendo chini ya Chama cha Tanganyika African National Union (TANU), kikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kama ilivyokuwa kwa nchi zote zilizotawaliwa na Uingereza enzi hizo, Katiba ya Tanganyika au kwa jina sahihi Katiba ya Uhuru (The Tanganyika [Constitution] Order in Council, 1961) ilitolewa kwenye Ofisi ya Makoloni ya Uingereza na kutiwa sahihi (to assent) na Malkia wa Uingereza Novemba 27, 1961 kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanganyika na kuanza kutumika.
Chini ya Katiba hiyo, Tanganyika ilitangazwa kuwa nchi ya Kidemokrasia yenye Vyama vingi vya siasa chini ya Waziri Mkuu [Nyerere], huku madaraka ya Malkia yakiendelea kubakia akiwakilishwa na Gavana nchini.
Chini ya mfumo huo wa Westminster, ukuu wa Bunge (Parliamentary Supremacy) uliendelea kutambuliwa na kuheshimiwa kwa kuzingatia haki na demokrasia.
Utangulizi wa Katiba hiyo ulisomeka hivi:
Na kwa kuwa haki hizo zitatekelezwa na kulindwa katika jamii ya kidemokrasia ambayo Serikali yake inawajibika kwa Bunge huru lenye kuwakilisha wananchi, ambalo Wajumbe wake ni wa kuchaguliwa na ambayo Mahakama zake ni huru na zenye kutoa haki bila woga wala upendeleo......
Kwa heshima zote, niharakishe kutamka mapema hapa kwamba, matakwa haya ya aina ya Serikali na Bunge bado yanasomeka vivyo hivyo kwenye utangulizi wa Katiba yetu ya sasa (ya 1977), lakini utekelezaji wake ni kinyume, wa dhihaka na kwa njia ya ukiukaji mkubwa wa Katiba yenyewe.
Kwa mfano, kuna ukweli gani kwamba Bunge letu ni lenye wajumbe wa kuchaguliwa (kuwakilisha majimbo na wananchi), wakati limesheheni wabunge wa kuteuliwa [na Rais] na Wabunge wa Viti Maalumu?
Kuna ukweli gani kwamba Mahakama zetu ni huru, wakati majaji wote ni wateule wa mhimili wa utawala (Rais), kiasi kwamba amlipaye mpiga zumari ndiye huchagua wimbo?
Iko wapi demokrasia ya kweli, ya kila mtu kushiriki katika uongozi wa nchi, wakati demokrasia imefungwa kwenye jela ya vyama vya siasa, ili mradi kwamba mtu hawezi kugombea nafasi ya uongozi wowote nchini (urais, ubunge, udiwani) isipokuwa kupitia vyama vya siasa, kana kwamba wananchi hawana uwezo wa kufikiri na kutenda nje ya vyama vya siasa?
Katiba ya Uhuru ya Tanganyika ya 1961, ilikuwa na upungufu mmoja mkubwa, tofauti na Katiba za nchi huru nyingine za Kiafrika enzi hizo: haikuwa na ibara kuhusu Haki za Binadamu, inadhaniwa hiyo ilitokana na kupitiwa tu kwa Watunga Katiba wa Uingereza!.
Chini ya Katiba hiyo ya Uhuru, nchi ilikamatwa na kuongozwa na viongozi wa tabaka dogo la vibwenyenye wadogo wadogo [petty bourgeoisies], likiundwa na waliojiita wanaharakati wa mapambano ya uhuru; wakiwamo viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara wa ngazi za kati, wanaharakati wa vyama vya ushirika, waalimu na watumishi wa serikali wa ngazi za chini.
Kama ambavyo ilivyo sasa, ambapo makundi haya yamecharuka kuvamia nafasi ya uongozi wa siasa (ubunge na udiwani), ndivyo ilivyokuwa enzi za uhuru, na kusema kweli historia inajirudia, kwa wananchi wa kawaida (wasio na ubavu kifedha na kujuana) kugeuzwa watazamaji tu kwa yanayotokea nchini.
Matokeo yalikuwa ni nchi kushikwa na kuongozwa na tabaka la vibwenyenye lenye sera zisizo na mashiko, wala mkakati endelevu katika nyanja za kiuchumi na kisiasa. Kwa kifupi, tabaka hili lilishika na kuridhia tu mfumo kandamizi wa zamani wa kikoloni kutumikia matakwa ya kikoloni, kwa jina lingine ukoloni mamboleo.
Kwa mfano, chini ya Katiba hiyo, vibwenyenye hao walishindwa kuvunja/kufuta mfumo wa uzalishaji wa kinyonyaji ndani ya nchi na uhusiano wake na ubepari wa kimataifa. Kwa sababu hii, uhuru [wa bendera] kwa mwananchi wa kawaida haukuwa na maana kwake.
Kutokidhi kwa Katiba hiyo na matarajio ya wananchi kunathibitishwa na migomo mingi na mikubwa enzi hizo katika mashamba makubwa ya makabaila, iliyoongozwa na Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), kiasi kwamba mmoja wa viongozi wakuu wa shirikisho hilo, Victor Mkelo, alipelekwa uhamishoni (mafichoni) katika maeneo duni ya mmoja wa Mikoa ya Magharibi kwa miezi mitatu.
Hapo Serikali ikaweza kuzima migomo kwa nguvu za dola; TFL ikafutwa, badala yake ikaundwa Jumuiya ya Wafanyakazi (National Union of Tanganyika Workers) NUTA, kama chama cha propaganda kwa wafanyakazi wenye njaa ndani ya nchi yenye utajiri wenye kunufaisha vitabaka.
Haikuishia hapo, mwaka 1962, Serikali ikafuta vyama vikuu 34 vya Ushirika na Vyama vya Ushirika vya Msingi 850 vilivyokuwa vinazalisha karibu asilimia 25 ya mazao ya ndani kwa soko la nje; badala yake likaundwa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (Cooperative Union of Tanganyika CUT) kuwalewesha wakulima kwa propaganda ndani ya uchumi uliokuwa unaendeshwa kunufaisha vitabaka vya kibwenyenye vya kuibukia.
Ndani ya TANU namo mambo hayakuwa shwari. Januari 16, 1962, kwa shinikizo la wanachama wa Bara, Mwalimu Nyerere alikabiliwa na changamoto halali, kali na zenye nguvu, zikimtaka kutoa madaraka zaidi kwa Waafrika serikalini (Africanisation) na kuwaondoa wabunge wachache wawakilishi wa mataifa mengine (minority races) ili Bunge liwe la Waafrika tupu.
Wanachama hao walimtaka pia achukue hatua za makusudi kuhakikisha kasi nzuri ya maendeleo nchini; wakataka pia Tanganyika ipate madaraka ya ndani na kuitwa Jamhuri (kwa kumwondoa mwakilishi wa Malkia Gavana) haraka iwezekanavyo.
Na pale Nyerere alipoonekana kusitasita, hasa kuhusu suala la Africanisation, hali ya kisiasa nchini na kwa TANU ilianza kuwa tete, tena kwa kasi ya kutisha.
Na alipoona kwamba hamkani si shwari tena, na kwamba nchi ingeingia katika mtafaruku mkubwa, hatari na wenye madhara makubwa, Nyerere alilazimika kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu akimwachia Rashidi Kawawa kuongoza harakati, na yeye akabakia kama Mjumbe wa kawaida wa Baraza la Kutunga Sheria LEGCO.
Kufikia hapo, Katiba ya Uhuru ya 1961, iliyotambua ukuu wa Bunge na uhuru wa Mahakama bila mgawanyo wa madaraka wa aina ya mfumo wa Kimarekani, ilishinikizwa tu kurithi mfumo katili wa Kikoloni na kubakia kama ulivyokuwa kabla ya Uhuru. Na kwa sababu hayo hayakuwa matarajio ya umma wa Tanganyika kuhusu uhuru waliopigania, Katiba hiyo haikusalimika, ikatupwa nje.
Katiba gani ilichukua nafasi ya Katiba ya uhuru? Kwa nini nayo haikudumu? Je, kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kwenda na wakati, itaweza kusalimika?
..Itaendelea wiki ijayo.

Joseph Mihangwa