Kwa wanaopendekeza serikali 3...

chicco

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
748
Reaction score
254
Ni maswali mengi sana kuhusu mchakato huu wa katiba unaoendelea ambayo yananichanganya lakini leo naomba kuanza na wanaopendekeza serikali tatu wanisaidie kujibu baadhi ya maswali plz:

1: sawa, kutakuwa na serikali ya Tanganyika,Zanzibar na Shirikisho..Je viongozi wake wakuu wote wataitwa Rais?
(kama jibu la swali hapo juu ni ndio)
(i) Mgawanyo wa mamlaka na utawala utakuwaje?
(ii) Mkuu wa majeshi atakuwa yupi?
(iii) yupi atakuwa na mamlaka ya ardhi?
(iv) Itakuwaje kama may be zanzibar akishinda cuf,Tanganyika akashinda cdm na shirikisho akashinda ccm(kwa kuzingatia uhasama uliopo baina ya vyama hivi), kuna mwongozo wowote wa kutuongoza tunapoingia kwenye mkwamo(mfano mzuri kama unaoendelea bungeni kuhusu kura ya siri au wazi) kwenye issues zinazohusu maslahi ya kitaifa?
2: Kwa mfano mmojawapo anavamiwa na adui kutoka nje ni msaada gani atapaswa kutoa patina wa shirikisho?
3: may be kipato cha mmojawapo kinakuwa hohehahe ni mfumo gani wa financial support unatolewa(au inatumika kama sasa tunavyokopeshwa kutoka nje,may be zanzibar anakopeshwa na tanganyika)? etc etc

Jamani tunaomba wakati mnajadili mfumo wa muungano muwe mnatusaidia na kujadili na namna tutakavyoenda kwenye huo muungano.........na kama kuna mtu ana rasimu ya pili ya katiba atusaidie wengine kuileta hapa tuijadili hasa kwenye issues za muungano.
NAWASILISHA
 
Uasama upi kama kila serekali itakuwa na katiba yake kijana?usiwe kama wale wanaotudanganya serekali 3 ni garama na tujuwavyo inapunguza garama sana ila inawanyima wezi wengi ilaji na ufalme
 
Maswali yako yote yamejibiwa kwenye rasimu ya pili ya katiba ya mzee Warioba. Imechapwa hata magezetini. Hakuna jipya hapo kuianzisha hoja hii. Tupo kwenye fikra za juu zaidi ya haya uliyoyaleta hapa.
 
Maswali yako yote yamejibiwa kwenye rasimu ya pili ya katiba ya mzee Warioba. Imechapwa hata magezetini. Hakuna jipya hapo kuianzisha hoja hii. Tupo kwenye fikra za juu zaidi ya haya uliyoyaleta hapa.
unaweza kunijuza zaidi wewe uliyopo juu?start kwa kuweka link hapa ya hiyo rasimu ya katiba kwanza.lengo ni kuwajuza wengi zaidi ambao hawajui hizo details zingine kuhusu muungano.mm naweza kuwa nafahamu but kuna wengine hawajui so kuleta mjadala kama huu inaweza kuwa darasa tosha kwa wengine....
 
Maswali yako yote yamejibiwa kwenye rasimu ya pili ya katiba ya mzee Warioba. Imechapwa hata magezetini. Hakuna jipya hapo kuianzisha hoja hii. Tupo kwenye fikra za juu zaidi ya haya uliyoyaleta hapa.

mkuu sina kitufe cha like but take my like.

kwanini watu hawataki kusoma katiba ambayo ipo kila kona? watu wa aina hii hawawezi kuleta maendeleo hata atawale lipumba au slaa.
 
Ni upuuzi Tanzania Bara kulilia kuwa na Tanganyika yet wao ni waKubwa!
 
uasama upi kama kila serekali itakuwa na katiba yake kijana?usiwe kama wale wanaotudanganya serekali 3 ni garama na tujuwavyo inapunguza garama sana ila inawanyima wezi wengi ilaji na ufalme
how?fafanua mkuu
 
Ni upuuzi Tanzania Bara kulilia kuwa na Tanganyika yet wao ni waKubwa![/QUOTE
sioni ubaya wa uwepo wa tanganyika as long as tumekubaliana na kuweka misingi imara ya kiutawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…